Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Je! Ni Vibaya Kuwa na Ndoto za Mchana?
    Amkeni!—1993
  • Shimo Kubwa Zaidi Ulimwenguni Lililopata Kuchimbwa na Binadamu
    Amkeni!—1993
  • ‘Kutoka Katika Milima Utachimba Shaba’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 1/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Talaka Mara tu baada ya ukumbusho wa pili wa ndoa yetu, mume wangu alilala na rafiki yangu wa karibu. Miaka miwili baadaye, aliniacha. Kwa hiyo nilipoona jalada la Amkeni! la Julai 8, 1993, lenye kichwa “Talaka—Je! Ni Mlango wa Kupata Furaha Zaidi?,” sikusisimka. Nyakati nyingine ni vigumu kwangu kujifunza habari ikaziayo maisha ya familia. Hata hivyo, niliona kuwa yatia moyo kusoma kwamba hatimaye “mume au mke asiye na hatia anaweza kutoka kwenye jaribu hilo akiwa mtu kamili mwenye nguvu na nishati zaidi.” Siwezi kusema kwamba nimefikia hapo, lakini ninafanya maendeleo. Nimekuwa katika mshuko wa moyo mkubwa sana. Lakini habari nyingi ambayo mmeandaa katika makala mengineyo juu ya mshuko wa moyo ilisaidia wazee wa kutaniko langu wanitegemeze kupitia nyakati fulani zilizo mbaya sana. Asante kwa ajili ya msaada wote mnaoandaa kupitia magazeti haya.

D. P., United States

Wazazi wa Kambo Niliposoma makala yenu “Madokezo kwa Wazazi wa Kambo” (Julai 8, 1993), nilisukumwa niwaandikie. Nina umri wa miaka kumi, na mimi huishi na mama yangu. Baba yangu alioa tena, kwa hiyo sasa nina mama wa kambo. Niliposoma jinsi watoto wengine huhisi juu ya wazazi wa kambo, nilifikiri, ‘Hizi ni hisia zangu kabisa!’ Nilifurahi kwamba mojawapo madokezo yenu lilikuwa kuepuka wivu. Mara nyingi, nilimwona mama yangu wa kambo kuwa mshindani. Nyakati nyingine baba yangu hunifanya nihisi kwamba ampenda mama yangu wa kambo zaidi ya vile alivyopata kunipenda wakati wowote. Natumaini baba na mama yangu wa kambo watasoma makala hiyo nzuri na wanielewe mimi zaidi.

V. N., United States

Kuchimba Shaba Mimi husoma magazeti yenu mara kwa mara kwa upendezi. Hata hivyo, nilijiuliza juu ya makala “Shimo Kubwa Zaidi Ulimwenguni Lililopata Kuchimbwa na Binadamu.” (Machi 8, 1993) Mngewezaje kuusifu mgodi huo wa shaba? Je! Biblia haisemi Mungu ataharibu wale wanaoiharibu dunia?

H. Y., Uingereza

Twajua vema juu ya tokeo la kimazingira liletwalo na uchimbaji wa shimo lililo wazi. Hata hivyo, makala yetu iliripoti tu juu ya mgodi huo wa shaba kuwa jambo la upendezi, si ukiwa uchocheaji wa biashara ya migodi. Hata hivyo, bila kupendelea, ni lazima tukubali kwamba biashara ya umeme—kwa kweli, umma kwa ujumla—imekuja kutegemea shaba. Na sehemu kubwa ya shaba itumiwayo katika United States huchimbuliwa katika migodi ya mashimo yaliyo wazi. Basi, haingekuwa haki kulaumu biashara ya shaba pekee kwa ajili ya uharibifu wa mazingira utokeao. Hali hiyo ngumu ni kielezi kingine kinachoonyesha uhitaji wa Ufalme wa Mungu kuchukua usimamizi wa mambo ya dunia.—Mhariri.

Ndoto za Mchana Nina miaka 11, na nataka kuwashukuru kwa ajili ya makala za “Vijana Huuliza . . . ” juu ya ndoto za mchana. (Julai 8 na Julai 22, 1993) Sikuzote niliota juu ya kuwa mtu mwingine, na mmenisaidia nielewe kwamba badala ya kuwa na ndoto za mchana juu ya kupendwa, napaswa nijitahidi kuwa mwenye kupendeka.

J. K., United States

Baada ya kusoma makala hizo, nililia machozi. Wakati wangu mwingi ulitumiwa kwa ndoto za mchana—mara nyingi juu ya kuwa mashuhuri au juu ya wavulana au ngono. Hilo lingetukia hata kwenye mikutano ya Kikristo. Ndoto za mchana zilikuwa zikiongoza maisha yangu. Ningejitenga mbali na familia yetu na marafiki zangu na kuwa peke yangu chumbani mwangu. Nilikuwa mwenye huzuni na mwenye kuona aibu. Sasa nimezingatia moyoni shauri lenu na kulitumia. Nyakati nyingine fikira hizo hurudi, lakini sasa mimi hujaza akili yangu fikira nyingine au kufanya kazi ya upendezi wangu, na fikira hizo hutoweka. Asanteni sana.

T. P., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki