Kaa Mwenye Ladha Isiyo ya Kawaida
Na mleta-habari wa Amkeni! katika Visiwa vya Solomon
KAANAZI—je, hilo lasikika kuwa la kigeni?a Hupatikana katika mahali pachache tu, kutia ndani visiwa vya New Georgia, sehemu ya Visiwa vya Solomon.
“Kaanazi? Ndiyo, wapo hapa,” waeleza wenyeji, “lakini utahitajika kwenda kuwatafuta usiku.” Kaa hawa wa usiku hutumia wakati wa mchana ndani katika vitovu vyenye uwazi vya miti inayooza katika vichaka vilivyosongamana vya misitu. Wakija nje usiku, hujilisha, ndiyo, kwa nazi, ambazo kutoka kwa hizo wanararua makumbi kwa vibano vyao vyenye nguvu mno, lakini wao hula pia mimea mbalimbali ya kijani iliyo laini. Ili kuona kiumbe hiki chenye kuvutia, mtu lazima atafute ishara zenye kujulisha za makumbi yaliyoraruliwa yaliyoachwa penye kiingilio cha uwazi mweusi katika mashina yanayooza ya miti iliyoanguka.
Wanakisiwa wanaeleza kwamba wakati wa Juni na Julai, kaa hao huchimba ardhini, na hapo, baada ya kuambuka gamba la nje, wanakuza gamba jipya lililo kubwa zaidi kabla ya kujitokeza. Kwa kuwa kaanazi wengine huishi hadi miaka 50, mtu aweza kuthamini saizi kubwa mno wanazoweza kufikia. Nilipokuwa nikitazama, mmoja alitokeza kutoka chimbo lake, akiwa na urefu wa mguu wa yapata sentimeta 50.
Kwa kusikitisha, usalama unaodhaniwa wa chimbo lao la kuambukia si kinga dhidi ya mwindaji, ambaye anaweza kutambua shimo la kimviringo ardhini linaloonyesha mwanzo wa chimbo. Mara kiumbe huyo asiyeweza kujikinga aburutwa nje, akiamuliwa kimbele kwa ajili ya meza ya mtaalamu wa vyakula. Mikahawa katika Asia humgharimisha sana kaa huyu, hasa nyama iliyoko kwenye, maungo yake ya nyuma yaliyo laini, ya mviringo.
Kwa hivyo hapa katika Visiwa vya Solomon, uwezekano wa kutoweka kwa kaanazi ni jambo lenye kuhangaisha kikweli. Idara ya Uvuaji Samaki huweka kipimo juu ya idadi ya kaa jike wenye kutaga mayai na juu ya kaa wanaoweza kuuzwa nje ya Kisiwa. Wengine wamedokeza kuwekwa kwa mashamba ya kufugia ambayo kwayo kaa hao wanaweza kuachiliwa kuingia katika makao yao ya asili. Lakini utafiti zaidi ungehitajika, kwa kuwa yajulikanayo kuhusu tabia zao za uzazi hayatoshi.
Kisa cha idadi ya kaanazi inayodidimia chakazia zaidi uhitaji wa mfumo wa ulimwengu ambao utasitawisha mazingira yaliyosawazika. Chini ya huo, kila kimoja chini ya aina ya viumbe hai kwenye mazingira ya viumbe vya Muumba wa kidunia kinaweza kufanya sehemu yacho katika kutimiza unabii wa Zaburi 148:5-10: “Na vilisifu jina la BWANA [“Yehova,” NW], kwa maana aliamuru, vikaumbwa. . . . Msifuni BWANA [“Yehova,” NW] kutoka nchi, . . . Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.”
[Maelezo ya Chini]
a Hujulikana pia kuwa robber crab.