Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 7/8 uku. 12
  • Madokezo kwa Wazazi wa Kambo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Madokezo kwa Wazazi wa Kambo
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Matatizo ya Pekee ya Familia za Kambo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Familia za Kambo Zinaweza Kufanikiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Kushughulika na Familia ya Kambo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 7/8 uku. 12

Madokezo kwa Wazazi wa Kambo

SHIRIKA la Idadi ya Watu la U.S. latabiri kwamba familia zenye washiriki wa kambo zitapita familia za kawaida kwa idadi kufikia 1995. Kufikia wakati huo, watoto 59 kwa kila watoto 100 wataishi katika “familia zilichochanganyika” (familia yenye mzazi wa kambo) kabla wafikie umri wa miaka 18. Yanayofuata hapa ni madokezo machache ya kusaidia idadi inayoongezeka ya wazazi wa kambo.

Acha Familia Hiyo Ikue: Wazazi wa kambo ni lazima wakumbuke kwamba inachukua muda kwa watoto wa kambo kukubali mzazi mpya. Mstadi wa matatizo ya akili Mavis Hetherington anaeleza sababu inayofanya miezi michache ya kwanza—au miaka—iwe migumu sana: “Katika wakati wa mapema wa ndoa ya pili, wote wawili wana na mabinti wanakuwa wakali, wenye kununa, wenye kupinga na wenye hasira si tu kwa baba yao wa kambo bali kwa mama yao. Wanamkasirikia . . . mama yao kwa kuolewa tena.” Wazazi wa kambo ni lazima wajaribu kuelewa hisia za watoto, hata kama ni vigumu kufanya hivyo.—Ona Mithali 19:11.

Jenga Uhusiano Mzuri Kwanza: Joy Conolly, katika kitabu chake Stepfamilies, aonya kwa hekima kwamba wazazi wa kambo watakuwa kwa hali bora zaidi ya kurekebisha tabia ya watoto wao wa kambo baada ya kujenga uhusiano mzuri pamoja nao. Kabla ya wakati huo, huenda ikawa bora kwa mzazi halisi ashughulikie nidhamu inayohitajika. (Linganisha Mithali 27:6.) Kwa upande mwingine, wazazi wa kambo wanaweza kupatia watoto hisia ya kuwa na maisha mazuri kwa kutegemeza mambo fulani ambayo watoto hao wamekuwa wakifurahia—kama vile kutembea muda mrefu au kucheza michezo pamoja. Lakini, baba wa kambo wasitumie wakati wa milo kuwa nafasi ya kusomea familia.

Epuka Kuonyesha Upendeleo: Baba wa kambo au mama wa kambo apaswa kuepuka, kama inawezekana, kuonyesha ishara yoyote ya upendeleo kuelekea watoto wake halisi, hata jambo hilo liwe gumu kadiri gani nyakati fulani.—Linganisha Warumi 2:11.

Mkaribiane kwa Kutahadhari: Uchunguzi wa hivi karibuni wa familia za kambo ulipata kwamba mara nyingi ni vigumu hasa kwa baba wa kambo na binti wa kambo kupatana. Mwandikaji mmoja analitaja jambo hilo hivi: “Baba wa kambo hujaribu kuwasiliana, na wasichana hao hawataki. Baba wa kambo hujaribu kutoa nidhamu fulani, na wasichana hao hukataa.” Mwandikaji huyo amalizia hivi kwa ufupi: “Inaonekana hakuna kitu ambacho baba wa kambo anaweza kufanya, wakati wa mapema wa uhusiano wao, na wasichana hao ambao hufanikiwa.” Basi saburi nyingi na hisia-mwenzi zinahitajika. Ingawa wasichana huthamini sifa za mdomo kutoka kwa baba yao wa kambo, mara nyingi hawahisi starehe kwa mambo ya kugusana kama vile makumbatio. Baba wa kambo apaswa atambue kwamba msichana aweza kuhisi hivyo. Kama anahisi hivyo, basi anapaswa kutilia mkazo kutoa sifa za mdomo na mawasiliano badala ya wonyesho halisi wa shauku.—Linganisha Mithali 25:11.

Jihadhari na Wivu: Mambo yaliyoonwa yanaonyesha kwamba mabinti wengi wa kambo huwa na mwelekeo wa kuwaona mama wa kambo kuwa washindani wao. Mama wa kambo anayetazamia msichana ahisi hivyo na ambaye anafikiria hisi hizo anaweza kwa hekima kuepuka mashindano ya kutaka ukuu. Baba anaweza kufanya mambo mengi ya kumhakikishia binti yake upendo wake wenye kuendelea na staha. (Mithali 15:1) Watafiti wanatahadharisha kwamba akina mama wa kambo hujaribu haraka kwa bidii na upesi mno kuwa mama anayekubalika kwa mabinti zao wapya wa kambo. Tena, saburi ndiyo ufunguo.

Kuwa mzazi wa kambo si rahisi. Lakini, kunaweza kufanywa, kama vile maelfu ya mifano inavyoonyesha. Na kumbuka, Biblia hutoa shauri bora zaidi kwa mafanikio katika hali yoyote ya familia inaposema: “Jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.”—Wakolosai 3:14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki