Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/22 kur. 4-6
  • Vijana wa Leo—Je, Ni Windo Rahisi kwa Ushetani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vijana wa Leo—Je, Ni Windo Rahisi kwa Ushetani?
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Usumbufu Hatari Unaoongezeka
    Amkeni!—1990
  • Inuko na Anguko la Ushetani
    Amkeni!—1994
  • Ibada ya Shetani Katika Wakati Wetu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Muono-Ndani Juu ya Habari
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/22 kur. 4-6

Vijana wa Leo—Je, Ni Windo Rahisi kwa Ushetani?

“IBADA ya Shetani inaenea miongoni mwa vijana,” likaripoti gazeti moja la Finland la Februari 27, 1993. Kulingana na habari zilizopatikana na polisi wa Tampere, Finland, wahalifu wahusikao na biashara ya dawa za kulevya wanaingiza wachanga, na hasa wasichana, katika ibada ya kishetani. Katika visa vingi wahanga hawa na waingizwa wapya ni watoto wa kuanzia miaka 10 hadi 15.[29] “Ibada ya Shetani imepata udongo wenye rutuba miongoni mwa matineja wachanga,” likaripoti gazeti hilo.

“Kutokea kupya kwa ibada ya Shetani si elekeo la kinyumbani (la Finland) tu,” gazeti hilo likaonya. “Kwa kielelezo, gazeti la Afrika Kusini Star la Johannesburg lilionya hivi majuzi kwamba ibada ya Shetani inachochea vijana weupe wa maisha ya juu nchini.” Kwa kweli, ibada ya kishetani ni hali mbaya sana ya kimataifa kwa wazazi na vilevile watoto.

Hasa, Ushetani huahidi kwamba utapata mengi kwa kufanya machache sana. “Abudu ibilisi; fanya kazi yake chafu, naye atakupa ukitakacho. Na ndiyo sababu watoto fulani huona Ushetani ukivutia sana,” likaeleza gazeti ’Teen.

“Mimi naamini kuishi maisha kamili kabisa,” akasema tineja kijana akiriye kuwa mshiriki wa kikundi kimoja cha kishetani. “Mimi naona kani mbili katika asili: wema na uovu. Yote watu wayasemayo kuwa maovu ndiyo mambo yakufurahishayo. Madhambi huleta utoshelevu wa kihisiamoyo, wa kimwili na wa kiakili,” akasema.

Mpelelezi mmoja wa Denver, Colorado, Marekani, aliye stadi wa kuchunguza vidhehebu vya kishetani, alipoulizwa kwa nini alifikiri matineja huelekea sana kufuata Ushetani kwa urahisi, alijibu hivi: “Sitasahau kamwe aliloniambia tineja mmoja wa Kishetani. Alisema, ‘Maisha yana faida gani? Sisi tutaishilia leo na kufanya tutakalo. Hakuna wakati ujao.’”

Dakt. Khalil Ahmad, mkurugenzi wa huduma za wabalehe kwenye Hospitali ya Nova Scotia katika Dartmouth, Kanada, alitamka maoni yake juu ya uvutio wa Ushetani. “Matineja wanatafuta msisimko. Wasio na hiari imara, ambao mara nyingi ndio hupata hasara, huvutiwa na [ushetani]. Huo huwapa kujiona wenye uwezo.”

Polisi mwingine mjuzi wa Ushetani, aliye mpelelezi wa San Francisco, aonyesha tatizo lenyewe hasa: “Ulimwengu wetu ni mahali pa kutojali wengine. Sisi hujihangaikia wenyewe kuliko kuhangaikiana. Twaishi katika jamii yenye jeuri, yenye mwelekeo hasi. Watoto huona hiyo kuwa njia ya kawaida ya maisha na hivyo huvutwa ndani ya Ushetani.”

Vijana wa leo wamehusika kadiri gani katika Ushetani? “Watoto wanajiua wenyewe na rafiki zao. Tuna tatizo,” akaonya Larry Jones, msimamizi wa Mfumo wa Kuchunguza Wingi wa Uhalifu wa Vidhehebu aliye pia luteni katika kikosi cha polisi cha Boise, Idaho, Marekani. Ofisa mwingine wa polisi, kutoka jimbo la Illinois, asakaye Ushetani katika cheo chake cha mshauri-polisi wa shule ya sekondari, alisema asilimia 90 ya vijana wachezao na ibada ya ibilisi huhusika kwa sababu ni mtindo, lakini asilimia 10 “hunaswa na kuingia ndani zaidi na zaidi.”

Gazeti moja la shule katika Brooklyn, New York, School News Nationwide, Januari-Februari-Machi 1994, katika sehemu yalo ya “Dini,” lilikuwa na makala yenye kichwa “Sababu Ambayo Ushetani Huvutia Matineja.” Liliripoti: “Baada ya wavulana wawili kupigana katika mahali pa mlo wa kujipakulia kwenye shule ya sekondari, mshindi aliruka juu akapunga mkono kwa salamu ya ajabu, akiwa amekunja ngumi kwa kuinua kidole-shahada na vidole vyake vidogo. Mwalimu wa sanaa hakuweza kuelewa kwa nini watoto wengi sana walichora picha za wanaume walio kama roho waovu wenye vichwa vya mbuzi. Na vitabu vya mafumbo ya kipepo vilifuliza kupotea katika maktaba ya shule.

“Kwa kweli, watoto hao walikuwa wakichezea uwezo, nguvu za ajabu, ufumbo wa Ushetani. Kwa walio wengi, ulikuwa mchezo tu na msisimuo. Kwa wengine, lilikuwa jambo zito—zito kabisa kwa Lloyd Gamble mwenye miaka 17—aliyepoteza uhai wake katika dhabihu ya kishetani.

“Baada ya kifo cha Lloyd na kukamatwa kwa ndugu yake wa miaka 15 kwa uuaji, watu wazima wa kaunti ya Monroe walijifunza kuzielewa ishara zilizokuwa zimekuwa za kifumbo sana hapo kwanza: kiishara-mkono kilicho ‘ishara ya ibilisi,’ picha za kichwa cha mbuzi na vitabu vilivyositawisha mawazio, desturi za kiibada na minuizo ya wale matineja.”

Ripoti zaelekea kutokuwa na mwisho za vijana wasiofikia utineja na matineja wanaoua wazazi na washiriki wengine wa familia zao kwa sababu ya ibada ya Shetani. Watoto wameuawa na watoto wengine katika vitendo hivyo. Kama watu wazima wa kishetani, watoto wamekata maungo ya wanyama na kuwaua. Wanyama walio vipenzi vya familia wamedhabihiwa juu ya madhabahu ya desturi za ibada ya kishetani. Nafasi hairuhusu hata uzungumzio mfupi tu wa machinjo yafanywayo na watoto ambao wamekubali kufuata dini ya kuabudu Ibilisi.

Je, hivi ni vielelezo vya watoto wenye kucheza-cheza tu na Ushetani? Je, wale walioingilia sana ibada ya Ibilisi ni wachache sana, watu adimu tu? Wale ambao wamepeleleza wazoevu hawa wa mafumbo ya kipepo wajibu hapana. David Toma, aliyekuwa naibu wa mpelelezi kisha akawa msemaji wa kutia motisha katika vijana, alisema kwamba katika kila shule ambako yeye huhutubu, yeye huuliza swali lilelile, “Ni wangapi kati ya nyinyi watoto mwamjua mtu fulani au mmesikia juu ya mtu fulani ahusikaye katika mazoea ya Kishetani?” Akadiria kwamba “theluthi moja kamili ya wanafunzi huinua mikono yao juu.”

Kulingana na Shane Westhoelter, msimamizi wa Mfumo wa Habari za Kitaifa, kuanzia asilimia 30 hadi 40 ya wanafunzi wa shule ya sekondari yahusika katika namna fulani ya mafumbo ya kipepo. Kwa kuongezea, Westhoelter ashikilia kwamba kufikia asilimia 70 ya matendo yote ya uhalifu yaliyofanywa na matineja walio chini ya umri wa miaka 17 huchochewa na mhusiko katika mafumbo ya kipepo.

[Blabu katika ukurasa wa 5]

Ibada ya Shetani imepata udongo wenye rutuba miongoni mwa vijana wa leo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki