Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 3/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 3/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Upweke Asanteni kwa ule mfululizo “Upweke—Unaloweza Kufanya Nao.” (Septemba 22, 1993) Mimi nililia machozi kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho. Ilinifanya nichunguze sana hisia ambazo nimekuwa nikiwa nazo hivi majuzi. Sasa nang’amua kwamba si mimi tu huhisi nikiwa mpweke. Natumaini sana kwamba nitaweza kufuata ushauri wenu na kuutumia maishani mwangu.

S. G., United States

Mimi niliguswa sana na makala hizo. Nimetibiwa nikiwa na mshuko-moyo wa kadiri kubwa nami huuona upweke kuwa adui yangu mkubwa zaidi. Mtu aliyeshuka moyo hung’ang’ana siku baada ya siku kupambana na kitu hiki chenye kummaliza mtu polepole. Makala kama hizo ni kama nuru katika giza la kukosa tumaini.

G. P., United States

Mimi nina miaka 21 nami natumikia nikiwa mtumishi wa huduma katika kutaniko la Mashahidi wa Yehova. Pia nimetumikia nikiwa painia (mweneza-evanjeli wa wakati wote). Lakini mara nyingi nimepambana vikali na upweke. Makala zenu zilikuwa jibu kwa sala zangu. Wazee wa kutaniko letu wamekuwa wakionyesha upendo sana na kutoa msaada, lakini sasa naona jinsi mimi niwezavyo kujiboresha. Nimefanya mabadiliko mengi katika mtazamo na matendo.

R. P., United States

Hivi majuzi nimekumbwa sana na upweke. Hata nashindwa kuwaeleza jinsi nimehisi nikisumbuka. Lakini hebu wazieni nilivyoshangaa kupokea Amkeni! la Septemba 22, 1993. Nilibaki mdomo-wazi! Nilimshukuru Yehova nikalisoma mara tu nilipoweza. Asanteni kwa mfululizo huo ulioandikwa vema wenye ushauri ufaao.

C. F., Uingereza

Hadithi za Mapenzi Zilizopotoshwa Mimi niligutuka nilipoona kile kihabari cha “Kuutazama Ulimwengu” cha “Hadithi ya Mapenzi ya Aina Tofauti.” (Oktoba 22, 1993) Kabla sijaanza kujifunza Biblia, nilikuwa nikiandika hadithi hizo zilizopotoshwa juu ya mapenzi ya watu wa jinsia moja. Niliposoma makala hiyo, ilinigonga ikanionyesha kwamba bado mimi nilikuwa nikifikiria hadithi hizo, nyakati nyingine nikisitawisha zilizo mpya katika uwazio wangu. Kwa sababu nyinyi mlishughulikia habari hiyo, mwishowe nimeweza kukomesha mawazo ya namna hiyo.

S. S., Japani

Mateso ya Kidini Hakuna hadithi nyingine yoyote kuhusu maisha ya kibinafsi imepata kunigusa kuliko ile yenye kichwa “Ee, Yehova, Msaidie Msichana Wangu Mchanga Aendelee Kuwa Mwaminifu!” (Septemba 22, 1993) Ilikazia akili na moyo wangu kwamba hata iwe ni jambo gani nitakalolazimika kupatwa nalo ili kushika ukamilifu wangu kwa Yehova, sikuzote yeye atanitegemeza.

C. D., United States

Ilikuwa haiwezekani kukosa kuguswa na hadithi hiyo kuhusu maisha ya kibinafsi. Binti yetu Esta aliiona makala hiyo kuwa nzuri ajabu! Yehova na asaidie watoto wetu kuwa na imani yenye nguvu jinsi hiyohiyo!

A. C., Ufaransa

Asanteni kwa ile makala “Washindi Wajapokabiliwa na Kifo.” (Mei 8, 1993) Sisi twafurahia uhuru wa kidini hapa. Lakini mimi nasali ili niweze kufuata kielelezo cha ndugu hao na kudumisha ukamilifu wangu nipatwapo na magumu ya aina nyinginezo.

S. M., Brazili

Athamini Uchoraji Nilipoiona picha ya ulimwengu mpya wa Mungu katika jalada la Amkeni! la Oktoba 22, 1993, nilifurikwa na shangwe. Niliendelea kukodolea macho picha hiyo, nikisali niweze kuishi huko. Niliitazama tena siku kadhaa baadaye, na bado ikawa na matokeo yaleyale. Asanteni wa kitia-moyo kizuri hivyo.

S. H., United States

Mimi sijui wachoraji wenu ni nani, lakini kazi yao huvutia kwelikweli! Kati ya michoro iliyo mizuri zaidi ambayo nimepata kuona ni ile iliyo katika vitabu na vichapo vyenu. Mimi mwenyewe ni mchoraji, nami naweza kuelewa uchoraji ukiwa bora kikweli.

D. W., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki