Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 1/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Jamii Kuungana Ule mfululizo “Je! Jamii Zote Zitapata Kuungana Wakati Wowote?” (Agosti 22, 1993) ulinisaidia kuona jinsi ubaguzi wa jamii ulivyoanza na jinsi ubaguzi huo umepitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ulinisaidia pia kuelewa sababu inayofanya Wakristo wote si lazima wawe wameshinda ubaguzi wao wote. Zamani jambo hilo lilikuwa likinivunja moyo sana. Lakini sasa najua kwamba huchukua muda kwa mtu kuondolea mbali mielekeo hiyo mibaya. Natazamia ulimwengu mpya wa Mungu, ambapo hapatakuwa tena na suala la jamii.

C. W., United States

Kutengeneza Kadi Asanteni kwa makala “Tupeleke Kadi.” (Agosti 8, 1993) Nyanya yangu amekuwa akitengeneza kadi kwa miaka mingi na kututumia sisi sote wajukuu. Nina umri wa miaka 13 na mimi mwenyewe nimekuwa nikitengeneza kadi kwa muda upatao miaka miwili. Kutumia maua yaliyofinywa, kama vile makala yenu ilivyodokeza hufanya vizuri. Nilijifunza kwamba mtu akiweka gundi juu ya maua na kisha unyunyize vimeremeti juu, matokeo huwa mazuri sana.

J. B., United States

Ulemavu Makala chache sana kuhusu ulemavu zimekuwa zenye uhalisi kama makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kukabilianaje na Ulemavu Wangu?” (Juni 8, 1993) Baada ya kutumikia kwa miaka kadhaa nikiwa mhudumu katika ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Roma, Italia, nilihusika katika aksidenti mbaya ya gari iliyoharibu uti wangu wa mgongo. Mambo rahisi kama kutembea na kushika glasi kwa ghafula yakawa magumu sana. Mara hiyo nilihitaji mtu wa kunisaidia kutoka kitandani, kunivisha, kunisaidia kupanda orofa, na kadhalika. Baada ya muda mrefu wa hasira, huzuni, kujihurumia, na machozi ya kindani, hatimaye nilikubali hali na kung’amua kwamba ilikuwa ni lazima nifanye yote niwezayo katika hali hiyo. Kwa utegemezo wa tabibu wa mazoezi ya mwili, wazazi, marafiki, hali yangu ikafanya maendeleo, na nimeendelea kutumikia katika ofisi ya tawi. Amini usiamini, mtu ajapokuwa mlemavu, bado aweza kuwa mtendaji na kutumikia sana!

A. E., Italia

Kukusanya Mawe Nikiwa daktari, nilisoma kwa upendezi mkuu makala yenu “Kutafuta Hazina ya Aina Tofauti.” (Julai 8, 1993) Hata hivyo, niliona kwamba mliposema kuhusu matumizi ya nyundo, hamkutaja chochote kuhusu kuvaa miwani ya kukinga macho. Hilo ni muhimu sana kwa sababu vipande vidogo vya mawe vyaweza kurushwa kwa urahisi na nyundo, na mawe hayo yaweza kuwa hatari sana kwa macho ya mtu.

G. T. W., Uingereza

Twathamini dokezo hilo lenye mafaa la usalama.—Mhariri.

Hisi ya Kunusa Nilifurahia sana makala “Hisi Yetu ya Kunusa Inayobadilika-Badilika.” (Julai 22, 1993) Miaka mitatu iliyopita nilifanya mradi wa sayansi ya asili juu ya habari hiyo. Watu wengi hawatambui jinsi mfumo wa hisi ya kunusa ulivyo muhimu. Asanteni sana kwa kuonyesha watu wengi jinsi hisi ya kunusa inavyochochea hofu.

L. T., United States

Hadithi za Wanyama Mimi ni Mzulu mwenye umri wa miaka 20 apendaye maajabu ya uumbaji. Nilithamini sana makala yenu “Mrukaji-Ghafula Mwenye Ukimya.” (Machi 8, 1993) Miongoni mwa Wazulu, bundi huonwa kuwa ndege mwenye kuashiria mabaya na huhusianishwa na uchawi. Watu wanapoona bundi, wao humfukuzia mbali. Kwa hiyo nilithamini sana makala yenu rahisi na yenye kuarifu.

Z. P. M., Afrika Kusini

Asanteni kwa makala “Wanamuziki Wanaoruka wa Ulimwengu wa Wadudu.” (Aprili 8, 1993) Mara nyingi panzi huhusianishwa na tauni. Lakini makala hiyo ilinifanya nionee mdudu huyo huruma—na pia ikaongeza hofu yangu yenye kicho kwa Muumba wetu mwenye hekima na mwenye uangalifu hata kwa mambo madogo-madogo sana.

V. P., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki