Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 8/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Hali ya Uharaka Tufeni”
  • “Dawa Iliyo Mbaya Kuliko Zote”
  • Jeuri Zaidi Dhidi ya Wanawake
  • Mioshi Yenye Sumu
  • Je, Gari la Magurudumu Manne Yenye Nguvu Ni Salama?
  • Vichezeo Vinavyochochea Jeuri
  • Kidude Kipya Chaonya Kuhusu Hatari ya Maradhi ya Moyo
  • “Kula Matunda na Mboga Zako”
  • Ming’atuko Kanisani
  • Maisha Katika Jiji Kubwa
  • UKIMWI—Je! Nimo Hatarini?
    Amkeni!—1993
  • UKIMWI—Matokeo Yenye Msiba Mkubwa kwa Watoto
    Amkeni!—1992
  • UKIMWI— Shida kwa Matineja
    Amkeni!—1992
  • Kusaidia Wale Walio na UKIMWI
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 8/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

“Hali ya Uharaka Tufeni”

Kwenye Kongamano juu ya UKIMWI lililofanywa katika Paris kwenye sherehe ya saba ya kila mwaka ya Siku ya UKIMWI Ulimwenguni, katibu-mkuu wa UM, Boutros Boutros-Ghali, aliwaomba viongozi wa serikali na mawaziri wa afya kutoka nchi 42 na kontinenti 5 “kutangaza hali ya uharaka tufeni” kutokana na ukuzi wenye kutisha wa mweneo wa UKIMWI. Kati ya Julai 1993 na Julai 1994, licha ya jitihada za ulimwenguni pote za kudhibiti mweneo wa UKIMWI, jumla ya idadi ya visa vya UKIMWI ulimwenguni iliongezeka kwa asilimia 60, ikifikia yapata milioni nne. Katika ripoti yenye kuhuzunisha, Shirika la Afya Ulimwenguni lilionya kwamba kwa kiwango cha sasa cha ukuzi, mweneo wa UKIMWI kwa kweli “watisha wakati ujao wa jamii nzima-nzima,” na kutabiri kwamba mapema kufikia mwaka 2000, kati ya watu milioni 30 na milioni 40 watakuwa wameambukizwa na virusi yenye kufisha ya HIV isababishayo UKIMWI.

“Dawa Iliyo Mbaya Kuliko Zote”

Kichwa kikuu kimoja cha hivi majuzi katika gazeti la habari Jornal do Brasil la Brazili kilifafanua sigareti kuwa “dawa iliyo mbaya kuliko zote.” Kulingana na mkurugenzi wa National Cancer Institute ya Brazili, Dakt. Marcos Moraes, biashara ya tumbaku inalenga vijana. Yeye alieleza kwamba “kadiri kijana anapoanza kuvuta sigareti mapema, ndivyo atakavyoendelea zaidi kuvuta sigareti. Na kadiri anavyojihatarisha kwa kuvuta sigareti, ndivyo alivyo na uwezo mkubwa wa kupata madhara ya kiafya.” Dakt. Moraes alionelea kwamba miongoni mwa wavutaji-sigareti milioni 30 katika Brazili, “milioni 2.4 ni watoto na wabalehe.” Yeye aongezea kwamba “sigareti huua [watu] zaidi kuliko UKIMWI, kokeni, heroini, alkoholi, mioto, aksidenti za gari na ujiuaji vikijumlishwa.”

Jeuri Zaidi Dhidi ya Wanawake

“Mashambulizi juu ya wanawake na waume zao ama wenzi wa kiume ndiyo aina iliyo ya kawaida zaidi ya jeuri ulimwenguni,” lasema gazeti la habari The Australian katika makala fulani kuhusu ripoti ya UM. Hiyo makala yaeleza kwamba “wanawake wengi kufikia robo ulimwenguni wanatendwa kwa ujeuri.” Katika nchi nyinginezo, kama vile Chile, Jamhuri ya Korea, Pakistan, Papua New Guinea, na Thailand, kiwango hiki ni cha juu hata zaidi. Katika nchi moja, karibu asilimia 80 ya idadi ya wanawake wanatendwa vibaya, likataarifu gazeti la habari jingine, The Sydney Morning Herald, katika kuzungumzia ripoti hiyohiyo ya UM. Wengi wa majeruhi pia huvumilia kutendwa vibaya kihisia-moyo kwenye kuendelea. Jeuri ya nyumbani ni tatizo gumu sana kusuluhishwa kwa sababu sikuzote hutukia faraghani. Mara nyingi marafiki, majirani, na watu wa ukoo hawapendi kuiripoti.

Mioshi Yenye Sumu

Maofisa wa afya katika Marekani wanahangaikia idadi ya watu wanaosumishwa na kaboni monoksaidi (CO). MMWR (Morbidity and Mortality Weekly Report) yataarifu kwamba “taifa zima, vifo karibu 590 hutukia kila mwaka kutokana na kusumishwa kusikokusudiwa kwa CO.” Hili halitii ndani vile visa vingi visivyotokeza maafa vya kusumishwa na CO. Kwa sababu hiyo gesi yenye kufisha haina rangi, mnuko, na ladha, ni vigumu kuitambulisha. Hiyo gesi hulemaza uwezo wa damu kuchukua oksijeni kwenye chembe, ikisababisha kuumwa na kichwa, kuchafuka moyo, matatizo katika mfumo wa hisi, koma, na kifo. Kulingana na MMWR, “mrundamano wa CO unaweza kuhusianishwa na utaratibu wowote wa uchomaji unaotukia ndani ya nyumba (k.v., mfumo wa kupasha nyumba joto, kupika, ama gari iliyowashwa injini ama kifaa kinachotenda kikitumia petroli)—hasa wakati vipitisha hewa havitoshi.”

Je, Gari la Magurudumu Manne Yenye Nguvu Ni Salama?

Wengi huamini kwamba sikuzote ni salama kuendesha gari la magurudumu manne yenye nguvu, hasa katika theluji na barafu. Hata hivyo, “kuhusu kusimamisha, magari ya magurudumu manne yenye nguvu hayana uwezo kupita yale magari yenye magurudumu mawili yenye nguvu,” laripoti The Wall Street Journal. Kulingana na maofisa wa bima, baadhi ya miundo maarufu zaidi (ya magari hayo) kwa kawaida husababisha “madhara yaliyopita kiasi na huwa na madai ya bima kwa sababu ya kugongana na magari mengine.” Kwa wazi, madereva wengi hujiamini kupita kiasi na hujihatarisha isivyofaa wanapoendesha magari ya magurudumu manne yenye nguvu. Marc Schoen, mtafiti katika Kitovu cha Kitiba cha UCLA katika Los Angeles alionelea kwamba “kupitia filamu na televisheni, watu wamekuja kuhusianisha magari ya magurudumu manne yenye nguvu na hali ya kujitegemea na uhuru.” Hali hii ya kuwa na uwezo na kutoshindika yaweza kuathiri uamuzi timamu, ambao hatimaye ndio sera bora zaidi kwa uendeshaji salama.

Vichezeo Vinavyochochea Jeuri

Kipindi fulani cha televisheni kuhusu matineja ambao hujigeuza, kana kwamba kwa kiinimacho, kuwa mashujaa wa mbinu za kivita za mikono kimekuwa maarufu sana miongoni mwa watoto katika Marekani. Wahusika katika televisheni huitwa Mighty Morphin Power Rangers. Wenye mamlaka za shule wanahangaikia ile ionekanayo kuwa tabia ya kupita kiasi inayodhihirishwa na watoto wadogo wakiigiza matendo ya jeuri ya Power Rangers. The Wall Street Journal laripoti kwamba katika uchunguzi wa majuzi, asilimia 96 “ya walimu waliohojiwa wasema wameshuhudia matendo ya ukatili yachochewayo na Morphin.” Katika visa vingine watoto ni wachanga sana kufikia miaka mitatu. “Watoto wadogo wanaweza kugeuka ghafula kuwa wanamasumbwi wakatili na wenye jeuri sana,” lasema Journal. Umaarufu wa hicho kipindi waonyeshwa katika mauzo yatazamiwayo ya dola milioni 300 ya vichezeo vya Power Ranger yatakayofanywa kwa mwaka mmoja.

Kidude Kipya Chaonya Kuhusu Hatari ya Maradhi ya Moyo

Wanasayansi katika Victoria, Australia, wamebuni kidude kipya ambacho kikiwekwa katika ngozi juu ya ateri kuu shingoni hutabiri hatari ya maradhi ya moyo. Bila upasuaji wa ndani, hicho hupima mwendo wa damu na mabadiliko katika msongo wa damu baada ya kila mpigo wa moyo. Kisha kompyuta yaweza kutumiwa ili kupiga hesabu ya “unyumbufu wa mfumo mzima wa moyo wa mgonjwa,” yasema ripoti katika gazeti la habari The Sydney Morning Herald. Hicho kifaa chaahidi kuwa sahihi zaidi kuliko mbinu za kawaida za kuchanganua hatari ya mtu kupatwa na maradhi ya moyo. Ingawa kiwango cha juu cha shahamu na msongo wa damu wa juu ni vionyeshi vyenye nguvu vya hatari, “watu wengi katika tabaka hizi hawajapata kamwe kuwa na mshiko wa moyo,” yasema hiyo ripoti, ikiongezea kwamba “kwa kutumia jaribio hilo, [wao] wangeponea kumeza madawa ghali ya kuteremsha kiwango cha shahamu ama kufuatia lishe yenye mipaka ambayo hawahitaji.”

“Kula Matunda na Mboga Zako”

Kwa miongo mingi wanasayansi wamependekeza kumeza karotini kama vibadala vya chakula. Beta-karotini ni karotini inayojulikana sana, na imehusianishwa na kuzuia maradhi ya moyo, maradhi ya ghafula, na kansa za aina fulani. Hata hivyo, utafiti mpya washuku manufaa za vibadala vya beta-karotini. Kulingana na The New York Times, mwanasayansi wa chakula Dakt. Paul LaChance “alitahadharisha dhidi ya kumeza vibadala vya karotini moja-moja.” Alieleza kwamba “katika vyakula vya asili sisi hupata mchanganyiko wa karotini, na bado hatujapata kujua jinsi ilivyo muhimu kupata mchanganyiko huu.” Mtafiti mwingine, Dakt. Regina Ziegler, alipendekeza kwamba “mpaka tutambulishe kuwapo kwa tabia za ukingaji katika matunda na mboga, hatuwezi kuviweka ndani ya kidonge cha kumeza.” Times laonelea kwamba “wastadi wengi wamerudia shauri lililotolewa kidesturi na mama: ‘Kula matunda na mboga zako.’”

Ming’atuko Kanisani

Kulingana na gazeti la Christ in der Gegenwart la Katoliki, watu milioni 28 katika Ujerumani, ama theluthi moja ya idadi ya watu, ni Wakatoliki. Katika miaka ya 1992 na 1993, jumla ya watu wapatao 350,000 iling’atuka kutoka Kanisa Katoliki. Askofu Karl Lehmann, mwenyekiti wa Kongamano la Maaskofu wa Ujerumani, ana wasiwasi kwamba kodi mpya ya serikali, itakayoanzishwa katika 1995, itatokeza ming’atuko itakayoongezeka haraka zaidi, laripoti Süddeutsche Zeitung. Washiriki wa kanisa katika Ujerumani wanahitajiwa kulipa kodi ya kanisa. Basi, yaonekana kwamba Wakatoliki wengine watajaribu kuepuka kodi mpya ya serikali kwa kung’atuka tu kutoka kanisani.

Maisha Katika Jiji Kubwa

Ingawa London, Uingereza, ni jiji lililo kubwa kupita yote katika Ulaya, kulingana na gazeti la habari The Independent, wakazi walo milioni saba kwa ujumla hawafurahi kuishi pale. Kati ya wakazi wa London waliohojiwa, 6 kati ya 7 waamini kwamba maisha katika jiji kuu yameharibika kwa miaka mitano iliyopita, uchafuzi na msongamano wa magari yakiwa miongoni mwa mahangaiko yao makuu. Walipoulizwa ni watu gani ambao wao hutumaini, asilimia 64 walitaja madaktari, polisi na walimu wakitumainiwa kidogo sana. Asilimia 2 walihisi wangeweza kutumaini wafanyabiashara wanaofanya kazi katika eneo la kibiashara la London. Yapata asilimia 60 waliamini kwamba eneo hili lilikuwa “limejaa watu ambao hujitajirisha kwa hasara ya wengine bila kufanyiza utajiri halisi.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki