Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 6/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Stesheni ya Redio Yabadilisha Muziki Wayo
  • Safari za Chungu
  • Kisukuku Kingine Bandia
  • Kasisi-Jeshi wa Kwanza Aliye Mwislamu
  • Farasi wa Mwituni Wapungua
  • Taabu za Ndoa za Uingereza
  • Kitabu cha Ujiuaji
  • “Tamaa Kubwa Sana ya Televisheni”
  • Aina Nyingine ya Hatari ya Magari
  • Lafudhi za Ndege
  • Kuelimisha Baba
  • Fanya Kusoma Kupendeze
  • Je! Televisheni Imekubadili Wewe?
    Amkeni!—1991
  • Kudhibiti Utazamaji wa TV
    Amkeni!—2006
  • Dhibiti Televisheni Kabla Haijakudhibiti Wewe
    Amkeni!—1991
  • TV—Je, Ni Mwizi wa Wakati?
    Amkeni!—2006
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 6/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Stesheni ya Redio Yabadilisha Muziki Wayo

Kwa uamuzi mkali usio wa kawaida, stesheni ya redio ya California ambayo hutangaza muziki mwingi wa rapu hivi karibuni ilitangaza kwamba haitaweka tena muziki ambao stesheni yauona kuwa “haujali jamii.” Huo ungetia ndani muziki wowote “unaotukuza matumizi ya dawa za kulevya, ngono ya waziwazi, wenye kutia moyo jeuri au kudharau wanawake.” The New York Times hivi karibuni liliripoti kwamba stesheni hiyo tayari imepiga marufuku nyimbo tisa, baadhi yazo zikiwa na vichwa visivyostahili kuandikwa. Mwelekezi wa programu ya stesheni asema kwa uthabiti kwamba badiliko hilo lilichochewa na tamaa ya kutumikia jamii vema. Stesheni zenye kushindana zasema kwamba sera hiyo mpya ilichochewa na tamaa ya kupata umashuhuri.

Safari za Chungu

Chungu husafiri vipi? Wengi huacha alama ya kemikali ili kwamba waweze kupata hatua zao na kuona njia yao ya kwenda nyumbani. Lakini Dakt. Rudiger Wehner, mstadi wa wanyama katika Chuo Kikuu cha Zurich, Uswisi, alishangaa jinsi chungu katika Sahara husafiri. Isitoshe, jua la jangwani lingekausha alama ya kemikali kwa dakika chache. Katika hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Texas, Dakt. Wehner alisimulia jinsi chungu wa jangwani hutumia mfumo wa kusafiria ulio mwerevu unaofanana na chombo kimoja kilichotumiwa wakati wa safari ya ndege ya Vita ya Ulimwengu ya 2. Chungu hutazama angani na kuona violezo vya mwanga ulio jinsishajincha usioweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu. Wanazunguka kwa mtindo ili kujirudisha nyuma na kuelekea moja kwa moja nyumbani. The Dallas Morning News lilichekesha hivi: “Ukipotea katika kaskazi ya jangwa la Sahara katikati ya siku, afadhali uulize chungu njia.”

Kisukuku Kingine Bandia

Nzi aliyezuiwa katika kipande kinene cha gundi, au masalia ya utomvu wa mti, alionwa na wanasayansi kuwa kiolezo kilichohifadhiwa vilivyo kutoka miaka milioni 38 iliyopita. Hata hivyo, gazeti New Scientist liliripoti kwamba kiolezo hicho kilichotunukiwa kwa kweli kimekuwa “sawa na ile shere ya Piltdown (mtu anayesemekana kuwa na mchanganyiko wa fuvu la mwanadamu na mnyama aliyepatikana kuwa shere).” Yaonekana kwamba angalau miaka 140 iliyopita, mtu fulani aliye mstadi wa kucheza shere kwa kweli alichonga kipande cha gundi, akafanya shimo katika mojapo nusu yacho, naye akamweka nzi wa chooni ndani yacho. “Kisukuku” hicho kiliuziwa Jumba la Hifadhi ya Historia ya Asili la Uingereza mnamo 1922 nacho kimekuwa kikichunguzwa na wanasayansi wenye kuongoza, hata kikatajwa kwenye kitabu cha visukuku karibuni katika 1992.

Kasisi-Jeshi wa Kwanza Aliye Mwislamu

Jeshi la Marekani linaandika makasisi wapatao 3,152 wanaowakilisha dini tofauti 243—zote hizo, kufikia hivi karibuni, ya aina ya “Uyahudi na Ukristo.” Sasa, kulingana na The Washington Post, jeshi limemweka kasisi-jeshi wa kwanza aliye Mwislamu. Akiwa na alama ya tepe ya mwezi-mwandamo kwenye vazi lake rasmi, kasisi huyo ni Imam, kiongozi wa kidini Mwislamu. Idara ya Ulinzi ya Marekani yasema kwamba kuna Waislamu 2,500 katika Jeshi la Marekani, ijapokuwa kikundi cha Kiislamu jeshini chadai kuwa idadi kamili yakaribia 10,000. Wanajeshi fulani Waamerika waliripotiwa kuwa waligeuzwa wawe Waislamu walipokuwa katika Saudi Arabia wakati wa vita ya Ghuba la Uajemi. Sasa, wanajeshi Wabuddha wanatafuta mmoja awe kasisi wao jeshini.

Farasi wa Mwituni Wapungua

Farasi wa mwituni waitwao lavradeiros wako huru katika eneo la Lavrado la kaskazini mwa Brazili. Kulingana na jarida Ciência Hoje la São Paulo, hao ni farasi wa mwituni wa mwisho ambao hawana ulinzi rasmi wa serikali. Kwa sababu ya uwindaji, uzalishaji wa aina tofauti, na biashara, wanapungua sana kwa idadi. Watu katika eneo la Lavrado wanakadiria kwamba farasi walikuwa 3,000 miaka michache tu iliyopita; leo kuna 200 tu. Lavradeiros kwa kawaida huzaa sana, wakinzao magonjwa, na wenye mbio sana—wanaweza kukimbia karibu kilometa 55 kwa nusu saa!

Taabu za Ndoa za Uingereza

Ndoa ina matatizo kila mahali Ulaya lakini labda si mahali pengine popote kuliko Uingereza, uchunguzi wa karibuni umeona hivyo. Eurostat, ofisi ya tarakimu ya EU (Umoja wa Ulaya), ilijaribu kupima mitindo ya maisha inayotofautiana ya wanawake milioni 177 wanaoishi katika mataifa yenye ushirika na EU. Kwa wastani, asilimia 6.5 ya wanawake walikuwa wakilea watoto bila wenzi wao, lakini katika Uingereza wastani ulikuwa wa juu—asilimia 10.1. Wastani ufuatao wa juu ulikuja kutoka Ujerumani, kukiwa na asilimia 7.7. Wanawake Waingereza waliolewa wakiwa na umri mchanga zaidi kwa wastani kuliko walivyoolewa wanawake wengine wa EU—kabla hawajafikia umri wa miaka 24. Pia kiwango cha talaka cha Uingereza kilikuwa cha juu zaidi.

Kitabu cha Ujiuaji

The Complete Manual of Suicide kimekuwa kitabu chenye kuuzwa sana katika Japani hivi karibuni; yaonekana kimesababisha vifo kadhaa. Kitabu hicho kinaelezea msitu wa Aokigahara wa hektare 2,500 chini ya Mlima Fuji kuwa “mahali pafaapo” pa kujiua. Katika kipindi cha miezi mitatu ya kuandikwa kichapo hicho, miili miwili ilipatikana imekufa katika Aokigahara; yote miwili ilikuwa na kitabu hicho Manual. Mwingine ambaye alitaka kujiua alipatikana akizurura kwenye msitu huo na kitabu hicho. Kufikia mwisho wa Oktoba 1993, ujiuaji ulikuwa umeongezeka katika Aokigahara tayari kwa asilimia 50 kwa mwaka wote uliopita. Hata hivyo, mtungaji wa kitabu hiki alikana kuhusika kokote kwa moja kwa moja kati ya ujiuaji wote huo na kitabu chake. Yeye alisema: “Najaribu kufanya maisha yawe rahisi kwa kutia ndani ujiuaji kuwa mojapo machaguzi ya maisha ya mtu, kwa kitabu hiki.”

“Tamaa Kubwa Sana ya Televisheni”

Kulingana na uchunguzi wa hivi karibuni, idadi yenye kuongezeka ya Waitaliano wanaathiriwa na “tamaa kubwa sana ya televisheni,” tamaa ipitayo kiasi ya kutumia wakati mwingi zaidi katika vipindi vya televisheni. Wakati wa juma la kiolezo, asilimia 82 ya Waitaliano walitazama televisheni, “na wale waliofanya hivyo walikuwa mbele ya kiwambo, kwa wastani, kwa muda wa saa zisizopungua tano” kwa siku, lahakikisha La Repubblica. Kati ya wenye umri wa miaka minne hadi saba, kutumia wakati katika televisheni kuliongezeka kwa asilimia 15 zaidi ya mwaka uliopita. Lakini “wahusika walioathiriwa sana na tamaa kubwa sana ya televisheni ni matineja na wale ambao hawakuendelea zaidi na shule ya msingi.” Je! watu hutazama televisheni kwa sababu televisheni inaendelea kuboreka? Francesco Siliato, mkurugenzi wa chuo hicho aliyechunguza utafiti huo asema kwa uthabiti: “Tarakimu hazionekani zikihusika hata kidogo na kiwango cha programu zinazotangazwa.”

Aina Nyingine ya Hatari ya Magari

Wazazi wenye daraka hufuata hatua zinazofaa wanapoendesha gari wakiwa na watoto wao, wakiwafunga kwa usalama hata wakienda kwa muda mfupi dukani. Lakini wachache waweza kugundua hatari ambazo watoto wanakabili mara tu wanapoingia dukani. Gazeti Parents liligundua hivi karibuni kwamba katika 1991 watoto wapatao 19,000 walio chini ya umri wa miaka mitano walihitaji kukimbizwa kwenye vyumba vya dharura Marekani baada ya kuanguka kutoka kwenye vigari vya kufanyia ununuzi. Kwa sababu hiyo, viwanda viwili vya nchi vyenye kutengeneza vigari vya dukani hivi karibuni vilikubali kuweka mishipi ya usalama kwa ajili ya watoto katika vigari vyote wanavyouza katika New York na Texas. Ishara kwenye vigari hivyo zitaonya wazazi pia wasiache watoto wao bila usimamizi.

Lafudhi za Ndege

Je! ndege mmoja aweza kujua kwamba mwingine anatoka kwenye eneo tofauti kwa kusikiliza tu jinsi anavyoimba? Gazeti National Geographic laripoti kwamba kulingana na Lance Workman, mstadi wa maisha ya wanyama kwenye Chuo Kikuu cha Glamorgan katika Wales, jibu miongoni mwa robini ni ndivyo ilivyo. Workman alipata kwamba aliporekodi kwenye utepe na kugeuzwa kwenye vielelezo vya kuonyeshwa kwa njia ya sauti ya nyimbo za robini, angeweza kuziweka kwa urahisi kulingana na eneo la Uingereza ambamo ndege ilitokea. Kwa kweli, wakati robini wa kiume kutoka Sussex alisikia sauti iliyorekodiwa ya yule mwingine wa kiume kutoka Wales, alivimbisha mabawa yake kwa hasira na akashambulia utepe huo!

Kuelimisha Baba

Wizara ya Elimu ya Japani imeanza mradi wa kuelimisha kina baba Wajapani, ambao hutumia kwa wastani dakika 36 tu kwa siku pamoja na watoto wao. Wizara hiyo inatoa udhamini wa “mfululizo wa semina za ‘elimu ya mambo ya nyumbani,’ wakiwa na lengo la kuwafanya kina baba wasaidie nyumbani na kutumia wakati zaidi na watoto wao,” laripoti Mainichi Daily News. Masomo hayo, yakiwa na sehemu tano za muda wa saa moja na nusu hadi mbili, yatafanyiwa katika au karibu na mahali pa kazi kwa wakati ufaao ili kufanya iwe rahisi kwa kina baba kuhudhuria. Ingawaje, miongoni mwa walio wa kwanza kunufaika na masomo hayo ni kina baba wanaofanya kazi katika Wizara ya Elimu, ambao wana tabia ya kutumia saa nyingi kufanya kazi ya ziada.

Fanya Kusoma Kupendeze

Tarakimu zaonyesha kwamba watu wazima Wakanada milioni 2.9 hawajui kusoma “vizuri kiasi cha kuweza kuelewa habari inayopatikana katika maisha ya kila siku,” The Toronto Star likaripoti hivi karibuni. Katika jitihada ya kushindana na ukosefu wa elimu, Juma la Kitabu cha Watoto Wakanada limeundwa kuchochea “shangwe na kupenda kusoma.” Kufundisha watoto kupenda kusoma katika kizazi cha leo cha muziki, televisheni na video si rahisi hata hivyo. Ufunguo ni kuanza watoto wakiwa wachanga na kupunguza vikengeusha-fikira. Gazeti hili lamnukuu msichana wa miaka kumi, ambaye familia yake iliondolea mbali televisheni yao, akisema: “[Kusoma] kwafurahisha nako kwanisaidia nijifunze.” Akasema mvulana wa miaka kumi: “Napenda kusoma kwa sababu ni njia ya kupata habari juu ya kitu chochote na kila kitu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki