Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 7/8 uku. 29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maafa Zaidi Wakati Ujao
  • Gharama Inayopanda ya Haki
  • Dawa za Kulevya Shuleni
  • Makao Mengi Zaidi ya Wanajeshi Kuliko Hospitali
  • Makosa Yenye Kuaibisha ya Kutia Tarehe
  • Bei ya Hila na Uchomaji Mali
  • Kulingana na The Times ya London, hila ya kadi za mkopo katika Uingereza hugharimu benki na majumba ya fedha pauni milioni 75 (dola milioni 150, za U.S.) kila mwaka. Na bado hata hesabu hii ni ndogo mno ikimithilishwa na gharama iliyokadiriwa ya uchomaji mali: pauni milioni 500 (dola milioni 1,000) katika 1990 pekee, wakati ambapo jumla ya hasara ya moto ilifikia pauni milioni 1,000 (dola milioni 2,000). Ingawa uharibifu wa mali unaofanywa na wanaume kutoka umri wa miaka 10 hadi 25 ndio kisababishi cha kawaida zaidi cha uchomaji mali, kufikia asilimia 20 ya visa vya uchomaji mali vinafungamanishwa na hila—biashara, magari, na makao yanaharibiwa kimakusudi ili kupata malipo ya bima. The Times laripoti kuwa takwimu za idara ya utengamano ya Serikali ya Uingereza zafunua pia kuwa shule 1,008 ziliharibiwa kimakusudi au kuharibiwa kwa kuchomwa katika 1988.
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1993
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1992
  • Pambano la Mwanadamu Dhidi ya Misiba
    Amkeni!—1995
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 7/8 uku. 29

Kuutazama Ulimwengu

Maafa Zaidi Wakati Ujao

Gazeti la Ujerumani Schweinfurter Tagblatt laripoti kuhusu taarifa ya WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni) kwamba, “Kwa sababu ya uharibifu wa mazingira, hesabu ya maafa ya asili itaongezeka sana kufikia mwaka 2000.” Kulingana na WHO, “sasa kuna maafa zaidi na zaidi ya mazingira yanayosababishwa na mwanadamu mwenyewe.” Mifano iliyotajwa ilikuwa ni maafa ya kemikali katika Bhopal (India) na Séveso (Italia), aksidenti katika vyombo vya kutengezea atomi katika Chernobyl (Urusi), mkasa wa kutona kwa mafuta karibu na ufuo wa bahari katika Alaska, na kuchomeka kwa sehemu za mafuta katika Kuwait. “Uchafuzi wa hewa, maji, na udongo, pamoja na kuharibiwa kwa utando wa ozoni na kupanda kwa halijoto la anga la dunia, kwaonyesha kuwa maendeleo ya viwanda ni yenye uharibifu,” makala hiyo yaongezea. “Watu zaidi ya milioni 50 wamepoteza makao yao kupitia maafa ya asili tangu mwanzo wa karne hii.”

Gharama Inayopanda ya Haki

Wakanada walitoa “zaidi ya dola bilioni 7.7 [milioni elfu] mwaka jana kwa polisi, mahakama, magereza na msaada wa kisheria,” laripoti The Toronto Star. Hilo lamaanisha kwamba kila Mkanada hutumia dola 295 kwa mwaka kutegemeza mfumo wa haki. Kujapokuwa na utumizi huu mkubwa wa pesa, “kiwango cha uhalifu kilipanda kwa asilimia 32,” yasema Star. Hesabu ya wafungwa gereza ilipanda kwa asilimia 37 kati ya 1981 na 1987. Akitoa maelezo kuhusu gharama kubwa ya haki, Sherry Kulman, mkurugenzi mkuu wa Sosaiti ya John Howard katika Toronto, alisema: “Bilioni saba [milioni elfu] ni pesa nyingi sana na mimi nashangazwa kuwa watu hawasemi ‘ngoja kidogo, ni nini kinaendelea?’” Yeye aliongezea: “Je! huu si wakati watu wanapaswa kung’amua kwamba mfumo huo haufanyi kazi?”

Dawa za Kulevya Shuleni

Vijana hupataje kutumia dawa za kulevya shuleni? Abílio Pereira, mkuu wa polisi katika Rio Grande do Sul, Brazili asema “Dawa za kulevya haziingizwi shuleni kwa mikono ya wageni, bali kupitia wanafunzi wenyewe,” “Hakuna mtu anayekubali dawa za kulevya kutoka kwa mtu asiyemjua.” Yeye aongezea: “Nilizoea kupata wavulana wa miaka 17 wakiwa na marijuana. Sasa tuna matatizo na wavulana wa miaka 12 na hata 10.” Kwanza, dawa za kulevya zaweza kutolewa bure katika hali ya ustarehe, lakini mara vijana wakishakuwa wazoevu, wachuuzi wanaanza kuziuza. Alberto Corazza, mkuu wa polisi wa wilaya katika São Paulo asema kwamba “Hakuna shule ambamo dawa za kulevya haziingizwi,” Gazeti Veja lasema: “Haijapata kamwe kuwa rahisi jinsi hii kununua dawa za kulevya shuleni, eneo la wachuuzi wa dawa za kulevya halijapata kamwe kuwa kubwa jinsi hii kati ya wanashule na kamwe haijapata kuwa vigumu jinsi hii kudhibiti aina hii ya biashara.”

Makao Mengi Zaidi ya Wanajeshi Kuliko Hospitali

Gazeti Demos, linalochapishwa na Taasisi ya Uchunguzi ya Viuo Vikuu vya Uholanzi liliripoti kuwa serikali nyingi kuzunguka ulimwengu hutumia asilimia 5.4 ya jumla ya mapato ya taifa katika utendaji wa kijeshi lakini asilimia 4.2 pekee kwa utunzaji wa afya. Uwiano katika nchi zinazoendelea unakosa usawa hata zaidi: asilimia 5.6 kwa ulinzi lakini asilimia 1.4 pekee kwa utibabu. Demos lasema kuwa serikali mbalimbali Kusini-Mashariki mwa Esia, ndizo za kwanza katika orodha kwa kutumia pesa mara saba zaidi kwa mambo ya kijeshi kuliko ya afya.

Makosa Yenye Kuaibisha ya Kutia Tarehe

Miaka kumi na moja iliyopita, Joan Ahrens, nyanya msanii katika Afrika Kusini, alifanyiza michoro mizuri akitumia mawe kama nguo ngumu ya kuchorea, akiiga usanii wa kitamaduni wa kabila la Bushman wa Afrika Kusini. Baadaye, moja ya mawe yake yaliyochorwa liliokotwa kwenye uwanda karibu na iliyokuwa nyumba yake katika jiji la Pietermaritzburg. Hatimaye lilifikishwa kwa mtunzi wa makao ya kuhifadhia vitu katika jiji. Bila kujua chanzo cha jiwe hilo la sanaa, mtunzi huyo alilipeleka Uingereza litiwe tarehe na Chuo Kikuu cha Oxford katika idara ya radio-kaboni. Wastadi walikadiria kuwa mchoro huo ulikuwa wa miaka 1,200! Kwa nini kuwe na kosa kama hilo lenye kuaibisha? Kulingana na ripoti katika Sunday Times ya Afrika Kusini, “imedhibitishwa kwamba mafuta ya kuchorea yaliyotumiwa na Bi Ahrens ulikuwa na mafuta ya asili yaliyokuwa na kaboni—kitu pekee kilichotiwa tarehe na Oxford.”

Bei ya Hila na Uchomaji Mali

Kulingana na The Times ya London, hila ya kadi za mkopo katika Uingereza hugharimu benki na majumba ya fedha pauni milioni 75 (dola milioni 150, za U.S.) kila mwaka. Na bado hata hesabu hii ni ndogo mno ikimithilishwa na gharama iliyokadiriwa ya uchomaji mali: pauni milioni 500 (dola milioni 1,000) katika 1990 pekee, wakati ambapo jumla ya hasara ya moto ilifikia pauni milioni 1,000 (dola milioni 2,000). Ingawa uharibifu wa mali unaofanywa na wanaume kutoka umri wa miaka 10 hadi 25 ndio kisababishi cha kawaida zaidi cha uchomaji mali, kufikia asilimia 20 ya visa vya uchomaji mali vinafungamanishwa na hila—biashara, magari, na makao yanaharibiwa kimakusudi ili kupata malipo ya bima. The Times laripoti kuwa takwimu za idara ya utengamano ya Serikali ya Uingereza zafunua pia kuwa shule 1,008 ziliharibiwa kimakusudi au kuharibiwa kwa kuchomwa katika 1988.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki