Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 12/8 kur. 14-15
  • Wanawake Je! Wanastahiwa Leo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanawake Je! Wanastahiwa Leo?
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Wanawake Je! Wanastahiwa Nyumbani?
    Amkeni!—1992
  • Cheo cha Wanawake Chenye Maendeleo Katika Nyakati za Kisasa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Wanawake Wana Wakati Ujao Gani?
    Amkeni!—1998
  • Heshima na Staha Chini ya Utunzaji wa Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 12/8 kur. 14-15

Wanawake Je! Wanastahiwa Leo?

KWA nini swali hilo lizuke? wanaume fulani wenye kushangaa huenda wakauliza. Lakini tuchunguzapo kutendwa kwa wanawake katika muda wote wa historia, na siku hizi katika ulimwengu wote, maswali machache yaliyo rahisi yatupa sisi dokezo la jibu hilo.

Katika mahusiano ya kibinadamu, ni nani hasa ambao wamekuwa wenye kuonewa na nani wamekuwa waonezi? Ni nani hasa ambao wamepigwa katika ndoa? Wanaume au wanawake? Ni nani ambao wamelalwa kinguvu nyakati za amani na za vita? Ni nani hasa ambao wamekuwa wenye kutendwa vibaya kingono wakati wa utoto? Wavulana au wasichana? Ni nani ambao wamelazimishwa na sheria za kibinadamu wawe raia wa cheo cha chini? Ni nani ambao wamenyimwa haki ya kupiga kura? Ni nani wamekuwa na fursa ndogo ya kupata elimu? Wanaume au wanawake?

Maswali yaweza kuendelea zaidi, lakini mambo ya hakika yajieleza yenyewe. Katika kitabu chake May You Be the Mother of a Hundred Sons, Elisabeth Bumiller aandika, kutokana na mambo aliyojionea katika India: “Mwanamke Mhindi wa ‘kawaida’ anayewakilisha asilimia 75 ya wanawake na watoto wa kike milioni mia nne katika India, huishi katika kijiji. . . . Yeye hawezi kusoma wala kuandika, ingawa angependa, na inaelekea hajasafiri zaidi ya kilometa thelathini na mbili kutoka mahali alipozaliwa.” Huku kutokuwa na usawa katika elimu ni tatizo si katika India tu bali ulimwenguni pote.

Katika Japani, kama ilivyo katika nchi nyingine nyingi, tofauti hiyo iko. Kulingana na The Asahi Year-book cha 1991, idadi ya wanafunzi wanaume katika mitaala ya miaka minne ya chuo kikuu ni 1,460,000 hali ile ya wanawake ni 600,000. Bila shaka, wanawake ulimwenguni pote wanaweza kutoa ushuhuda juu ya fursa zao chache kuhusu elimu. ‘Elimu ni ya wavulana’ ndio mwelekeo ambao wamelazimika kukabili.

Katika kitabu chake cha hivi karibuni Backlash—The Undeclared War Against American Women, Susan Faludi auliza maswali fulani yafaayo kuhusu hali ya wanawake katika United States. “Ikiwa wanawake Waamerika wana usawa jinsi hiyo, kwa nini wao huwakilisha theluthi mbili za watu wazima wote walio maskini? . . . Kwa nini wangali wanaelekea sana kuishi katika nyumba zisizofaa na hawapokei bima ya afya, na malipo ya uzeeni mara mbili kama wanaume?”

Wanawake ndio wamekuwa wakiteseka zaidi kupita wote. Ni wao ambao wamestahimili ufidhuli, matukano, udhia wa kingono, na kukosewa staha na wanaume. Huko kutendwa vibaya hakumo tu katika zile zinazoitwa eti nchi zinazositawi. Halmashauri ya Sheria ya Bunge la U.S. hivi karibuni ilikusanya ripoti juu ya jeuri dhidi ya wanawake. Ilitoa mambo ya kushtua sana. “Kila dakika 6 mwanamke hulalwa kinguvu; kila sekunde 15, mwanamke hupigwa. . .. Hakuna mwanamke asiyepatwa na uhalifu wenye jeuri katika nchi hii. Kati ya wanawake Waamerika walio hai leo, watatu kati ya wanne wanapatwa na angalau uhalifu mmoja wenye jeuri.” Katika mwaka mmoja, kuanzia wanawake milioni tatu hadi nne walitendwa vibaya na waume zao. Hali hiyo yenye kusikitisha ndiyo iliyoongoza kwenye kupitishwa kwa Sheria Inayopinga Jeuri kwa Wanawake ya 1990.—Ripoti ya Bunge, The Violence Against Women Act of 1990.

Acheni sasa tuchunguze baadhi ya hali ambazo wanawake wamevumilia ukosefu wa staha kutoka kwa wanaume kuzunguka ulimwengu. Halafu, katika makala mbili za mwisho katika mfululizo huu, tutazungumzia jinsi staha ya wote wawili yaweza kuonyeshwa na wanaume na wanawake katika kila hali ya maisha.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki