Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Ni Vibaya Kuwa na Ndoto za Mchana?
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mizungu Baada ya kuisoma makala “Maoni ya Biblia . . . Je! Kuna Hatari Katika Kufanya Mizungu?” (Septemba 8, 1993), sasa naelewa kwelikweli kwa nini kufanya mizungu ni kosa. Hivi majuzi umekuwa mtindo kwenye shule yangu kufanya kile ambacho mtu angeweza kukiita kuwaomba roho watabiri wakati ujao. Wenzangu huniambia, ‘Wewe hutaki kujiunga nasi?,’ na ingawa nimekataa, nimekuwa nikijiuliza kwa nini ni kosa. Nilijaribu kutafuta jibu lakini sikuweza kupata la kuniridhisha. Baada tu ya kukata tamaa kutafuta, makala yenu ikatokea. Iliniandalia jibu la kuridhisha. Asanteni kwa kuichapisha.

M. K., Japani

Katuni Nilipendezwa na makala yenu “Je! Katuni Zenye Jeuri za Televisheni Hudhuru?” (Desemba 8, 1993) Niliifurahia kwelikweli kwa sababu watoto wadogo wengi huvutwa na programu hizo zenye jeuri. Nina miaka 13.

D. L., Marekani

Kuunganisha Ulimwengu Niliguswa sana na ule mfululizo “Ni Nini Kitakachounganisha Ulimwengu?” (Desemba 22, 1993) Nilikuwa nikihisi huzuni moyoni juu ya habari zinazoendelea kutoka Bosnia na Herzegovina na kutoka Somalia—wanavyolazimishwa kuishi chini ya hali za vita, njaa, na kifo. Hata hivyo, mfululizo huu ulionyesha dawa ya kweli na jinsi inavyofanya kazi kikweli katikati ya msiba wa ulimwengu huu. Baada ya kuwa mjumbe kwenye mkusanyiko wa kimataifa wa Mashahidi wa Yehova katika Poland huko nyuma katika 1989, naweza kuona kwamba udugu wenye upendo na muungano ambao Mashahidi wa Yehova hufurahia ni kama muujiza wa ki-siku-hizi.

H. K., Japani

Kuchinjwa kwa Sehemu za Uzazi za Wanawake Nataka kuwashukuru nyinyi kwa moyo mweupe kwa kuchapisha ile makala juu ya tohara ya kike (“Mamilioni Wanateseka—Je! Wanaweza Kusaidiwa?”) katika toleo lenu la Aprili 8, 1993. Tangu niliposoma makala hiyo nimehisi huruma nyingi kwa majeruhi hoi wa zoea hilo. Hilo huendelezwa na wazazi waongozwao na mawazo yasiyofaa juu ya hali ya kufanya ngono kwa mwanamke. Lakini si upendo kupasisha watoto zoea hilo la kupita kiasi ambalo mara nyingi lina madhara mazito ya kimwili na ya kimawazo.

J. O. K., Nigeria

Kuutazama Ulimwengu Nilitaka tu kuwaandikia ili kuwaambia mnafanya kazi nzuri sana. Ile sehemu “Kuutazama Ulimwengu” imesaidia sana nihitajipo kuandika ripoti za habari fupi kwa ajili ya shule.

J. W., Marekani

Nina miaka 14, nami husoma Amkeni! kwa kawaida. Mimi hufurahia makala zote. Hata hivyo, sehemu hususa ambayo ningependa kuwashukuru kwayo ni “Kuutazama Ulimwengu.” Mimi hujifunza kutokana nayo mambo mbalimbali yaliyo mengi sana. Sikuzote hiyo hueleza mambo ya sasa, na mara nyingi mimi hupata humo mambo tunayoyazungumza sasa shuleni. Pia mimi huthamini uhakika wa kwamba nyinyi hamtoi kamwe maoni yenu wenyewe juu ya vihabari hivyo. Hiyo hufanya iwe rahisi kuishiriki habari pamoja na watu wengine bila kuingilia ubishi.

T. M., Marekani

Ndoto za Mchana Ninawaandikia kuwashukuru sana kwa zile makala za “Vijana Huuliza . . .” zenye habari za kuarifu juu ya ndoto za mchana. (“Je! Ni Vibaya Kuwa na Ndoto za Mchana?,” Julai 8, 1993, na “Naweza Kuachaje Ndoto Nyingi za Mchana?,” Julai 22, 1993) Baada ya kuisoma makala ya pili, nilitambua kwamba mimi nimekuwa mwotaji mzoelevu wa ndoto za mchana kwa miaka mingi. Utoto wangu ulikuwa wa kutendwa vibaya, na kwa kujiepusha kuwaza mabaya niliyotendwa (kwa ndoto za mchana) niliingia polepole katika gereza la akili nilipokuwa mtu mzima. Ndoto za mchana zimeharibu matokeo yangu kazini na wakati wa kuendesha gari. Hata zimeathiri ndoa yangu vibaya. Kwa msaada wa makala zenu, nimeanza kurudisha nguvu zangu za kukaza fikira juu ya jambo moja na uwezo wangu wa kufikiri, kwa kuwa na nidhamu nyingi, jitihada, na sala.

L. G., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki