Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Upweke Nataka kuwashukuru sana, sana, kwa ajili ya ule mfululizo “Upweke—Unaloweza Kufanya Nao.” (Septemba 22, 1993) Ulikuja katika siku niliyokuwa nikihisi mpweke sana. Hata ingawa ulinifanya nilie, nahisi vema zaidi baada ya kuusoma. Naweza kufikiri juu ya marafiki wangu kadhaa wanaoweza kupata kitia-moyo kwa kuusoma.
B. H., United States
Hata ingawa nilikuwa nimetamani kupata makala kama hiyo kwa muda fulani, ilikuja bila kutazamiwa kabisa. Ningependa kutoa shukrani zangu za moyoni kwa ajili ya ushauri uliokuwamo. Kwa kweli upweke ni mgumu kuuelewa ikiwa hujaupata.
Nina miaka 38 na nimepatwa na upweke mwingi sana, baada ya kuwa mtoto wa pekee na baadaye kubadili-badili kazi-maisha yangu na kupata talaka. Habari hiyo ilikuwa yenye kutia nuru na kuelimisha. Hata hivyo, hamkutaja kwamba upweke waweza kuongoza kwenye ukosefu wa adili katika ngono, utumizi mbaya wa madawa ya kulevya, na mashirika mabaya.
J. B., United States
Katika makala hii hususa, tulichagua kukazia juu ya njia za kushinda upweke badala ya kukazia hatari zao. Hata hivyo, twathamini maoni hayo.—Mhariri.
Nondo na Vipepeo Nikiwa mtu mwenye kupendezwa na biolojia, ningependa kuongeza jambo moja katika makala “Nondo au Kipepeo—Waweza Kuwatofautishaje?” (Mei 8, 1993) Njia dhahiri zaidi ya kubainisha mara moja kati ya nondo na kipepeo ni kutazama vikao vyao. Nondo huketi mabawa yake yakiwa yamefunguliwa tambarare; naye kipepeo, mabawa yake yakiwa yamefungwa pamoja yakisimama wima.
Y. Y., United States
Asante kwa habari hiyo ya ziada.[1] “The World Book Encyclopedia” lasema kwamba hilo ni kweli kwa habari ya ‘vipepeo na nondo walio wengi.’—Mhariri.
Vijana Huuliza . . . Asanteni kwa makala “Je! Ninakua kwa Njia ya Kawaida?” (Septemba 22, 1993) Dada yangu ni mchanga zaidi yangu, naye ni mrefu sana. Sasa najua kwamba hiyo haimaanishi nitakuwa mfupi daima.
C. L., United States
Asanteni kwa makala “Vipi Juu ya Kuzurura-zurura?” (Juni 22, 1993) Sijapata kuwa aina ya tineja ambaye huzurura-zurura na vijana wengine. Hiyo ilinifanya nihisi kwamba nilikuwa na kasoro fulani. Lakini makala hiyo ilinisaidia kujua kwamba kuzurura-zurura kwaweza kukuletea matata makubwa. Kupika, kuchora, kuandika barua, na kuhubiri ni njia bora zaidi za kutumia wakati wangu.
K. R., United States
Nina miaka 11 pekee, lakini nilifurahia sana ile makala “Naweza Kuepukaje Kupata UKIMWI?” (Septemba 8, 1993) Mama yangu nami tulizungumza juu yayo pamoja. Asanteni kwa kueleza kindani jinsi ya kuwa salama kutokana na virusi ya UKIMWI. Nilifikiri ungeweza kuipata kwa njia nyingi mbalimbali!
L. K., United States
Jumba la Hifadhi ya Uangamizo Hivi karibuni msimamizi wangu wa kazi alipanga kuzuru Jumba la Ukumbusho wa Uangamizo. Nilimpa makala ya Mei 8, 1993, “Jumba la Hifadhi ya Uangamizo na Mashahidi wa Yehova” ili kuboresha ziara yake. Jumba hilo hupeana maono 500 ya watu binafsi yaliyoko kwenye kadi. Kadi yake ilikuwa na ono la mmoja wa Mashahidi wa Yehova—Emma Arnold. Familia yangu ilikutana na ile ya Arnold katika 1951 na tulikuwa na picha zao katika kitabu chetu cha picha. Msimamizi wangu alishangaa kwamba alipata ono si la Mashahidi tu bali pia la Shahidi ambaye familia yetu ilijua! Nilishiriki naye na wengine kazini picha zetu na ono la mwana-mkwe wa Dada Arnold, Max Liebster, lililotokea katika Mnara wa Mlinzi la Mei 1, 1979.
J. K., United States