Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 6/8 uku. 3
  • Je! Kweli Muziki Waweza Kukudhuru?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kweli Muziki Waweza Kukudhuru?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Ninaweza Kuwekaje Muziki Mahali Pao Panapofaa?
    Amkeni!—1993
  • Ninaweza Kuwa na Usawaziko Jinsi Gani Kuhusu Muziki?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Jilinde na Muziki Usiofaa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Kupata Shangwe Yamuziki—Ni Nini Ufunguo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 6/8 uku. 3

Je! Kweli Muziki Waweza Kukudhuru?

EBU wazia hili: Mfanyakazi mwenzako akukaribisha kwa mlo mkuu nyumbani kwake. Unakubali. Jioni inapoendelea, unajifunza mambo kadhaa ya kushangaza juu ya mkaribishaji wako. Yeye ana tabia ya ukatili, aonyesha mielekeo ya kujiua, atumia lugha chafu, na kuendeleza ibada ya Ibilisi. Sasa, je, ungependa kutumia jioni nyingine pamoja naye? “La!” unajibu.

Zaidi ya hiyo, ingekuwaje kama mtu huyo angerekodi usiku huo itikadi zake na mielekeo yake iliyopotoka na kukupa ukanda huo? Je! ungejihatarisha kwa kuusikiliza ukanda huo kwa kurudia-rudia? Haielekei hivyo.

Hata hivyo, uhakika ni kwamba mamilioni ya watu leo hujihatarisha kwa njia hiyo. Na matokeo yamekuwa ni kwamba wengi wanaosikiliza muziki huo huiga mawazo na mwenendo unaoendekezwa na muziki kama huo.

Tunaongea juu ya muziki gani? Mielekeo yenye kupotoka inaweza kupatikana katika karibu kila aina ya muziki. Hata ikiwa mmoja apendelea muziki wa umahiri, jazi, au aina nyingineyo ya muziki, kuna uhitaji wa kutahadhari na kuwa mteuzi.

Hata hivyo, kuna aina nyinginezo za muziki zinazozungumzia habari zisizofaa kabisa kwa njia ya wazi sana. Jambo hilo latokeza magumu ya pekee. U.S. News & World Report lafafanua habari ya msingi ya muziki wenye mdundo mzito kuwa “uasi wa mamlaka wa utineja, kutia ndani ngono nyingi yenye jeuri na mawazo ya mara kwa mara ya kujiua.” Dkt. David Elkind azungumza juu ya beni nyingine za wanamuziki ambazo “zina tabia mbaya sana ya kutumia lugha chafu na kuwa na mwenendo mbaya hivi kwamba zinashushia heshima muziki wote wa roki.” Katika maeneo mengine, vifuniko vya muziki hata huwa na ishara ya kuonya juu ya lugha chafu inayotumiwa humo ndani.

Je! watu wanaitikia tu isivyofaa muziki wasiopenda, au kuna sababu ya kweli ya kuhangaika? Ebu tuchunguze kwa makini baadhi ya muziki wa roki unaofikia watu wengi sasa kupitia rekodi, vidio za muziki katika televisheni, na maonyesho ya muziki jukwaani. Chunguza namna muziki unavyoathiri watu. Kisha ujiamulie kama aina hiyo ya kitumbuizo ni raha isiyodhuru au sumu ya akili. Je! ni kitu ambacho wewe na familia yako mngefurahia au hata kujihatarisha kwacho?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki