Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 3/8 uku. 30
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wahanga wa Buchenwald
  • Dini Katika Sehemu za Mashambani za Uchina
  • Heshima Nyingi Mno?
  • Kupumua Moshi wa Mvutaji Sigareti
  • Watumiaji Wakuu wa Dawa za Kulevya Ulimwenguni
  • Wezi wa Vitabu
  • Kusumbuliwa kwa Makasisi wa Kike
  • Sigareti—Je, Wewe Huzikataa?
    Amkeni!—1996
  • Mamilioni ya Uhai Yakitokomea Moshini
    Amkeni!—1995
  • Je, Kuvuta Sigara Ni Dhambi?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Watetea Tumbaku Waanzisha Puto la Hewa-Joto
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 3/8 uku. 30

Kuutazama Ulimwengu

Wahanga wa Buchenwald

Jina Buchenwald lapeleka fikira zenye kuogopesha sana akilini mwa wale ambao wanakumbuka Nazi ya Ujerumani. Ikiwa karibu na Weimar, ambayo mpaka hivi karibuni ilikuwa Ujerumani Mashariki, Buchenwald ilikuwa kambi ya mateso yenye sifa mbaya sana katika ukatili wa kibinadamu kwa robo ya milioni wafungwa. Leo, husimama kama ukumbusho wa taifa na nyumba ya hifadhi kwa wahanga wa maovu, lakini bado kuna mabishano kuhusiana nayo. Ulrich Schneider msimamizi mpya wa ukumbusho, aliteuliwa kuinua kifuniko cha utambulisho kutoka kwa wafanya kazi watumwa 65,000 ambao walikufa huko. “Inafaa, kwa mfano, kwamba askari wa Urusi wakumbukwe hapa,” akasema. “Lakini Wafaransa wengi sana, Wabelgiji, na Waholanzi pia walikufa hapa, na uangalifu mdogo umetolewa kwao.” Alitaja pia uhitaji wa “kutoa masimulizi yenye mkazo zaidi” kuhusu vikundi vingine, kutia ndani Mashahidi wa Yehova.

Dini Katika Sehemu za Mashambani za Uchina

Wang Zhen, makamu wa waziri wa kwanza wa Uchina, asema kwamba dini za Magharibi zinaenea katika jamii za ukulima katika Uchina, kulingana na South China Morning Post na kuripotiwa katika gazeti World Daily la United Sates la lugha ya Kichina. Wang Zhen asema kwamba katika vijiji vya ukulima, ambako asilimia 70 ya wakazi wanaishi, “Watu zaidi na zaidi wanataka kujiunga na makanisa.”

Heshima Nyingi Mno?

Makundi ya United States Methodist yapaswa kutafuta njia nyingine za kuheshimu maaskofu wao badala ya kuwapa pato kubwa la kifedha. Hilo ni pendekezo la uchunguzi la shule ya kidini ya Methodist katika United States. Uchunguzi ulipata kwamba makundi kwa kawaida yanatoa zawadi za fedha zifikazo kiasi cha dola 40,000 na magari yenye kiasi cha thamani ya dola 20,000 kwa maaskofu wanaostaafu au kuhama. Laandika Christianity Today: “Kulikuwa na wakati ambapo zawadi hizo zilikusudiwa kuongezea mshahara mdogo wa maofisa wa kanisa. Lakini kwa habari ya mwaka ujao, mshahara wa maaskofu wa UM [United Methodist] utaongezeka kupita dola 66,000. Kwa kuongezea, maaskofu hupewa nyumba za bure na hupewa alawansi ya dola 41,000 kwa kuendesha ibada.

Kupumua Moshi wa Mvutaji Sigareti

Moshi unaotolewa na wavutaji tumbaku unavutwa bila kutaka na wasiovuta. Kulingana na uchunguzi wa karibuni kupumua moshi wa wavutaji sigareti sasa kunaangamiza maisha za maelfu katika Australia. Inaaminika kwamba “zaidi ya Waaustralia 1000 wasiovuta sigareti hufa kila mwaka kwa sababu ya ugonjwa wa moyo unaosababishwa na kupumua moshi wa wavutaji sigareti,” likaripoti The Australian. Gazeti hilo liliandika kwamba ‘moshi huu kutoka sigareti ya mvutaji’ una kaboni monoksaidi na nikotini, ambavyo hupunguza utendaji wa moyo na “uwezo wa damu kupeleka oksijeni kwenye moyo na sehemu nyinginezo za mwili.” Uchunguzi ulifikia mkataa kwamba “kwa kila watu wanane wafao kwa uvutaji wa tumbaku, mmoja asiye mvutaji hufa kutokana na kupumua moshi wa sigareti.”

Watumiaji Wakuu wa Dawa za Kulevya Ulimwenguni

Gazeti L’Express la Paris laripoti kwamba Wafaransa ndio watumizi wakuu ulimwenguni wa dawa za kulevya zinazoamriwa na daktari. Katika 1989, walitumia kiasi cha fedha za kifaransa milioni 90,000 (dola milioni 18,000 milioni U.S.) kununua dawa hizo, huo ni wastani wa fedha za kifaransa 1,598 (dola 320, U.S.) kwa kila mtu. Kulingana na gazeti la Kifaransa La Croix, Wafaransa hutumia dawa za kutuliza maumivu na za kusaidia kupata uzingizi mara tano zaidi ya Waamerika. Tatizo hilo limeenea na lawapata watu wa kila umri. Wengi sasa wanaogopa kwamba hatari ya uzoevu ni halisi kabisa. Mmoja kati ya wabalehe watano huondoka ofisini mwa daktari akiwa na kikaratasi chenye ruhusa ya daktari ya kumwezesha kununua tembe za kumsaidia kupata usingizi au utulivu. Asilimia ya watoto wa umri wa chini ya mwaka mmoja, hupewa kwa ukawaida dawa za kutibu matatizo ya neva na ya ulaji. Gazeti la kila siku la Le Figaro laripoti kwamba katika Ufaransa, kati ya asilimia 25 na 30 ya watu wazima ni watumiaji wa muda mrefu wa aina moja au nyingine ya dawa za kuwatuliza.

Wezi wa Vitabu

Walinzi wa vitabu na wengine katika biashara ya vitabu wanasumbuliwa na ongezeko la wizi wa vitabu. Kulingana na New York Times Book Review, Mary Ellen Quinn, mkrugenzi wa ukusanyaji na usitawishaji wa Maktaba ya Taifa ya Chicago, asema kwamba ‘kila mwaka mfumo wa maktaba labda hununua vitabu vingi kama vile vinavyoibwa.’ Baadhi ya madaktari, waandishi, mahakimu, wanaseminari, walimu, na hata watunza maktaba wamehusishwa katika orodha ya wezi wa vitabu, na mtaalamu mmoja aliita watu ambao huiba vitabu kuwa “baadhi ya watu mashuhuri zaidi ulimwenguni.” Watafiti wanadai kwamba Biblia “kwa wazi ndicho hasa kitabu chenye kuibwa zaidi, kinachopendwa zaidi ya vyote hivi kwamba watu hawawezi kujizuia kukiiba.”

Kusumbuliwa kwa Makasisi wa Kike

Katika uchunguzi uliofanywa na Kanisa United Methodist Church katika United States, zaidi ya robo tatu za makasisi wa kike wa kanisa hilo waliripoti kwamba wamesumbuliwa kingono. Kulingana na Ecumenical Press Service (huduma ya habari ya World Council of Churches), uchunguzi huo huo uliripoti pia kwamba asilimia 41 ya makasisi wa kike wa kanisa hilo walifunua kwamba kusumbuliwa kingono huko “kulitendwa na wafanyakazi wenzi au mapasta wengine.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki