Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 8/8 kur. 3-4
  • Msaada kwa Wanaokufa Katika Kizazi cha Kisasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msaada kwa Wanaokufa Katika Kizazi cha Kisasa
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Kuwafariji Watu Wenye Ugonjwa Usioweza Kupona
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Ni Utunzi Gani Ufaao kwa Walio Wagonjwa Mahututi?
    Amkeni!—1992
  • Msaada Bora Zaidi Unapatikana!
    Amkeni!—1992
  • Hospitali— Wakati Wewe Ni Mgonjwa
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 8/8 kur. 3-4

Msaada kwa Wanaokufa Katika Kizazi cha Kisasa

MWANAMKE huyo, ambaye yeye binafsi ni daktari, alikuwa ametoka tu kupitia ono lenye kutia uchungu sana. Alikuwa amemtazama nyanya yake wa miaka 94 akifa katika sehemu ya utunzaji wa wakati wote ya hospitali baada ya upasuaji wa kansa ambao “hakutaka kamwe.”

“Machozi yangu katika maziko yake hayakuwa kwa sababu ya kifo chake, kwani nyanya yangu alikuwa ameishi maisha marefu, makamilifu,” daktari huyo akaandika. “Nililia kwa sababu ya uchungu aliokuwa amevumilia, na kwa kukosa kutimiza matamanio yake. Nililia kwa sababu ya mama yangu na watoto wake, kwa hisi zao za kupoteza na kufadhaika.”

Hata hivyo, huenda ukafikiria uwezekano wa kusaidia mtu aliye mgonjwa sana kama huyo. Daktari huyo aendelea:

“Sana sana, nililia kwa sababu yangu: kwa hatia kubwa niliyohisi kwa sababu ya kushindwa kumwokoa kutokana na uchungu na aibu, na kwa vile nilivyohisi nimepungukiwa nikiwa tabibu, bila uwezo wa kuponyesha, wala kuondoa kuteseka. Kwa sababu hakuna mahali popote katika mazoezi yangu nilipofunzwa kukubali kifo au kufa. Ugonjwa ulikuwa ndio adui—wa kukabiliwa kila wakati, kwa uwezo wote. Kifo kilimaanisha kushindwa, kutofaulu; kikiwa ugonjwa wenye kudumu kilikuwa kikumbusha cha daima cha ukosefu wa uwezo wa matabibu. Sura ya nyanya yangu mwenye umbo dogo akinitazama kwa macho ya woga akiwa katika kipatia hewa katika sehemu ya utunzaji wa wakati wote hunirudia-rudia hadi leo.”

Mjukuu huyo mwenye upendo alifanya suala tata la kiadili linalohusu tiba na sheria, liwe wazi, ambalo sasa linajadiliwa katika mahakama na hospitali kuzunguka ulimwengu: Ni nini kinachofaa zaidi kwa walio wagonjwa bila tumaini katika kizazi hiki chetu kilichoendelea kitekinolojia?

Wengine wana maoni kwamba chochote kiwezekanacho kitiba apasa kufanyiwa kila mtu aliye mgonjwa. Maoni hayo yanatolewa na Shirika la Matabibu na Wapasuaji Waamerika: “Jukumu la tabibu kuelekea mgonjwa mwenye kuzirai, mwenye akili punguani, au asiyezidi kukua halitegemei tazamio la kupona. Lazima tabibu atende nyakati zote kwa niaba ya afya njema ya mgonjwa.” Hilo lamaanisha kutoa matibabu yote au msaada wa kitiba ambao waweza kutumiwa. Je! wewe wahisi kuwa hilo ndilo linalofaa nyakati zote kwa mtu mgonjwa sana?

Kwa watu wengi njia hiyo yasikika kuwa ndio bora. Na bado, katika miongo michache iliyopita, maono ya utibabu ulioendelea kitekinolojia yametokeza maoni mapya yaliyo tofauti. Katika hati ya maana ya 1984 yenye kichwa “Daraka la Tabibu Kuelekea Wagonjwa Wasio na Tumaini,” halmashauri ya matabibu kumi wataalamu walimalizia: “Kupunguzwa kwa utibabu mwingi sana kwa wagonjwa wasio na tumaini ni kwa hekima ikiwa utibabu huo ungerefusha tu mwendo mgumu na usiostarehesha wa kufa.” Miaka mitano baadaye madaktari hao hao walichapisha makala moja yenye kichwa hicho hicho iliyoitwa “Mtazamo wa Pili.” Wakifikiria tatizo lile lile, wao walitoa taarifa iliyo wazi hata zaidi: “Matabibu wengi na wenye maadili . . . basi, wamemalizia kwamba, ni jambo la kimaadili kutotia [umajimaji] wa chakula na kemikali ndani ya wanaokufa, walio wagonjwa bila tumaini, au wagonjwa waliozirai kabisa.”

Hatuwezi kupuuza maelezo hayo kuwa mawazo tu au mjadala tu ambao hauna maana halisi kwetu. Wakristo wengi wamekabiliwa na maamuzi yenye kusumbua kuhusiana na hayo. Je! mpendwa wetu aliye mgonjwa bila tumaini apaswa kuendelezwa kuwa hai kwa kipatia hewa? Je! kulishwa kwa njia ya mishipa au njia nyingine zisizo za asili zapaswa kutumiwa kwa aliye mgonjwa mahututi? Wakati hali yakosa tumaini, je! fedha zote za mtu wa ukoo, au familia nzima, zapasa kulipia matibabu, labda likihusisha kusafiri hadi hospitali ya mbali ili kupata matibabu ya hali ya juu zaidi?

Bila shaka unafahamu kwamba maswali kama hayo ni magumu kujibu. Hata iwe ungependa kusaidiaje rafiki au mpendwa aliye mgonjwa, ikiwa ungekabiliwa na maswali hayo huenda ukajiuliza: ‘Mkristo ana mwongozo gani? Ni misaada gani inayoweza kupatikana? La maana hata zaidi, Maandiko husema nini kuhusu jambo hilo?’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki