Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/8 kur. 21-23
  • Wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Mungu Zaidi ya Mmoja Hivi?
  • Kushindwa Kuacha Alama ya Kudumu
  • Kutafuta Waongofu Kwingineko
  • Yatakayofunuliwa na Wakati Ujao
  • Kufanya Wanafunzi wa Kweli Leo
    Amkeni!—1994
  • Nuru ya Kiroho kwa “Kontinenti Yenye Giza”?
    Amkeni!—1994
  • Mavuno ya Jumuiya ya Wakristo Katika Afrika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/8 kur. 21-23

Wamishonari Mawakili wa Nuru au wa Giza?—Sehemu 3

Wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo

Warudi Kule Ambako Yote Yalianzia

ASIA ndiyo makao ya asili ya wanadamu. Ndiko Muumba alikoanzisha ibada safi. Ingawa wanadamu waliibadilisha kwa dini bandia upesi baada ya hapo, ibada ya kweli hatimaye ilipata uendelevu katika Asia katika Israeli ya kale halafu katika Ukristo. Kwa hiyo wamishonari Wanaulaya wa Jumuiya ya Wakristo walipopeleka ujumbe wao Asia, walienda kwenye kontinenti ambako uhai wa kibinadamu na dini ya kweli zilikuwa zimeanzia. Je, wao wangetokea kuwa mawakili wa nuru au wa giza jingi zaidi?—Mwanzo 2:10-17.

Ni Nini Mungu Zaidi ya Mmoja Hivi?

Haiwezekani kuamua kwa uhakika ni wakati gani na jinsi gani imani ya Kikristo iliwasili India mara ya kwanza. Mwanahistoria wa kidini wa karne ya nne Eusebius asema kwamba yule mtume Mkristo Tomaso aliipeleka huko katika karne ya kwanza. Wengine husema kwamba “Ukristo” ulianzishwa huko kati ya karne ya pili na ya nne. Wakati wavinjari Wareno walipowasili huko mwishoni mwa karne ya 15, walipata “Wakristo wakiunda kikundi chenye kukubaliwa na kustahiwa katika jamii ya Kihindi.”—The Encyclopedia of Religion.

Padri Mhispania Francis Xavier alikanyaga kontinenti ndogo ya India katika 1542. Alikuwa mshirika wa Ignatius wa Loyola, mwanzilishi wa tabaka la kidini la Sosaiti ya Yesu, lijulikanalo kwa kawaida kuwa Wayesuiti. The New Encyclopædia Britannica humtaja Xavier kuwa “mishonari wa Katoliki ya Kiroma aliye mashuhuri zaidi wa nyakati za kisasa,” ikimwita “mwenye kutumika kama chombo cha kuanzisha Ukristo katika India, Jamii-Visiwa ya Malay, na Japani.”

Ingawa maisha ya Xavier yalikuwa mafupi kwa kulinganisha—alikufa katika 1552 akiwa na umri wa miaka 46—miaka yake kumi ya utumishi wa kimishonari ilijaa utendaji. Asemekana aliwatia wamishonari moyo wakubali kufuata desturi na lugha ya watu waliowatumikia.

Wamishonari wa kwanza wa Kiprotestanti kwenda India waliwasili katika 1706, yapata miaka 85 kabla William Carey hajachapisha An Enquiry Into the Obligations of Christians to Use Means for the Conversion of the Heathens. Uchapishaji wa kitabu hiki umeitwa “kitia-alama katika historia ya Kikristo.” Baada ya kukiandika, Carey alitumikia miaka 40 katika India akiwa mishonari.

Wakati ulipoendelea kupita, wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo walisambaa katika sehemu zote za nchi. Tabaka za watu wa hali ya chini, hasa wakataliwa-na-jumuiya, zilianza kugeukia dini za Jumuiya ya Wakristo kwa kukosa tumaini la wakati ujao ulio mzuri zaidi katika Dini ya Kihindu. Hata hivyo, The Encyclopedia of Religion yasema kwamba “elekeo hili lilikosa kukubaliwa na wamishonari wengi na idadi kubwa ya viongozi Wahindi Wakristo walioelimishwa.”

Akifunua ukosefu wa matokeo wa Jumuiya ya Wakristo, mwanahistoria Will Durant aandika hivi: “India leo huamini kwa uthabiti kama zamani tu katika miungu ambayo imepuuza kwa muda mrefu umaskini wa nchi hiyo hali moja na ukiwa wayo. . . . Wakati maoni ya uzushi au miungu ya kigeni ilipokuja kupendwa na wengi kwa njia kubwa ya kuleta wasiwasi, wao [Wabrahma] waliivumilia, kisha wakaifyonza ndani ya vungu zenye nafasi kubwa za imani ya Kihindu; mungu zaidi ya mmoja hivi hangeweza kuleta tofauti kubwa katika India.” Katika kitabu chake The Jesuits, kilichochapishwa katika 1984, Manfred Barthel asema hivi: “Wahindi walishikamana na ng’ombe wao watakatifu mwishowe; Dini ya Kihindu ilidumu muda mrefu kuliko wote Wayesuiti na Wamoguli, na leo yaonekana inapeleka miungu yayo ya ziada kwenye Magharibi ya Kikristo.”

Kushindwa Kuacha Alama ya Kudumu

Jumuiya ya Wakristo ya mapema, iliyokuwa tayari imegawanyika ikawa kanisa la Magharibi na la Mashariki, ilipatwa na mgawanyikano zaidi katika karne ya tano. Nestorius, askofu mkuu wa Constantinople, alikuja kuhusika katika ubishi mkali ulioongoza kwenye kuundwa kwa kikundi chenye kujitenga kutoka lile kanisa la Mashariki, yaani Kanisa la Kinestoria.

Wanestoria walikazia kazi ya kimishonari. Mmoja wa wamishonari wao, Alopen, yaonekana alianzisha imani za Kinestoria katika China katika 635 W.K. Lile kanisa la Magharibi, kwa upande mwingine, halikufika China mpaka karibu 1294, wakati yule ndugu-mtawa aliye mfuasi wa Francisca, John wa Monte Corvino, alipoanzisha misheni huko.

Lakini, kwa kadiri kubwa utendaji wa kimishonari katika China haukuanza hadi kuwasili kwa Matteo Ricci, Myesuiti Mwitalia, katika miaka ya 1580. Uprotestanti ulipokuwa uking’ang’ania kuimarisha guu lao katika Ulaya ya baada ya Marekebisho ya Kidini, Ukatoliki ulikuwa ukijishughulisha kutafuta waongofu nje ya Ulaya. Kampeni za uvinjari za Ureno na Hispania, yote mawili yakiwa ni mabara yenye kufuata sana Ukatoliki, zilisaidia sana majaribio ya kanisa ya kufanya hivyo.

Wamishonari wa karne ya 17 na ya 18 walipata kadiri fulani ya mafanikio yawezekana kwa sababu “idadi kubwa ya [hao] (hasa Wayesuiti) ilisitawisha mtazamo wa kuvumilia sana maoni ya wengine,” kama vile kisemavyo The Cambridge History of China. Profesa wa historia ya Kichina Hans H. A. Bielenstein afafanua hivi: “[Wayesuiti] walikazia mifanano kati ya Ukristo na Dini ya Confucius, wakimsawazisha Mungu wa Kikristo na Mbingu ya Kichina, bila kutokeza katao lolote juu ya kuabudu mababa waliokufa. Hii yaeleza ni kwa nini Wayesuiti walifanya waongofu katika milki fulani-fulani, lakini pia ni kwa nini hawakuacha alama yoyote ya kudumu.”

Katika 1724 maliki Mchina alishutumu peupe dini za Jumuiya ya Wakristo na kufukuza walio wengi wa wamishonari wa kigeni. Wamishonari Wakatoliki walirudi, fursa ilipowawezesha. Wamishonari Waprotestanti walijiunga nao, huku Robert Morrison kutoka Sosaiti ya London ya Wamishonari akiwa miongoni mwa walio wa kwanza kuwasili, katika 1807. Alianzisha koleji iliyokusudiwa si kueneza imani zake tu bali pia kujulisha China kwa utamaduni wa Magharibi na kujulisha wanafunzi wa Magharibi kwa utamaduni wa Mashariki. Kufikia 1819, Morrison alikuwa amemaliza tafsiri ya Biblia nzima kwa msaada wa William Milne.

Wamishonari fulani walijitoa kuleta aina tofauti ya nuru. Dakt. Peter Parker akawa ndiye mishonari wa kwanza wa kitiba kwenda China, akisaidia kupanga kitengenezo Sosaiti ya Kitiba ya Kimishonari iliyoanzishwa Canton katika 1838. Wamishonari wengine walijitoa kufuatia mambo ya kielimu, kuunga mkono jitihada ngumu za kufadhili wanadamu, au kutatua matatizo ya kijamii. Kulingana na The Cambridge History of China, kiasi fulani cha kazi ya tafsiri waliyofanya wamishonari ‘ilifaa zaidi kwa kufanya Ulaya ipate uelewevu mwingi zaidi juu ya China kuliko kuisitawisha hali ya Wachina ya kuupokea Ukristo.’

Wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo walishindwa pia kuwapa Wachina kielelezo cha muungamano na udugu wa Kikristo. Waprotestanti ndio hasa waliokosa muungamano. Katika muda wa miongo minne wamishonari wao waliongezeka kutoka 189 hadi 3,445. Kufikia 1905 kila moja ya zile sosaiti 60-na-zaidi za kimishonari ilikuwa ikieneza namna yayo yenyewe ya fundisho fulani hususa la Kikristo. Wamishonari Wakatoliki pia waliweka mfano usiofaa wa vile Ukristo upasavyo kuwa. The Cambridge History of China yataja “lile zoea lililoenea kwa mapana la kuingilia mambo ya kienyeji ya kisiasa na ya kihukumu ili kuwapata watu wawezao kuwa waongofu.”

Kutafuta Waongofu Kwingineko

Chini ya karne moja baada ya mvinjari Mreno Ferdinand Magellan kukanyaga Visiwa vya Filipino kwa mara ya kwanza katika 1521, wamishonari Wakatoliki huko walikuwa wamebatiza watu karibu milioni mbili. Leo, asilimia 84 ya idadi ya watu huko ni Wakatoliki wa Kiroma. Mfumo wa kielimu ulioanzishwa na kanisa bila shaka wasaidia kueleza sababu ya mafanikio haya. Lakini kisababishi kingine kisichopasa kuachiliwa, asema mwandikaji mmoja, ni kwamba wamishonari hao ‘waliwaruhusu waongofu kubaki na nyingi za imani na mazoea yao ya kidini.’

Kanisa lilipata mafanikio machache kwingineko. Kwa kielelezo, idadi ya Wakatoliki katika Japani ni asilimia 0.3 tu kati ya Wajapani wote. Katika Jamhuri ya Korea, tarakimu yaikaribia-karibia alama ya asilimia 6.

Japani ilipata mgusano wayo wa kwanza na Wanaulaya katika 1542. Katika 1549, mishonari Myesuiti Francis Xavier, pamoja na waandamani wachache, alipokewa kwa urafiki. Muda si muda idili hii ya mwanzo ilipoa wakati viongozi Wajapani ‘walipoanza kushuku kwamba utendaji wa kimishonari wa Ulaya huenda ukawa utangulizi wa kushindwa kisiasa na yule mfalme Mhispania (kama walivyojua ilikuwa imetokea katika Filipino),’ aandika profesa wa historia J. Mason Gentzler.

Katika 1614 “wamishonari waliharamishwa kuwa adui za serikali kisha maliki akaamrisha kwamba Ukristo haungevumiliwa tena katika milki zake. . . . Waongofu waliokataa kuikana ile dini mpya walisulibiwa kwa makumi ya maelfu . . . , hali maogofyo mabaya zaidi yaliwekwa akiba kwa wamishonari hao . . . waliochomwa kwa moto au wakakaangwa wakiwa hai, wakakatwa maungo, wakatupwa ndani ya mashimo yaliyojaa nyoka wenye sumu,” miongoni mwa matendo mengine ya unyama.—The Jesuits.

Ukatoliki ulianzishwa Korea katika 1784, nao Uprotestanti ukaanzishwa karne moja baadaye. Huu wa mwisho “ulikua upesi zaidi kwa sababu wamishonari Wamarekani walileta si ile Gospeli tu bali pia elimu, dawa na tekinolojia,” laeleza gazeti Time. Sera hii ya kufanya waongofu kwa njia nyinginezo ambazo ni zaidi ya ufunzi wa kidini tu yaonekana ingali ikitumika. Profesa wa falsafa Son Bong Ho wa Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Seoul anukuliwa kuwa akisema hivi: “Makanisa yale ambayo yamekazia baraka za vitu vya kimwili yamekua upesi kuliko madhehebu yale makubwa-makubwa.”

Yatakayofunuliwa na Wakati Ujao

Twapaswa kuwaonaje wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo wa wakati uliopita? Kile walichowakilisha hakikuwa namna safi ya ibada iliyoanzishwa na Yesu. Hata hivyo, wengi wao bila shaka walikuwa na moyo mweupe. Vyovyote vile, waliitafsiri Biblia katika lugha nyingi za kienyeji na kufundisha angalau mawazo fulani ya Biblia.

Namna gani wamishonari wa Jumuiya ya Wakristo walioenda Afrika, ambayo imeitwa ile Kontinenti Yenye Giza? Soma juu ya hili katika toleo letu linalokuja katika makala “Nuru ya Kiroho kwa ‘Kontinenti Yenye Giza.’”

[Sanduku katika ukurasa wa 23]

“Yehova” Katika Biblia ya Kichina

John W. Davis, mishonari na mtafsiri wa karne ya 19 alisababu hivi: “Ikiwa Roho Mtakatifu asema Yehova mahali popote pale katika Kiebrania, mbona mtafsiri hasemi Yehova katika Kiingereza au Kichina? Ana haki gani ya kusema, nitatumia Yehova katika mahali hapa na kibadala chalo katika mahali pale? . . . Ikiwa katika kisa chochote kile ni kosa kutumia Yehova katika tafsiri hiyo mbona basi mwandikaji aliyepuliziwa alilitumia hapo awali?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki