Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/22 kur. 11-12
  • Wakati Mengi Yahitajiwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Mengi Yahitajiwa
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wakati Ujao
  • Kulikabili Hilo Tatizo
    Amkeni!—1997
  • Kulea Mtoto Aliye Mgumu
    Amkeni!—1994
  • “Kaa Tuli na Ukaze Fikira!”
    Amkeni!—1997
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/22 kur. 11-12

Wakati Mengi Yahitajiwa

INGAWA mengi ya madokezo katika makala iliyotangulia yaweza kusaidia sana, wakati fulani msaada zaidi huhitajika katika hali hususa. Machunguo ya uhusiano wa visababisha ukuzi na mazingira yatia ndani, kwa kielelezo, ripoti za watoto ambao si tu wasisimukaji bali walio hatari sana. Watoto hawa, hata ingawa watunzwa na familia zenye upendo, hutokeza tabia zao za kuharibu kwa kuvunja-vunja vitu, kupigia watu kelele, kuanzisha mioto, kufyatua bunduki, na kuchoma kwa visu (vikiwako), na kuumiza wanyama, watu wengine, ama wao wenyewe, ikitokea akilini mwao kufanya hivyo. Kihalisi, wao ni kifanani cha fujo.

Kama wapate ama wasipate msaada wa kitiba, ili kupata utunzi bora wa mtoto wao, ni uamuzi wa kufanya kibinafsi. Kila familia lazima iamue jinsi ya kukabiliana na mahitaji mbalimbali ya mtoto wao, wakiwa akilini na uhakikisho wenye kufariji uliopewa kwa wazazi kwenye Mithali 22:6.

Moja ya matibabu yenye kubishaniwa zaidi, sasa ni suala la kutumia dawa. Dawa inayopendekezwa kila mara, Ritalin, imekuwa na matokeo mchanganyiko. Familia nyingi zimependezwa sana na maendeleo ya mtoto wao anapotumia Ritalin ama dawa nyingine zinazorekebisha utendaji. Hata hivyo, mjadala unaendelea sasa, si kuhusu ule uwezo ufaao tu wa dawa hizi bali kuhusu kule kupendekezwa kwazo kupita kiasi. Hakika, madaktari fulani hupiga thamani yazo kabisa, wakisema, kwa kielelezo, kwamba Ritalin ikitumiwa kwa kipindi kirefu yaweza kuwa na athari nyingi zenye madhara. Hata hivyo, lazima ikaziwe tena kwamba familia nyingi na madaktari hutaja athari chache mbaya pamoja na tabia iliyoboreka na ya kielimu. Kwa kupendeza, watu wazima wengi waliopatikana kuwa na ADD na wanaotumia dawa hizo wanafurahia matokeo pia. Hivyo basi, kutumia dawa ni uamuzi wa kibinafsi unaotegemezwa na utafiti wa uangalifu na kwa ukadirio.

Kwa wale ambao wamejaribu kutumia dawa na wakawa na matokeo mabaya, kuna njia za badala ya matibabu. Familia nyingi zilisoma kuhusu na kupata matokeo mazuri kwa kutumia vitamini na matibabu ya miti-shamba ama muunganisho wa yote mawili. Kama ilivyotaarifiwa mapema, ADD/ADHD yaweza kusababishwa na hali fulani kwa kutosawazika kwa kibiokemia ndani ya ubongo ambako matibabu haya huaminiwa kuwa huweza kurekebisha.

Kwa kuongezea, kuna visababishi vingine ambavyo wengine huamini huanzisha mengi ya matatizo yahusianayo na ADD/ADHD. Dakt. Doris Rapp, katika kitabu chake Is This Your Child?, husema kwamba “watoto fulani wana ugonjwa wa kimwili na/ama kihisia-moyo, kitabia, na matatizo ya kusoma yanayohusiana kwa sehemu ama kwa msingi na mzio ama hali ya kimazingira.” Pia, miitikio kwa dai za rangi, sukari, na vikolezo mbalimbali huenda kwa kweli yaigize matatizo haya kwa hamaki, kubadilika kwa mahasa ghafula, na kukosa usingizi.

Familia nyingi zimejifunza jinsi ya kurekebisha tabia ya watoto wao, hata hivyo utendaji wao wa kielimu waweza kutokeza tatizo la ziada. Kwa wengine, huduma za kipekee kama vile ukufunzi, ushauri, vikundi vya kuhimiza, na walimu wa kipekee huenda wasaidie. Kwa sababu watoto hawa huonekana wafanya vema katika mpango wa ana kwa ana, familia fulani, kwa madokezo ya daktari wao, zimepata mafanikio kwa mafunzo ya nyumbani.

Miradi mingi mipya ya kielimu si ya kupuuzwa pia, kama ule wa Dakt. Mel Levine Schools Attuned, ambao hutaja kwa sifa upekee wa kila mmoja na utofauti-tofauti wa watoto. Programu ya Dakt. Levine hutetea ubuni wa desturi ili kutosheleza mahitaji ya kila mtoto. Popote mfikio huu ulio tofauti-tofauti katika kusoma umeanzishwa katika Marekani, matokeo yaonekana kuwa yalikuwa mazuri.

Wakati Ujao

Kulea watoto kwaweza kulinganishwa na kununua makao mapya. Yote mawili huhitaji masurufu ya maisha; hata hivyo, kwa sababu ya hali, wanunuzi wanaotarajia kununua huenda walazimike kuridhika na kiwango kisichotimilika. Vivyo hivyo, wazazi wasio wakamilifu wanaolea watoto wasiokamilika katika ulimwengu wa Shetani wanalazimika kuridhika na kiwango kisichotimilika. Makao yaliyonunuliwa karibuni huenda yakawa na sehemu zisizopendeza, lakini kwa kufanya kazi na kufikiri kidogo, sehemu nyingi zisizopendeza zaweza kuondolewa karibu zote. Hata sehemu iliyo ngumu kurekebisha kiufundi yaweza karibuni kuwa sehemu yenye kuvutia sana ya makao hayo.

Vivyo hivyo, ikiwa wazazi watabadilikana kwa kila uhitaji wa mtoto asiye wa kawaida, yeye aweza kuwa sehemu yenye urembo ya maisha zao. Kila mtoto lazima athaminiwe kwa sifa zake mwenyewe. Hivyo basi, kaza macho kwa zile zilizo chanya. Badala ya kufinya watoto, tia moyo ubuni wa kila mmoja, na thamini kwamba yeye ni mtu mstahika astahiliye heshima na upendo—zawadi yenye thamani kutoka kwa Yehova Mungu.—Zaburi 127:3-5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki