Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 6/22 kur. 3-4
  • Kufanya Kazi kwa Bidii—Matokeo ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kufanya Kazi kwa Bidii—Matokeo ni Nini?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Kazi Ngumu Huleta Furaha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kufanya Kazi kwa Bidii—Wakati Kunapofaa
    Amkeni!—1993
  • Kufanya Kazi kwa Bidii—Je! Kunahatarisha Afya Yako?
    Amkeni!—1993
  • Jinsi ya Kufurahia Kazi Ngumu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 6/22 kur. 3-4

Kufanya Kazi kwa Bidii—Matokeo ni Nini?

Na mleta habari za Amkeni! katika Japani

“‘VINYWAJI vinavyoongeza nguvu’ vimekuja kupendwa sana, kukiwa na vinywaji zaidi ya aina 200 vinavyopatikana na vinauzwa kufikia yeni milioni 900 kwa mwaka mmoja,” laripoti Mainichi Daily News, gazeti mashuhuri zaidi la Japani. Kupendwa sana kwa vinywaji hivyo, ambavyo husemwa kuwa vinaongeza nguvu mara hiyo kwa wafanyakazi ambao wamechoka, “kwaonyesha tamaa ya Wajapani ya kufanya kazi wajapokuwa na mkazo wa akili, ukosefu wa usingizi na hali ya hewa yenye joto jingi ya wakati wa kiangazi,” ripoti hiyo yaendelea kusema.

Katika upande ule mwingine wa Pasifiki, “karibu Mwamerika mmoja kati ya kila wanane waliripoti kuwa wao hufanya kazi kwa muda wa saa 60 au zaidi kwa juma,” kulingana na Ofisi ya Takwimu za Kazi za U.S. Wale wenye kazi za juu hulazimika kutoa wakati wao mwingi na nishati kwa kazi hivi kwamba nyakati nyingine kazi zao hutawala maisha zao.

Katika karibu kila tamaduni, watu mmoja mmoja wanaofanya kazi kwa juhudi, kwa kudhamiria, na kwa bidii husifiwa kuwa watu wenye sifa bora. Hata mwandikaji mmoja wa kale wa Biblia alisema hivi: “Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake [ya bidii, New World Translation] Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.” (Mhubiri 2:24) Kwa ujumla, watu kila mahali bado wanaamini sifa hizo. Wawe wanaona kufanya kazi kwa bidii kuwa kunafaa au la, watu wengi zaidi hufanya kazi kutoka asubuhi hadi usiku, siku tano, sita, au hata saba kwa juma.

Hata hivyo, kazi hiyo ya bidii imetimiza nini? Katika nchi kama vile Japani na Ujerumani, “miujiza” ya kiuchumi iliyotokea tangu mwisho wa Vita ya Ulimwengu 2 inatamaniwa sana na nchi zinazoendelea. Mataifa hayo mawili yaliinuka baada ya kushindwa na kuwa mamlaka kuu za kiuchumi ambazo ulimwengu mwingine wote hauwezi kupuuza. Lakini, ujitoaji kwa kazi umekuwa na matokeo gani kwa watu wengi mmoja mmoja?

Ingawa kiwango cha maisha katika Japani kimepanda sana, gazeti Mainichi Daily News laripoti kwamba Wajapani wengi zaidi “bado wanapata ugumu wa kujiona kuwa ni matajiri kihalisi katika maisha zao za kila siku.” Na kwa ubaya zaidi, katika jitihada zao za kutafuta yale yanayoitwa eti maisha ya juu, wengi wanakuwa wagonjwa au hata wanakufa kutokana na kazi ya kupita kiasi na mkazo wa akili. Vivyo hivyo, katika uchunguzi mmoja katika United States, theluthi moja ya mameneja elfu tatu waliochunguzwa walihisi kwamba walikuwa wakifanya kazi nyingi zaidi, wakichoka mno, na hawakuwa na shauku kwa kazi zao.

Wanawake wanaofanya kazi pia wanaonyesha kuwa wanataabika. Uchunguzi mmoja wa Italia ulionyesha kwamba wanawake wanaofanya kazi katika nchi hiyo hufanya kazi kwa wastani wa muda wa saa 30 zaidi ya waume zao kila juma. Kwa kuongezea kutumia muda mrefu wa saa katika ofisi au kiwanda, wanawajibika kushughulikia kazi za nyumbani wanaporudi nyumbani. Mfanyakazi mmoja mwanamke alikiri hivi kwa gazeti Europeo: “Sina wakati wa kujifurahisha kabisa. Sina wakati wa kufanya mambo yangu mwenyewe. Siwezi kuendelea katika hali hii.”

Vipi juu ya maisha ya familia? “Katika kufuatia utajiri wa kimwili, tunajidhabihu wenyewe na familia zetu kwa ajili ya pesa na uwezo,” asema Herbert Freudenberger, mtaalamu wa New York anayeshughulikia uchovu wa kazi. Kwa sababu ya waume zao kufungwa na kazi, wake wengine wa wafanya biashara wa Uingereza wanaofanya kazi nje ya nchi wanaripotiwa kuwa hujihisi kuwa wapweke na kukosa furaha. Lakini si wao tu wanaohisi upweke.

Fikiria matokeo ya maisha ya familia katika Japani, ambapo idadi inayopungua nusu ya wafanyakazi wa ofisi wenye umri wa makamo hurudi nyumbani kabla ya saa mbili za usiku. Wanawake wengine tayari hawawaoni waume zao kuwa wenzi halisi wa ndoa; hawataki kuwaona nyumbani muda mrefu zaidi. Matangazo ya biashara ya televisheni hutaja kwa ufupi kuvunjika moyo kwa wake, yakisema: “Waume wana afya bora zaidi na inafaa zaidi wakiwa mbali na nyumbani.”

Kutokana na hayo, ni wazi kwamba kufanya kazi kwa bidii kuna manufaa na hasara. Kunapofanywa kupita kiasi, kunaweza kuwa mzigo. Kwa hiyo, kufanya kazi kwa bidii kunaweza kufaaje na kuwe chanzo cha furaha badala ya kuwa mzigo?

Kwa upande mwingine, ni jambo zito kadiri gani wakati watu mmoja mmoja wanapoweka kazi mbele ya mambo mengine yote au wanapoendelea na kazi hata matokeo yawe nini? Ebu tuchunguze kwa uangalifu mambo hayo yanayohusu kufanya kazi kwa bidii.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki