Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/22 kur. 10-12
  • Mahali Ambapo UKIMWI Umeenea Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahali Ambapo UKIMWI Umeenea Sana
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wale Walioumizwa Vibaya Zaidi
  • “Lile Tatizo Kuu la Kiafya la Wakati Wetu”
  • Lile Pigo la Kijamii la UKIMWI
  • Jambo Linalofanywa
  • Suluhisho
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
  • UKIMWI—Matokeo Yenye Msiba Mkubwa kwa Watoto
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI— Lile Wazazi na Watoto Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/22 kur. 10-12

Mahali Ambapo UKIMWI Umeenea Sana

KWA miaka iliyopungua 15, UKIMWI umeeneza maafa na huzuni katika kila kontinenti duniani. Kwa miaka michache tu, kombora hili la kibiolojia limezagaa kwa viwango vyenye kuenea mno. WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni) limekadiria kwamba ulimwenguni pote watu 5,000 wanaambukizwa kila siku. Hiyo ni sawa na watu watatu kila dakika! Nchi zilizoathiriwa zaidi zimekuwa zile maskini zaidi, zile eti zinazoitwa ulimwengu unaositawi. WHO lilibashiri kwamba nchi hizi, kufikia mwaka 2000, zitafanyiza asilimia 90 ya maambukizo yote ya HIV na hatimaye asilimia 90 ya visa vyote vya UKIMWI.

Wale Walioumizwa Vibaya Zaidi

Rose alikuwa na umri wa miaka 27 na aliyeolewa akiwa na watoto watatu wakati mume wake alipokuwa mgonjwa ghafula. Alikufa miezi kadhaa baadaye. Kisababishi cha kifo cha mumeye hakikujulikana hasa wakati huo. Madaktari walichungua ugonjwa wa kifua kikuu. Watu wa ukoo walisema alikuwa amelogwa. Watu wa ukoo upande wa mume walianza kunyakua mali ya Rose. Wakwe zake walichukua watoto wake kwa nguvu wakati alipokuwa hayupo nyumbani. Rose alilazimika kurudi kijijini alikotoka. Miaka miwili baadaye alipatwa na mashambulio ya kutapika na kuhara. Wakati huo ndipo aling’amua kwamba mume wake alikuwa na UKIMWI na kwamba pia yeye alikuwa ameambukizwa. Rose alikufa miaka mitatu baadaye, akiwa mwenye umri wa miaka 32.

Hadithi zenye kuhuzunisha kama hii sasa ni za kawaida. Katika maeneo mengine familia nzima na hata vijiji vimefyekwa kabisa.

“Lile Tatizo Kuu la Kiafya la Wakati Wetu”

Serikali katika nchi zinazositawi hazina uwezo zijaribupo kukabiliana na tatizo hili. Kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali za kifedha na kuwapo kwa mambo mengine ya kutangulizwa ya dharura na ghali, UKIMWI unathibitika kuwa kifyekaji kiletacho maangamizi makuu. Mshuko wa ulimwenguni pote, upungufu wa chakula, misiba ya asili, vita, desturi za kitamaduni, na ushirikina mbalimbali hufanyiza tu hilo tatizo kuwa kubwa. Kuandaa utunzi maalumu unaohitaji vifaa na madawa kwa ajili ya maambukizo yaliyo ya kawaida ya wagonjwa wa UKIMWI ni ghali. Mengi ya mahospitali makubwa sasa yamesongamana, yako katika hali mbaya, na bila wafanyakazi wa kutosha. Wagonjwa wengi walio na UKIMWI sasa wanapelekwa nyumbani wafe wakiwa huko ili kufanyiza nafasi kwa ajili ya idadi iliyozidi kukua ya wagonjwa wengine wenye uhitaji. Kuhusiana na UKIMWI limekuwa ongezeko lenye kutisha katika maambukizo ya ziada kama vile kifua kikuu. Nchi nyingine zimeripoti kwamba vifo vya kifua kikuu vimerudufika katika miaka mitatu iliyopita, na nyakati nyingine, wengi kufikia asilimia 80 ya wagonjwa walio hospitalini wenye UKIMWI wana kifua kikuu.

Lile Pigo la Kijamii la UKIMWI

Ule mweneo wa UKIMWI si kwamba tu unapiga mfumo wa utunzi wa afya bali pia sekta zote za kiuchumi na kijamii. Wengi kufikia asilimia 80 ya wale walioambukizwa wako katikati ya umri wa miaka 16 na 40, kile kikundi cha umri chenye kutokeza mazao zaidi katika jamii. Wengi wa wachuma-mishahara wa familia wako katika umri huu. Familia nyingi zawategemea, lakini wanapokuwa wagonjwa na hatimaye kufa, walio wachanga zaidi na wazee-wazee waachwa bila utegemezo. Katika jamii yoyote ya Kiafrika, wazazi wa mtoto wanapokufa, kidesturi mtoto anahodhiwa na kuchukuliwa kwa familia ya watu wa ukoo wa karibu. Hata hivyo, leo wazazi wanapokufa, babu na nyanya ama watu wa ukoo walio hai mara nyingi ni wazee sana ama tayari wana mzigo mzito wa kujaribu kuandaa mahitaji yanayohitajiwa ya watoto wao wenyewe. Hali hii imeongoza kwa masaibu ya mayatima na ongezeko katika idadi ya watoto wa mitaani. WHO latabiri kwamba katika bara la Afrika lililo chini ya Sahara peke yake, zaidi ya watoto milioni 10 wataachwa wakiwa mayatima kufikia mwisho wa karne hii.

Wanawake wanapata hiyo balaa ya UKIMWI kuwa yenye mkazo na kuchosha pia. Kwa msingi ni wanawake wanaohitajiwa kuandaa utunzi wa uuguzi wa mchana na usiku kwa wagonjwa na wanaokufa—hili ni ziada ya kazi nyingine zote za nyumbani wahitajizo kufanya.

Jambo Linalofanywa

Mapema katika miaka ya 1980, maofisa wa serikali wengi, wakipuuza balaa inayohusianishwa na UKIMWI na bila habari juu ya uharaka ambao ingeenea kwao, walikuwa baridi na wenye kuridhika na hali. Hata hivyo, katika 1986 serikali ya Uganda ilitangaza vita dhidi ya UKIMWI. Kwa miaka tisa iliyopita, Uganda imekuja kusifika kwa kuwa na “mbinu za kudhibiti UKIMWI zilizo za kisasa zaidi.”

Leo, kuna mashirika zaidi ya 600 ya kitaifa na kimataifa na mashirika katika Uganda ambayo yanashughulikia kujaribu kudhibiti ueneaji wa UKIMWI. Mashirika haya na ubinadamu yameanzisha mfumo wa vitovu vya kuelimisha kuhusu UKIMWI kotekote nchini. Uelewevu wa umma kuhusu balaa ya UKIMWI unaletwa kwenye uangalifu wa watu kupitia drama mbalimbali, dansi, nyimbo, programu za redio na televisheni, magazeti ya habari, na simu. Pamoja na utunzi wa nyumbani na msaada wa kimwili, mashauri huandaliwa kwa wale wenye UKIMWI pamoja na wajane na mayatima.

Miongoni mwa Mashahidi wa Yehova, utunzi kwa mayatima na wajane huonekana kuwa sehemu ya ibada ya Kikristo. (Yakobo 1:27; 2:15-17; 1 Yohana 3:17, 18) Kutaniko halinyakui daraka la washiriki wa familia la kutunza walio wao wenyewe. Lakini ikiwa hakuna washiriki wa karibu wa familia, ama ikiwa mayatima na wajane hawawezi kujiandalia kifedha wenyewe, kwa njia ya upendo kutaniko huwasaidia.

Kwa kielelezo, Joyce alikuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova aliyeishi katika Kampala, mji mkuu wa Uganda. Yeye alikuwa jeruhi wa UKIMWI naye alikufa katika Agosti 1993. Kabla ya kufa aliandika simulizi linalofuata: “Nilikua nikiwa Mprotestanti na baadaye niliolewa na Mkatoliki. Hata hivyo, ningeweza kuona wengi katika kanisa langu wakitenda kwa upotovu wa kiadili, kwa hiyo nikaacha kwenda kanisani. Dada yangu mkubwa zaidi alikuwa akijifunza Biblia pamoja na Mashahidi wa Yehova, na aliponitembelea, alinieleza kuhusu mambo yale aliyokuwa akijifunza kutoka kwa Biblia.

“Mume wangu alipinga sana kujifunza kwangu Biblia. Hata wazazi wangu walianza kunipinga, hasa baba yangu. Upinzani huu uliendelea kwa miaka miwili, lakini hawakunivunja moyo, kwani nilikuwa nimesadikishwa kwamba nilikuwa nikijifunza kweli. Nilipomwambia mume wangu kwamba nilitaka kubatizwa, alighadhabika sana. Alinitenda vibaya kimwili na kuniambia niondoke nyumbani. Kwa hiyo niliondoka na kuishi nikiwa peke yangu katika chumba kidogo cha kukodisha.

“Wakati fulani baadaye mume wangu aliniomba nirudi. Haikuwa muda mrefu baada ya mimi kurudi kwamba alianza kudhoofika na kuwa mgonjwa. Nilishangaa, kwani alikuwa sikuzote na afya nzuri. Hatimaye tulikuja kufahamu kwamba alikuwa na UKIMWI. Alikufa katika 1987. Kwa wakati huu nilikuwa painia wa kawaida [mweneza-evanjeli wa wakati wote], na hata ingawa sasa nilikuwa mjane mwenye watoto watano, niliendelea katika utumishi wa upainia.

“Miaka minne baadaye, katika 1991, niling’amua kwamba nilipata UKIMWI kutokana na mume wangu. Nilianza kudhoofika kimwili na kuugua harara ya ngozi, upotezo wa haraka wa uzani, na mashambulio ya daima ya homa. Bado niliendelea kupainia nami nilikuwa nikiongoza mafunzo ya Biblia 20, lakini kadiri nguvu zangu zilivyozidi kudhoofika, ilinibidi kuyapunguza hadi 16. Saba wa wanafunzi hawa hatimaye walibatizwa.

“Sikuhisi kuachwa peke yangu ama kushuka moyo kamwe, kwa sababu kutaniko lilikuwa utegemezo halisi kwangu. Hatimaye, ilinibidi kukosa baadhi ya mikutano kwa sababu ya kudhoofika kimwili. Akina ndugu waliirekodi kwa niaba yangu kwenye kaseti, nami nililishwa kiroho kwa kuendelea. Wazee wa kutaniko walitengeneza orodha ili kwamba dada zangu wa kiroho wangeweza kupokezana zamu katika kutunza mahitaji yangu na hata kukaa nami usiku kucha. Hata hivyo jambo moja lilinifadhaisha—watoto wangu. ‘Ni nini kitawapata nitakapoondoka?’ Nilijiuliza.

“Katika Afrika mali ya mtu aliyekufa mara nyingi hutwaliwa na watu wa ukoo, kwa hiyo nilisali daima kwa Yehova kuhusu jambo hili. Niliamua kuuza nyumba yangu na kujenga nyumba ndogo za kukodisha ili kwamba sikuzote watoto wangu wangekuwa na mahali pa kuishi na kiasi fulani cha mapato ya kawaida. Akina ndugu katika kutaniko waliuza nyumba kwa niaba yangu na wakaweza kununua ploti nyingine ya ardhi, nao wakajenga hizo nyumba kwa niaba yangu. Niliishi katika moja yazo nami nilihisi amani ya akili kujua kwamba watoto wangu wangetunzwa.

“Watu wangu wa ukoo walikuwa na ghadhabu sana kwamba niliuza nyumba, nao wakaanzisha pambano la kisheria dhidi yangu. Kwa mara nyingine tena, akina ndugu walinisaidia na wakashughulikia jambo hilo kwa niaba yangu. Tulishinda hiyo kesi ya kisheria. Ingawa sasa najihisi nikiwa mdhaifu zaidi, tengenezo la Yehova lenye upendo na tumaini la Ufalme zanipa ari ya kuendelea. Kwa sababu ya hali yangu sasa nimelazwa hospitalini. Bado ningali na dada zangu wa kiroho wakitunza mahitaji yangu mchana na usiku, kwani hospitali haiwezi kuandaa chakula cha kutosha na matandiko.”

Baada ya kukaa hospitalini miezi sita, Joyce alipelekwa nyumbani. Siku mbili baadaye alikufa. Watoto wake watano sasa wanatunzwa na dada mmoja painia katika kutaniko ambaye pia ana watoto watatu wake mwenyewe.

Suluhisho

Katika Uganda, mahali ambapo tayari UKIMWI umeenea mno, Rais Yoweri Kaguta Museveni alitaarifu hivi: “Ninaamini kwamba itikio lililo bora zaidi kwa hatari itokezwayo na UKIMWI na maradhi mengine yanayopitishwa kingono ni kuwa wenye heshima, staha, na daraka kuhusu tunalowiwa na kila mtu kwa jirani yake awe wa kiume au wa kike.” Kwa ufupi, kuna uhitaji wa kurudia adili za mke au mume mmoja mnamo mpango wa ndoa. Kila mtu akubali kwamba hii ndiyo njia pekee ya kuwa salama na njia pekee ambayo UKIMWI waweza kudhibitiwa. Hata hivyo, ni wachache huamini kwamba kiwango kama hicho cha maadili chafikilika.

Mashahidi wa Yehova wako miongoni mwa wale ambao si kwamba wanaamini adili kama hiyo yawezekana tu bali wanaitumia. Na zaidi, wao huamini, kama Joyce alivyoamini, katika ahadi ya Mungu ya mbingu na nchi mpya ambazo katika hizo uadilifu utakaa. (2 Petro 3:13) Katika ulimwengu uliosafishwa uovu wote, wakati huo Yehova Mungu atatimiza ahadi iliyorekodiwa kwenye Ufunuo 21:4: “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”

[Picha katika ukurasa wa 10]

Baba achukua mwanaye aliyekufa kutokana na UKIMWI ili azikwe

[Hisani]

WHO/E. Hooper

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki