Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Michezo ya Kusisimua—Je! Niijasirie?
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI— Lile Wazazi na Watoto Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Wazazi Waungaji-Mkono Shukrani ya kipekee sana kwa ule mfululizo “Wazazi Iweni Waungaji-Mkono!” (Agosti 8, 1994) Hivi majuzi, mwalimu mkuu wa shule ya binti yangu mdogo zaidi alizungumza pamoja na kikundi cha wazazi juu ya suala la uwasiliano mzuri wa mwalimu na mzazi. Nilimpelekea mwalimu mkuu gazeti hilo, naye akalisoma mara hiyo. Majuma mawili baadaye binti yangu aliniletea gazeti la shule la kila mwezi. Sehemu ya makala hiyo juu ya uwasiliano mzuri ilikuwa imepigwa chapa tena ili kwamba jumuiya yote inufaike kutokana na habari hiyo.

W. B., Marekani

Wolfini Nilifurahia ile makala “Ni Nyangumi? Ama Ni Dolfini?—La, Ni Wolfini!” (Februari 22, 1994), juu ya mvyauso nusu dolfini na nusu nyangumi. Mwishoni mwaita tokeo hili “kuona mara nyingine tena uwezo wa ajabu wa tofauti mbalimbali ambazo Mungu ameumba katika uumbaji wake.” Sikukubaliana na hili kwa sababu ujamiiano haungetokea katika mazingira yao ya kawaida.

K. G., Marekani

Hatukumaanisha kwamba ujamiiano kama huo ulikuwa wa kawaida au kwamba Mungu aliusababisha. Hata hivyo, mwanadamu hawezi kupewa sifa kwa kuwapo kwa kiumbe huyo mwenye kuvutia. Mivyauso huwapo kwa sababu ya “uwezo wa ajabu wa tofauti mbalimbali ambazo Mungu ameumba katika uumbaji wake.” Hivyo makala yetu ilimpa Mungu sifa anayostahili.—Mhariri.

Michezo ya Kusisimua Katika makala “Vijana Huuliza . . . Michezo ya Kusisimua—Je! Niijasirie?,” mlifanya vyema katika kuwaonya vijana juu ya hatari ziwezekanazo za urukaji banji. (Julai 8, 1994) Juma moja halikumalizika baada ya kuisoma, Shirika la Utangazaji la Uingereza likaripoti kwamba vijana wanne walipata haribiko baya sana la jicho kwa sababu ya kuruka banji. Asanteni kwa gazeti lenu zuri ajabu.

D. F., Uingereza

Ile makala juu ya michezo iwezayo kuleta kifo iliniwacha nikiwa macho kabisa! Wakati mmoja nilipanda jabali lenye mwinamo mkali na kujikuta nikishindwa kwenda mbele wala nyuma. Hadi leo hii mimi hutetemeka jinsi ilivyobaki kidogo nife. Ungekuwa upotezo wa kipumbavu kama nini wa uhai wangu!

L. T., Marekani

Nilithamini sana makala hiyo. Mahali ninapoishi, watoto hushiriki katika mingi ya michezo hii yenye kusisimua. Wao wanajaribu sikuzote kunifanya niicheze pamoja nao. Ingawa hivyo, katika habari, mara nyingi mimi huona ripoti za watu wafao au waumizwao vibaya sana kutokana na michezo iyo hiyo isemekanayo kuwa yenye kufurahisha wanayoniambia kuihusu. Baada ya kusoma makala hiyo, nilitambua kwamba ingekuwa kukosa hekima kwa upande wangu kuhatarisha uhai wangu, ambao Yehova Mungu alinipa, kwa ajili ya msisimko wa muda tu.

J. S., Marekani

UKIMWI Kwa zaidi ya miaka mitatu nilitumikia nikiwa mweneza-evanjeli wa wakati wote. Hata hivyo, kwa sasa siwezi. Nina UKIMWI. Asanteni kwa kushughulikia jambo hili gumu kwa uwazi katika makala “Kusaidia Wale Walio na UKIMWI.” (Machi 22, 1994) Naweza kuona kwamba kwa unyofu mnahangaikia masilahi ya kila mtu. Hata hivyo, yaonekana kwamba wengi wamekosa kufahamu sehemu za makala hiyo zilizotia moyo kuwa na huruma kwa ajili ya wenye kuteseka na wamekazia akili kwenye “tahadhari zifaazo” zilizotajwa. Ni kana kwamba makala hiyo ilitoa leseni kwa wengine kuwa baridi. Nashindwa kile kitakachotokea wakati nitakuwa katika hali mbaya zaidi, na kuhitaji kwelikweli upendo na utegemezo wa ndugu zangu. Je, baadhi yao watakataa kunitembelea kwa sababu wanaogopa kuambukizwa na virusi hiyo?

M. N., Marekani

Twathamini maelezo haya ya moyo mweupe. Haikuwa nia yetu kuvunja moyo upaji wa utegemezo kwa wagonjwa wa UKIMWI. Kwa hakika, tulitaarifu hivi: “Kwa kutegemea maoni yakubaliwayo sasa, kukutana katika hekaheka za kawaida hakupitishi UKIMWI. . . . Mtu asiwe akiogopa-ogopa kuwa karibu na watu wenye UKIMWI.” Tahadhari zilizodokezwa zaweza kusaidia wengine wahisi kiwango fulani cha ulinzi wanaposhughulika kwa huruma pamoja na wagonjwa wa UKIMWI.—Mhariri.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki