Je, Mna Kipepeo-Madoido Katika Shamba Lenu?
IKIWA mnao, utasisimuka kwa urembo wao. Kipepeo-madoido ni nini? Ni mojapo ya maelfu ya aina ya vipepeo ambavyo hurembesha ulimwengu wetu na mojapo ya spishi zaidi ya 750 ziwezazo kupatikana katika Marekani na Kanada. Mmoja anayeonyeshwa hapa, great spangled, alipigwa picha katika shamba la majani eneo la mashambani la Virginia. Great spangled huonyesha mapaku magavu ya kifedha kwenye sehemu ya chini ya mabawa ya nyuma. Mtunza-bustani hii alipanda maua-mwitu yawayo marefu katika kisehemu fulani cha bustani ili kuvutia vipepeo—kulikuwa na mimea ya rudbekisia manjano na Floksi-urujuani.
Ikiwa ungependa kuwavutia vipepeo katika shamba lako, jaribu kukuza maua-mwitu katika sehemu fulani ya shamba. Labda waweza kununua paketi ya mbegu za maua-mwitu yatakayokua kuwa unamna wenye kupendeza wa rangi uwezao kuvutia viumbe hawa wahitajio uangalifu sana. Ikiwa unaishi katika eneo lifaalo la ulimwengu, kichaka cha budleia kitavutia vipepeo kama vile sumaku. Kisha chukua kamera na darubini ya macho mawili, na ujifurahishe!