Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 11/8 uku. 31
  • Busara ya Nyani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Busara ya Nyani
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • ‘Kuendelea Kulishika Sana Neno la Uzima’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Somo la 2
    Masomo Yangu ya Biblia
  • Masomo Yangu ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Watoto ‘Kwa Kuazimwa’ Zoea Hili Ni la Hekima Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 11/8 uku. 31

Busara ya Nyani

Katika Sierra Leone, Afrika Magharibi, kuna msemo: “Nyani hamwambii tu mtoto wake, ‘Jishikilie kwa nguvu!’ Yeye husema, ‘Angalia chini.’”

Hili laleta kwenye akili picha ya nyani mchanga aliye juu kwenye miti, akishikamana na mgongo wa mama yake. Wazo la msemo huo ni kwamba kama mama anasema ajishikilie kwa nguvu, mtoto wake huenda akafanya hivyo kwa muda mfupi, lakini kwa kuwa hajui sababu ya agizo lake, huenda akasahau upesi na kulegeza kushika kwake.

Hata hivyo, mtoto huyo akitazama chini, ataona jinsi alivyo mbali sana na chini na atafahamu kwa kina kwamba uhai wake unahusika. Naam, angeweza kuumizwa vibaya au hata afe! Akiwa ameielewa hatari vizuri kabisa, ana msukumo mwingi wa kushikilia kwa mkazo. Sasa onyo au amri yoyote itaheshimiwa sana.

Ni kanuni nzuri jinsi gani kwa kufundisha wengine, hasa watoto. Fundisho la hadithi hiyo ni kwamba badala ya kutoa amri tu, ni jambo la maana kutia uelewevu.

Bila shaka, katika pindi fulani huenda kusiwe na wakati wa kufanya hilo kwanza. Kwa mfano, ikiwa mtoto bila kuangalia kwa uangalifu anaanza kuvuka barabara iliyojaa magari yenye kupita, unaweza kumwamuru asimame na arudi mara moja. Hapa kutoa amri kwanza ni kwa maana. Lakini elezo la hatari ambayo mtoto huyo alikuwa nayo laweza kutia uelewevu.

Faida ya mfikio huu—si kuamuru tu bali pia kutia uelewevu—unapatikana katika mithali ya Biblia: “Yeye ashikaye sheria ni mwana mwenye hekima [uelewevu, NW].”—Mithali 28:7

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

©Shirika la Kizuolojia (uchunguzi wa sayansi ya wanyama) la San Diego

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki