Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/8 kur. 3-4
  • Kuungua Nishati Ni Zamu Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuungua Nishati Ni Zamu Yako?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuungua Nishati Ni Nini?
  • Kuungua Nishati—Waweza Kuikabilije Hali?
    Amkeni!—1995
  • Kuungua Nishati—Ni Nani Aliye Hatarini na kwa Nini?
    Amkeni!—1995
  • Jinsi ya Kukabiliana na Uchovu Mwingi
    Amkeni!—2014
  • Ninaweza Kuepukaje Uchovu wa Kupita Kiasi?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 1/8 kur. 3-4

Kuungua Nishati Ni Zamu Yako?

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA JAPANI

“Watumishi wa hoteli katika Sweden, walimu katika Japani, wafanyakazi wa posta katika Marekani, madereva wa basi katika Ulaya na wafanyakazi wa mitambo yenye milolongo ya bidhaa kila mahali wanaonyesha ishara zinazoongezeka za mkazo wa kazi.”—MAINICHI DAILY NEWS.

NOBUAKI alichoka sana. Kwa kufanya kazi mchana na usiku, alikuwa ameajiri waajiriwa wapya 130 kwa muda wa miezi minne. Alikuwa ndiye meneja wa tawi jipya la mfumo wa masoko makubwa-makubwa ya mjini katika Japani, na kwa jitihada alizofanya chini ya msongo wa kazi, akawa ameajiri watu walioshindwa kutimiza viwango alivyotarajia. Walipigana na kulalamika juu ya hali yao ya kazi. Isitoshe, mwajiriwa wa kiume alitoroka na mwajiriwa wa kike. Nobuaki alikuwa akiumwa na kichwa mara nyingi kila siku. Muda si muda akawa hawezi kwenda kazini, na siku zile alizojilazimisha kwenda, alikuwa akija nyumbani mara hiyo. Alikuwa ameungua nishati, kama ujiti wa kiberiti ambao umezimika hatimaye.

Wake wakaao nyumbani wakati wote huungua nishati pia. Baada ya miaka miwili ya kuwa nyumbani pamoja na watoto wake watatu, Sarah alikosa sana subira kwao. “Nilihisi kama kwamba nilikuwa nikifanya kazi na kufanya kazi na kufanya kazi tu, sawasawa na kuwa katika shimo lisilo na kikomo,” akatamka. Mama-watoto afanyapo kazi ya kimwili na tena kulea watoto, uwezekano wa kuungua nishati huongezeka. Betty, akiwa katika miaka yake ya 40, alijikuta katika hali ya kusawazisha umama na kazi-maisha fulani, kujaribu kutimiza mafungu yote mawili hadi ukamilifu. Alijaribu kupendeza kila mtu—mume wake, watoto wake, mwajiri wake, na wafanyakazi wenzake. Msongo wake wa damu ulipanda, na matukio madogo yalimuudhi. Aliungua nishati.

Kuungua nishati hugonga majeruhi wasiotarajiwa pia. Shinzo, mhudumu Mkristo hodari, alikuwa mwenye zihi na mawazo bora. Alienda kusaidia mahali ambapo palikuwa na uhitaji mkubwa wa walimu Wakristo. Hata hivyo, katika muda wa miezi michache, alihisi amechoka kabisa, akajifungia chumbani mwake mchana kutwa. Alihisi kama kwamba alikuwa katika handaki lisilo na mtokeo. Alitatizika kuamua mambo, hata juu ya atakachokula mchana. Hakuhisi akitaka kufanya lolote. Alikuwa ameungua nishati kabisa.

Kuungua Nishati Ni Nini?

Basi kuungua nishati ni nini? Herbert Freudenberger na watafiti wengine walianzisha neno hili katika miaka ya katikati ya 1970, nalo likaja kueleza “hali ya kuchoka kabisa kutokana na kujihusisha na watu katika hali zenye kudai utumizi mwingi wa hisia-moyo.” Pia, “kuchoka kabisa kimwili au kihisia-moyo, hasa kutokana na mkazo au anasa za utapanyaji.” (American Heritage Dictionary) Hata hivyo, kuna tofauti ndogo-ndogo katika fasili ya neno hili, ikitegemea mtafiti mwenyewe.

Ingawa kuungua nishati hakuna fasili halisi ya kitiba, majeruhi hutambuliwa kwa dalili kama vile uchovu, kukosa idili, kuwa hoi, kukosa tumaini, na unyong’onyevu. Jeruhi huhisi amechoka kabisa na huudhiwa na matukio madogo. Hakuna cha kumchochea atende. Kila kitu huonekana kinamlemea, na huenda akatafuta ovyo msaada kwa mtu yeyote yule amwonaye. Jitihada zote kazini na nyumbani huenda zikaonekana za bure tu. Hisia ya kukosa tumaini hutawala. Ikiwa wewe una dalili hizi pamoja na unyong’onyevu, kukosa kufurahia kitu chochote, basi ingeweza kuwa unaungua nishati.

Kuungua nishati kwaweza kuathiri kazi na maisha ya familia. Wapaswa kuepuka hilo. Lakini jinsi gani? Ili ujue, acha kwanza tuone ni nani wenye mwelekeo wa kuungua nishati na kwa nini.

[Sanduku katika ukurasa wa 4]

Dalili za Kuungua Nishati

“Kuungua nishati-kazi hurejezea hali ya kisaikolojia yenye kudhoofisha iletwayo na mkazo wa kazi usioondolewa, ambao hutokeza:

1. Akiba za nishati zilizodhoofika

2. Nguvu zilizopungua za kukinza ugonjwa

3. Ukosefu wenye kuongezeka wa uradhi na kuwa na matazamio mabaya

4. Kukosa kwenda kazini kwa kadiri yenye kuongezeka na kukosa matokeo kazini.

“Hali hii inadhoofisha kwa sababu ina uwezo wa kuwalegeza, hata kuwamaliza nguvu kabisa, watu ambao kwa kawaida huwa wenye afya, wenye nishati, na hodari wa kazi. Kisababishi chayo cha msingi ni mkazo usioondolewa, wa aina iendeleayo siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka.”—The Work/Stress Connection: How to Cope With Job Burnout, na Robert L. Veninga na James P. Spradley.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki