Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 kur. 13-21
  • Je! Umepata Kujiuliza?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Umepata Kujiuliza?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Umepata Kujiuliza? Majibu ya Biblia
  • Nafsi Yako Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Maoni Yako Juu ya Nafsi Huathiri Uhai Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Je, Watu Wabaya Watateketezwa Milele?
    Amkeni!—2009
  • Ni Nini Kinachompata Mtu Anapokufa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 1/8 kur. 13-21

Je! Umepata Kujiuliza?

Je! waamini kwamba mwanadamu ana nafsi isiyoweza kufa inayoendelea kuwako baada ya kifo cha mwili? Mamilioni, labda mabilioni, huamini kwamba mwanadamu amepewa nafsi ihamiayo ulimwengu mwingine au katika hali ya kuwako baada ya kifo au hubadilika kuwa kiumbe kingine. Biblia husema nini juu ya nafsi? Utapata maswali yafuatayo kuwa yenye kuvutia na yenye kuelimisha. Ili kupata majibu, twadokeza uchunguze maandiko yaliyotajwa au utazame ukurasa 21.

1. Je! Adamu aliumbwa mbinguni, au duniani?—Mwanzo 1:26-28.

2. Je! Adamu aliumbwa akiwa na hali ya kuweza kufa, au ya kutoweza kufa?—Mwanzo 2:15-17.

3. Kama Adamu angetii na hangetenda dhambi, je, yeye angelikufa?—Warumi 6:23.

4. Je! mwendo aliochukua Adamu ulithibitisha kwamba angeweza kufa au hangeweza kufa?—Mwanzo 3:19; 5:5.

5. Kwa kufanya dhambi, je, Adamu alipoteza makao ya kidunia, au ya kimbingu?—Mwanzo 1:26-28.

6. Ikiwa Yesu alikuja kurudisha kile kilichopotezwa na kuanguka kwa Adamu, ni nini kitakachorudishwa?—Zaburi 37:29; Warumi 5:18, 19; Ufunuo 21:1-4.

7. Je! Adamu alifanyizwa kwa sehemu mbili tofauti, nafsi na mwili?—Mwanzo 2:7; 1 Wakorintho 15:45.

8. Ikiwa unaamini kwamba Adamu alikuwa nafsi na mwili, ni sehemu gani iliyofanya dhambi, ni nafsi au ni mwili?—Zaburi 51:1-4.

9. Ukijibu, “Ni nafsi,” kwa nini ni lazima mwili uteseke?

10. Ukijibu, “Ni mwili,” kwa nini ni lazima nafsi iokolewe?

11. Ikiwa mtu huenda mbinguni kwa kufa, je, hilo halithibitishi kwamba dhambi na kifo ni baraka badala ya kuwa laana kama vile Biblia isemavyo?—Warumi 5:12; 6:21-23.

12. Ni adhabu gani aliyopewa Adamu kwa sababu ya dhambi yake—kifo, au kuendelea kuwapo mahali pengine?—Mwanzo 2:16, 17; 3:19.

13. Je! kulikuwa na adhabu moja kwa ajili ya mwili na nyingine kwa ajili ya nafsi?—Mhubiri 9:5, 10; Ezekieli 18:4.

14. Je! Mungu hata alifikiria mateso ya milele katika moto wa helo?—Yeremia 7:31.

15. Kulingana na Paulo, mshahara wa dhambi ni nini?—Warumi 6:23.

16. Je! Paulo ataja mateso ya milele katika moto wa helo?—Warumi 6:7.

17. Ikiwa moto wa helo upo kikweli, kwa nini mtu angeteseka kwa umilele wote ili kulipa kwa ajili ya muda mfupi wa maisha ya kutenda dhambi? Je! haki ya Mungu imepungukiwa zaidi ya ile ya mwanadamu?—Warumi 9:14.

18. Je! wanaume wa kale waaminifu waliamini kwamba walikuwa na nafsi iliyoenda ama mbinguni ama kwenye moto wa helo?—Mwanzo 37:35; Zaburi 89:48; Matendo 2:34.

19. Tumaini la kweli kwa ajili ya wafu ni jipi?—Yohana 5:28, 29; 11:23-26; Matendo 24:15.

20. Ikiwa hakuna nafsi isiyoweza kufa, watu fulani (144,000) wanakujaje kutawala pamoja na Kristo mbinguni?—1 Wakorintho 15:42-49, 53, 54; Ufunuo 14:1, 4; 20:4.a

[Maelezo ya Chini]

a Maneno “nafsi isiyoweza kufa” hayaonekani mahali popote katika Biblia. Neno “kutokufa” (Kigiriki, a·tha·na·siʹa) laonekana mara tatu tu katika Biblia na si kwa uhusiano na nafsi kamwe. (1 Wakorintho 15:53, 54; 1 Timotheo 6:16) Ili kupata maelezo mengi zaidi juu ya lile litukialo baada ya kufa na tumaini la kweli kwa ajili ya wafu, ona kichapo Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko, kurasa 205-12 (Motoni), 232-36 (Nafsi), 261-65 (Roho), na 334-41 (Ufufuo), kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

Je! Umepata Kujiuliza? Majibu ya Biblia

Yafuatayo ni baadhi ya maandiko yaliyotajwa pamoja na maswali kwenye ukurasa 13:

1. “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, . . . mwanamume na mwanamke aliwaumba. . . . Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha.”—Mwanzo 1:27, 28.

2. “Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”—Mwanzo 2:16, 17.

3. “Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”—Warumi 6:23.

4. “Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”—Mwanzo 3:19.

5. Ona Na. 1.

6. “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, . . . Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”—Ufunuo 21:3, 4.

7. “BWANA [Yehova, NW] Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” (Mwanzo 2:7) Neno “nafsi” latafsiri lile la Kiebrania neʹphesh, “kile kipumuacho.” “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai.” Angalia, “akawa,” si “alipewa.”—1 Wakorintho 15:45.

8. “Dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, na kufanya maovu mbele za macho yako.”—Zaburi 51:3, 4.

9, 10. Maandiko hayahitajiwi.

11. “Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.”—Warumi 5:12.

12. Ona Na. 4.

13. “Walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, . . . hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.” (Mhubiri 9:5, 10) “Kama nafsi ya baba, ndivyo ilivyo nafsi ya mwana mali yangu vilevile; nafsi inayofanya zambi, itakufa.—Ezekieli 18:4, Zaire Swahili Bible.

14. “Wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, . . . ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.”—Yeremia 7:31.

15. Ona Na. 3.

16. “Yeye aliyekufa amesamehewa haki mbali na dhambi.”—Warumi 6:7.

17. “Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!”—Warumi 9:14.

18. “Maana Daudi hakupanda mbinguni.”—Matendo 2:34.

19. “Nina tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.”—Matendo 24:15.

20. “Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.” Ikiwa kutokufa ‘huvaliwa,’ basi hakurithiwi. (1 Wakorintho 15:53) “Nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, . . . Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.”—Ufunuo 14:1, 4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki