Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/22 kur. 17-18
  • Kwa Nini Kujenga kwa Mbao?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Kujenga kwa Mbao?
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jengo la Mbao Lililo la Kale Kupita Yote
  • Nyumba za Kijapani
  • Umaridadi wa Mbao
  • Zawadi ya Mbao
  • Je! Sanamu Zinaweza Kukusaidia Umtumikie Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Kuchunguza Umaridadi wa Miaka Mingi wa
    Amkeni!—1998
  • Uchongaji wa Vinyago—Sanaa ya Kiafrika ya Kale
    Amkeni!—1997
  • Useremala wa Kipekee wa Japani
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 10/22 kur. 17-18

Kwa Nini Kujenga kwa Mbao?

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA JAPANI

ZIKIMETAMETA kama maganda ya kifedha ya samaki katika jua tulivu la kaskazini-magharibi mwa Urusi ni kuba 22 zenye umbo la kitunguu-mviringo juu ya kanisa la mbao. Kuziangalia kwa karibu zaidi kwafunua kwamba hizo kuba zimefunikwa na maelfu ya vigae vya mbao, sasa vikiwa vimechakaa umri. Kwa karibu miaka mia tatu, jengo hili la mbao kwenye kisiwa katika Ziwa Onega limestahimili vipupwe vikali vya hiyo nchi. Kwa unyamavu lathibitisha kwa kutazamisha ule udumifu wa mbao.

Majengo mengine hutoa uthibitisho wenye nguvu hata zaidi. Yakiwa yametapakaa kotekote katika Ulaya kaskazini ni majengo ya mbao ambayo yamekuwa yakitumika kwa muda mrefu zaidi. Mathalani, kazi ya ufundi ya watu wa Norway waliojenga sana kwa mbao yapata karne ya 12 bado nyumba zao zaweza kuonekana katika sehemu za mashambani. Kuvuka kwenda Uingereza, bado yakiwa yanajasiria hali ya hewa iliyo kali, ni majengo ya mbao karibu na mji wa Ongar, Essex, yaliyojengwa karibu mwaka wa 1013. Lakini lile linaloonekana kuwa babu ya yote ni hekalu la mbao katika Japani ambalo lina umri wa karne nyingi.

Jengo la Mbao Lililo la Kale Kupita Yote

Imewezekanaje kwa Hekalu hili la Horyuji la mbao kudumu kwa muda mrefu hivyo? Kwa msingi ni kwa sababu ya ujuzi mzuri wa mbao wa maseremala wa kwanza. Walijua ni mbao gani ya kuchagua na ni sehemu gani ya kutumia kwa kazi hususa. Wao walichagua hinoki (mteashuri wa Kijapani), ambao ulikuwa na ukuzi wa umri wa angalau miaka elfu kabla ya kukatwa.

Seremala mahiri Tsunekazu Nishioka, aliyekufa hivi majuzi, alitumia wakati mwingi wa maisha yake akifanya kazi katika kujenga upya hekalu hekalu. Yeye alidai kwamba misumari—iliyofanana na visu vya samurai, iliyotengenezwa kwa ufundi wa kufua na kuchoma kwa kurudia—imechangia pia sehemu muhimu katika udumifu wa hilo hekalu. Katika kazi hiyo ya kulijenga upya, misumari ya zamani ilitumiwa kwa sababu kama alivyosema, “misumari ya kisasa haidumu kwa miaka 20.”

Wengine huenda washuku kama kweli Hekalu la Horyuji lina umri wa miaka 1,300, kwani asilimia 35 yalo imebadilishwa katika karne hii. Hata hivyo, nyingi za nguzo kuu, mihimili kuu, na penu ni za mbao za kwanza. Nishioka alisema hivi: “Nafikiri hilo hekalu litadumu miaka mingine 1,000.”

Kukiwa na mbao za aina hii karibu nao, si ajabu kwamba Wajapani wa kale walipendezwa na mbao. Hata leo nyumba zao hudhihirisha kwamba upendezi huu ulipitishwa kwao.

Nyumba za Kijapani

Ndani ya nyumba, mbao hutumiwa sana, lakini hazipakwi rangi. Nguzo, milango, fanicha, na kadhalika, hufanyiwa uhitimisho ambao huacha nyuzi na rangi ya kiasili ikitamanisha. Mbao kwenye veranda huwa hazifanyiwi uhitimisho kabisa. Mbao ambayo haijahitimishwa huandaa kiunzi cha kiasili cha miti na visitu bustanini. Matokeo huwa ni upatano na utulivu wa kindani badala ya usisimukaji.

Wajapani wengi husema kwamba hii ndiyo aina ya nyumba ambayo wangetamani kuwa nayo. Hata hivyo, mbao za hali ya juu za kujenga nyumba kama hiyo sasa ni ghali mno kwa mfanyakazi wa kawaida. Hata hivyo, Wajapani hupenda kutumia mbao popote wawezapo kutumia kwa sababu historia imewafunza kwamba licha ya kuonekana vizuri, mbao hufaa mazingira yao, ambayo hutia ndani matetemeko ya dunia ya mara kwa mara, tufani, viangazi vyenye unyevu wenye joto, vipupwe vyenye baridi.

Mbao ni baraka kwa nchi zinazopatwa na tetemeko la dunia, kwani hizo hubeta na kuyumba bila tatizo wakati wa mkazo ilhali vifaa kama vile mawe vingeatuka. Mbao pia zina sifa yenye kutokeza ya kudumisha unyevu na kuhami joto. Licha ya mvua na unyevu katika Japani kutoka Juni hadi Agosti, nyumba haziozi. Mbao hubadilika na kuandaa kiasi cha starehe wakati huu kwa sababu zaweza kufyonza unyevu kutoka hewani na baadaye hukauka. Hata hivyo, mbao yavutia mtu wa kawaida kwa sababu tofauti sana.

Umaridadi wa Mbao

Ulimwenguni kote watu walio wengi huchagua mbao kwa sababu ya umbo layo. Albert Jackson na David Day katika kitabu chao Collins Good Wood Handbook waeleza: “Kwa sababu mbao ni bidhaa ya asili, kila ubao haulinganiki. Kila sehemu ya ubao iliyotolewa mtini, au hata kutoka kwa ubao ule ule, utakuwa tofauti. Huenda ikiwa na uthabiti au rangi ileile, lakini haina kigezo kilekile cha unyuzi. Ni unamna huu mwingi wa tabia, uthibitifu, rangi, wororo na hata harufu ambao huifanya mbao ivutie hivyo.”

Kwa nini unamna mwingi hivyo uonekane kwenye nyuzi za mbao? Ili kutaja sababu ya kwanza, ingawa miti fulani hukuza nyuzi zilizonyooka, mingine hufanyiza nyuzi zenye mafundo, ilhali mingine hutokeza nyuzi zenye kuwimbika ama kujipinda. Kisha, kadiri miti inavyokua mara hujipinda au hubadili upande wa ukuzi, hutoa matawi, na wadudu huingia na kutoka. Zote hizi hufanyiza vigezo vyenye kupendeza. Kwa kuongezea, kigezo huonekana tofauti kulingana na upande ambao mbao imekatwa kuuelekea. Mbao moja ya kahawia nyekundu hivi ambayo imekatwa ili kuwa na kigezo cha milia yenye kuvumika imeitwa katika nchi fulani mbao punda-milia na katika nyingine mbao simba-marara.

Kuongezea ule umaridadi wa mbao ni zile rangi za aina nyingi. Si mbao zote ambazo zina rangi ya kahawia. Mpingo wenye kiini cheusi hutoka India na Sri Lanka, kamuwudi yenye rangi ieneayo kutoka nyekundu hadi zambarau-nzito hutoka Afrika Magharibi, na mahogani nyekundu-nzito hutoka Amerika ya Kati na Kusini. Mbao nyangavu ya kimachungwa, ambayo inapowekwa kwa jua hubadilika kuwa kahawia yenye wekundu mzito yatoka Brazili. Mbao nyingine ni za kijani kibichi, na nyingine ni nyekundu. Alaska huandaa mwerezi wenye mbao ya manjano yenye kufifia, na mkuyu wa Ulaya umefifia hata zaidi. Mwishoni mwa hiyo tamasha ni mbao zilizofifia sana, zimefifia hivi kwamba hazina rangi.

Wenye kuvutia kwa watu wengi pia ni ule uturi wa mbao. Mbao moja yenye uturi ni mberoshi, ndiyo maseremala wa Sulemani walitumia kusakafisha hekalu. (1 Wafalme 6:15) Labda ule uturi wa mbao ya mberoshi ulipenya hewa na kuchangamana wakati mwingine na ule wa uvumba. (2 Mambo ya Nyakati 2:4) Mberoshi wasifika si kwa kuwa na uturi tu bali pia kwa kuwa mdumifu na kuweza kukinza uozaji.

Mengi, mengi zaidi yangeweza kusemwa katika kusifu mbao. Wema wayo ni mwingi mno hivi kwamba wengi huuliza ni lipi lingeweza kusemwa dhidi yayo.

Zawadi ya Mbao

Ni kweli, si mbao zote ziwezazo kukinza wadudu wasumbufu, wala si mbao zote hukinza uozaji au hudumu kwa mamia ya miaka. Hangaiko kuu la kujenga kwa mbao ni moto. Hata hivyo, katika joto lililopita kiasi mbao nzito huchomeka polepole, hupoteza uthibitifu wazo polepole, na huchukua muda mrefu kuanguka kuliko feleji. Hata hivyo, ni nyumba chache leo zenye mihimili na nguzo kubwa za mbao za muundo wa kale. Hivi kwamba mtu angeweza kutoroka nyumba inayochomeka kwa kasi iwezekanavyo.

Mbao si kifaa cha ujenzi hafifu. Badala yake, mbao ambayo imechaguliwa na kutengenezwa ifaavyo yaweza kufanyiza jengo lililojihami vizuri ambalo litaandaa mamia ya miaka ya utumiaji. Mamlaka fulani hudai kwamba haingeweza kamwe kuoza ikiwa tutaitunza ifaavyo. Viwavyo vyote, kwa hakika mbao ni mojapo kifaa cha ujenzi kilicho bora ambacho Muumba ametupatia.

[Picha katika ukurasa wa 17]

Kuba zenye umbo la kitunguu-mviringo juu ya kanisa la mbao kwenye kisiwa katika Ziwa Onegao

[Credit line]

Tass/Sovfoto

[Picha katika ukurasa wa 18]

Hekalu la Horyuji la mbao katika Japani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki