Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Sayari Isiyojulikana”
  • Badiliko la Haraka la Maadili Katika Kanada
  • Mwono-Mbele wa Karne ya 20
  • Mpando wa Uhalifu Katika Japani
  • Hatari za Kutiwa Damu Mishipani
  • Sehemu za Dubu
  • Spishi Zilizohatarishwa za Brazili
  • Watu Walioko Sayarini
  • Uhusiano Bora Ndio Ufunguo
  • Mfumo Tata wa Viumbe
    Amkeni!—2001
  • Spishi Zilizo Hatarini mwa Kutoweka—Mweneo wa Hilo Tatizo
    Amkeni!—1996
  • Sababu Inayofanya Spishi Ziwe Hatarini
    Amkeni!—1996
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

“Sayari Isiyojulikana”

Spishi tatu za nyani ambazo hazikujulikana awali zilipatikana kwenye misitu ya mvua ya Amazon katika muda wa miaka miwili tu. Ulimwenguni pote, wastani wa spishi mpya tatu za ndege huvumbuliwa kila mwaka. Kwa kukadiria spishi 1,200 za mbawakawa zilipatikana katika uchunguzi wa miti 19 katika Panama, na asilimia 80 yazo haikujulikana awali. Likaandika gazeti UNESCO Sources: “Idadi kubwa ya uhai yabaki bila kujulikana kwetu.” Kwa mfano, “asilimia 40 iliyokadiriwa ya samaki wa maji matamu wa Amerika Kusini yabaki kubainishwa. . . . Na ni nini tutapata katika vilindi vya bahari kuu ambavyo havijapata kuvinjariwa?” Tatizo huzidi unapofikiria idadi kubwa ya aina ndogo za uhai: bakteria, uyoga, nematodi, araknidi, wadudu, na mimea ambayo bado kuvumbuliwa. “Kwa kielelezo, gramu moja ya udongo wa kitropiki, yaweza kuwa na bakteria na vijiumbe maradhi vingi kufikia milioni 90.” Wengine hukadiria kwamba idadi ya spishi duniani huenda ikawa “ya juu kufikia milioni 200,” lasema UNESCO Sources. Licha ya uvinjari mwingi, dunia bado yabaki “sayari isiyojulikana.”

Badiliko la Haraka la Maadili Katika Kanada

“Kwa muda wa chini ya kizazi kimoja, Wakanada—Waingereza pamoja na Wafaransa—wamekataa mamlaka ya kanisa, ya serikali na umilikaji na ukuzaji uliokuwa ukiandaa faraja na utaratibu katika maisha ya kila siku na ya kijamii,” laripoti The Toronto Star. Kwa nini? Wanataka kujipatia mali mara moja. Kuna lile jaribio la “kuvipata vyote” sasa. “Kanuni za maadili za dini ya Kiyahudi na Ukristo zimebadilishwa na falsafa za kibinadamu, kanuni za kidesturi za Katoliki zimebadilishwa na falsafa za mali kwanza. Wachache wako tayari kuacha utafutaji wa mali kwa maisha ya baadaye, bila kutaja uzee wa mmoja,” likaongezea Star. Kamwe Mungu haonwi kuwa asiye wa kiasili. Basi, hakuna hofu, hakuna hisi za hatia. Mapendezi ya kiroho yaumia jitihada zote zielekezwapo kuelekea kupata upeo wa thawabu za ulimwengu wa mali.

Mwono-Mbele wa Karne ya 20

Je, mtu yeyote aliyeishi katika karne iliyopita angewazia maendeleo ya siku ya kisasa kama vile yale ya magari, usafirishaji mkubwa, muziki wa kielektroni, na mashine za faksi? Katika 1863, mwandikaji wa hadithi za kubuni Mfaransa Jules Verne, anayejulikana sana kwa kazi yake ya uandishi kama vile Around the World in 80 Days na 20,000 Leagues Under the Sea, alitabiri maendeleo hayo na mengi zaidi katika hadithi ya kubuni ambayo ilikuwa bado kuchapishwa wakati huo, yenye kichwa Paris in the 20th Century. Ingawaje mchapishaji wa Verne aliikataa kuwa isiyowazika na kuaminika, uandishi huo uliovumbuliwa majuzi ulifunua kwa usahihi wa kustaajabisha maisha katika karne yetu ya 20, kutia ndani silaha za hali ya juu, kiti cha umeme cha kufishia, uchafuzi, misongamano. Verne aliona kimbele halaiki ya watu iliyofikwa na magumu ambayo imepoteza upendezi katika mafanikio yaliyopita ya ustaarabu na utamaduni, jamii inayotumikishwa na ubiashara na uraibu kwa tekinolojia. International Herald Tribune ya Paris likaandika hivi: “Verne hakutabiri tu hatua za kisasa za kitekinolojia, bali pia alitambua baadhi ya matokeo yenye kuhofisha.”

Mpando wa Uhalifu Katika Japani

Japani, ambayo kufikia hivi majuzi ilifikiriwa kuwa isiyo na uhalifu kwa kulinganishwa, inapata ono la mpando katika uhalifu kwamba polisi waulaumu mshuko, ongezeko la uingizaji wa bunduki nchini bila ruhusa, na udidimiaji wa nguvu za magenge ya wahalifu uliopangwa. Kulingana na ofisa wa polisi Takaji Kunimatsu, uhalifu wa kutumia bunduki umefikia kiwango cha juu na, usipoangaliwa, ‘utatikisa kabisa misingi ya utaratibu wa umma’ katika Japani. Kulingana na Mainichi Daily News, uhalifu unaotendwa na “watu wa kawaida” pia unazidi kuongezeka, kwa sehemu ukisababishwa na “msongo usiopunguka kutoka maeneo yenye msongamano wa watu mjini.” Ili kusaidia wakaa-mjini kumudu, profesa wa elimu ya kijamii Susumu Oda alitoa madokezo kadhaa: Dumisha ustahifu wa kawaida, kama vile kuitikia salamu, kusema “tafadhali” inapofaa, na kutabasamu “ili kufyonza maoni yoyote ya uadui.” Jifunze ustadi wa kukataa kwa upole. Liwe zoea lako kutumia mnyororo wa ulinzi kwenye milango. Waone polisi kuwa waungamani. Na “usione mazoezi ya mikabala ya mikono kuwa njia ya kujilinda kutokana na uhalifu—yaelekea zaidi kumjeruhi mmoja vibaya sana.”

Hatari za Kutiwa Damu Mishipani

“Ugavi wa damu wa Kanada ungeweza kufanyiwa uchunguzi kwa mileani moja kutoka sasa na hatari za kutiwa damu mishipani zingekuwako bado,” likaripoti The Toronto Star. Akithibitisha mbele ya tume inayochunguza usalama wa ugavi wa damu wa Kanada, Dakt. William Noble wa Hospitali ya St. Michael alisema hivi: “Zimekuwako (hatari) na sikuzote zitakuwako.” Hatari za kutiwa damu mishipani hutia ndani “chochote kiwezacho kutokeza itikio la mzio hadi kuambukizwa UKIMWI kutoka damu iliyotolewa mchango,” lasema Star. Wastadi wanaopendekeza utiaji damu mishipani wadai kwamba wagonjwa zaidi na zaidi leo wanafadhaika kuhusu kuambukizwa UKIMWI kutokana na damu. Dakt. Noble asema hivi: “Hakuna siku inayopita bila kuwa na maongeo kuhusu ‘Je, nipendekeze kutia damu au la?’”

Sehemu za Dubu

“Kufanya magendo ya sehemu za dubu mweusi kutoka Kanada kwaweza kuwa kwenye faida kuliko kushiriki katika biashara ya kimataifa ya dawa za kulevya,” ladai The Toronto Star. Kuna uhitaji usio wa kawaida wa kibofu cha nyongo na makucha ya dubu mweusi na wauguzi wa dawa za kienyeji katika nchi tajiri zaidi za Asia, kama vile China, Korea Kusini, Japani, Taiwan, na Hong Kong. “Ofisa mmoja wa polisi wa California wa kukumbana na biashara hiyo amekadiria ‘thamani ya mitaani’ (thamani kwa mtumiaji wa mwisho) ya kilo moja ya kibofu cha dubu katika Asia ilipanda kuwa zaidi ya dola milioni 1 (za Marekani) kufikia wakati nyongo ilizimuliwa na nyongo ya ng’ombe ama nguruwe,” laongezea Star. “Kwa kulinganisha, thamani ya mitaani ya kokaine katika Metro Toronto imekadiriwa kuwa dola 100,000 kwa kila kilogramu.” Mtaalamu wa spishi zilizohatarishwa Carole Saint-Laurent, wa Hazina ya Wanyama Ulimwenguni/Kanada, asema hivi: “Ni biashara kubwa mno.” Kuna hofu kwamba uhitaji wa sehemu za dubu utazidi kuongezeka sana. Idadi ya dubu tayari kwa kiasi kikubwa imefyekwa katika Asia.

Spishi Zilizohatarishwa za Brazili

“Brazili ina misitu ya kitropiki mara tatu kuliko nchi nyingine yoyote ile, ni kiongozi wa ulimwengu katika wingi wa kibiolojia, na bado ina unamna mwingi wa uasili wa mamalia, spishi 460, katika eneo layo,” lasema gazeti O Estado de S. Paulo. “Lakini Brazili pia ndiyo kiongozi wa spishi zilizohatarishwa, 310, ambazo kati yazo 58 ni mamalia.” Ingawaje kufikia sasa hakuna mamalia iliyotoweka kabisa, “asilimia 12 ya mamalia za Kibrazili ziko hatarini,” kama vile “simba-tamarini, apatikanaye katika Brazili pekee.” Baadhi ya spishi zilizohatarishwa “huishi katika maeneo mazuilifu hivi kwamba usumbufu wowote wa mazingira yao ya asili waweza kutokeza kutoweka kwao.” Kulingana na gazeti hilo, spishi huamuliwa kuwa imetoweka ikiwa miaka 50 itapita bila kupata visukuku vyayo porini.

Watu Walioko Sayarini

Kulingana na tarakimu zilizofanywa na UNFPA (Hazina ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu), idadi ya watu kwenye sayari ilifikia bilioni 5.66 katikati ya 1994. Utabiri wakadiria kwamba idadi itaongezeka hadi bilioni 6 kufikia 1998, bilioni 8.5 kufikia mwaka 2025, na bilioni 10 kufikia 2050, mwingi wa ukuzi huu ukitukia katika Asia, Afrika, na Amerika ya Kilatini. Afrika, ikiwa na kiwango cha ukuzi cha mwaka cha asilimia 2.9, ndilo eneo lenye ukuzi wa kasi mno kupita yote duniani. Ulaya ni ya chini kupita yote—asilimia 0.3. UNFPA pia lataarifu kwamba kufikia mwishoni mwa karne, miaka mitano tu kutoka sasa, nusu ya idadi ya watu duniani wataishi katika maeneo ya mjini. Kufikia wakati huo, majiji 300 katika nchi zinazositawi yatakuwa na zaidi ya watu milioni moja, ikilinganishwa na majiji 125 leo.

Uhusiano Bora Ndio Ufunguo

“Ndiyo aina ya uhusiano wabalehe wanao—na si ule wa kifamilia—hilo huonyesha kama wabalehe watatumia dawa za kulevya ama kuwa na matatizo ya kitabia,” lataarifu The Toronto Star. Uchunguzi uliofanywa na Wakf wa Utafiti wa Uraibu kwa vijana 2,057 katika Ontario ulifunua kwamba “asili ya mahusiano ya familia yana matokeo yenye nguvu kuliko muundo wa familia yenyewe,” akasema mwanasayansi Ed Adlaf. Wabalehe walio katika mahusiano mazuri ya familia, hata ikiwa ni wazazi waliowahodhi ama wa kambo ama mama walio peke yao, waliendelea vizuri kuliko wale walio katika familia zilizokamili ambapo mahusiano mabaya yapo. “Wale ambao kwa kawaida huzungumza matatizo yao na wazazi walikuwa na kiwango cha chini kabisa cha utovu wa tabia,” likasema Star. “Wale ambao hawazungumzi kamwe na mzazi yeyote kuhusu matatizo walikuwa na viwango vya juu zaidi vya uraibu wa alkoholi, matumizi ya dawa za kulevya na utovu wa nidhamu.” Kiasi ambacho wabalehe hutumia na familia zao, ubora wa mahusiano yao, na kama wazazi hufuatilia mahali watoto walipo na utendaji wao ama la ni visababishi vya msingi katika kupunguza matatizo. Adlaf akasema hivi: “Ni muhimu kutumia wakati na kutafuta wakati ili uwe pamoja na watoto.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki