Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 8/22 uku. 31
  • Msiba Mwingine Tena wa Kimazingira

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msiba Mwingine Tena wa Kimazingira
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Msiba Baharini na Uharibifu wa Pwani
    Amkeni!—2003
  • Mafuta Hutoka Wapi?
    Amkeni!—2003
  • Walinzi wa Minara ya Taa—Kazi ya Kitaalamu Inayofifia
    Amkeni!—1998
  • Nuru Iokoayo Uhai
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 8/22 uku. 31

Msiba Mwingine Tena wa Kimazingira

IMESEMWA kwamba umeme haupigi mahali palepale mara mbili, lakini sivyo na meli kubwa za kubeba mafuta. Mara mbili katika miaka 20 iliyopita, bandari ya La Coruña katika kaskazini-magharibi mwa Uhispania imechafuliwa na mmwagiko mwingi sana wa mafuta.

Katika asubuhi mapema ya Desemba 3, 1992, meli ya kubeba mafuta ya Ugiriki Aegean Sea ilizama katika miamba inayochomoza kuingia baharini kutoka kwenye rasi ilipo La Coruña. Kwa muda wa saa chache meli hiyo ilivunjika vipande viwili, na saba kati ya tangi zayo tisa zilikuwa zimeshika moto. Moshi mkubwa mweusi uliotanda ulionyesha mahali ambapo rais wa Uhispania Felipe González alipataja kuwa “msiba mkubwa wa kimazingira.”

Meli Aegean Sea ilikuwa imebeba karibu tani 80,000 za mafuta yasiyosafishwa ya Bahari ya Kaskazini, na katika siku iliyofuata aksidenti hiyo, mafuta yenye kuenea kilometa 50 za mraba yalianza kushambulia hori nne zilizokuwa karibu. Miaka kumi na sita iliyopita meli ya kubeba mafuta Urquiola ilizama kwenye lango la bandari iyo hiyo, ikichafua pwani kwa mafuta yasiyosafishwa ya tani zaidi ya 100,000.

Mbali na uharibifu huo mkubwa waliofanyiwa viumbe wa baharini, riziki ya maelfu ya wavuvi, wengine kati yao wakiwa wametokea tu kupata ridhaa kwa ajili ya ule msiba wa kwanza, inatishwa tena. Ni kwa nini kuna aksidenti nyingi hivyo za meli za kubeba mafuta? Ingawa bahari ilikuwa na mawimbi makubwa katika usiku huo wa aksidenti ya juzi, inafikiriwa kwamba kosa la kibinadamu ndilo lilikuwa kisababishi kikubwa cha msiba huo.

Kwa kushangaza, Aegean Sea ilizama meta 90 tu kutoka kwenye mnara wenye taa ya kuonya—mnara wenye taa ya kuonya wa kale zaidi katika ulimwengu ambao ungali unatumiwa—ishara ya La Coruña. Ulijengwa na Waroma miaka karibu elfu mbili iliyopita, waliojua hatari za maji hayo ya pwani. Mnara wenye taa ya kuonya wa sasa, ambao unahifadhi mabaki ya usanii wa Waroma, bado unamweka taa yao ya kuonya. Kwa kusikitisha, katika usiku wa Desemba 3, 1992, onyo hilo halikutiiwa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Foto Blanco

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki