Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tume Hatari za Amani
  • Ugonjwa wa Akili Miongoni mwa Watoto
  • Kupuuza Taa za Trafiki
  • Jeuri ya Matineja
  • Kutangua Ubatizo wa Wafu
  • Mkazo Katika Hong Kong
  • Vifaa vya Kiumeme Vyashukiwa
  • Ile Ngano ya Kiunganishi Kinachokosekana
  • Pornografia ya Kompyuta Yapatikana kwa Watoto
  • Makasisi Wanaosumbuka
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
  • Majiji Makubwa ya Biashara
    Amkeni!—1994
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 11/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Tume Hatari za Amani

Kufikia sasa, zaidi ya watu elfu moja wameuawa wakijihusisha katika tume za Umoja wa Mataifa za kuhifadhi amani, laripoti gazeti la Ujerumani Frankfurter Allgemeine Zeitung. Idadi hii haitii ndani wale waliopoteza maisha zao wakati wa tume za mapambano za UM, kama vile katika Vita ya Ghuba. Kati ya vifo hivi 1,000, zaidi ya 200 vilitokea katika 1993 pekee. Kwa nini vingi hivyo? Gazeti hilo lilieleza kwamba Umoja wa Mataifa sasa unajihusisha katika aina tofauti ya vita. Ilhali katika wakati uliopita Umoja wa Mataifa uliingia kati na kusimamia kusuluhishwa kwa vita kati ya nchi mbalimbali, shirika hilo sasa lajihusisha katika “vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambavyo kwavyo mamlaka ya serikali huvunjika na hata vikundi vinavyojihusisha vitani hushindwa kulinda wafanyakazi wa UM.”

Ugonjwa wa Akili Miongoni mwa Watoto

Kulingana na The Sunday Times, katika shule za Uingereza, zaidi ya watoto 1,000 walio chini ya umri wa miaka 10 na 1,200 hivi walio kati ya miaka 10 na 14 wanatibiwa tatizo la kurukwa akili, mshuko-moyo mbaya sana, au matatizo ya kula; na kiasi cha ujiuaji kinapanda vilevile, kukiwa na watoto wachanga kufikia miaka sita wanaotisha kujiua. Wastadi fulani wa akili wanafikiri kwamba moja ya visababishi ni ukosefu wa mazungumzo ya maana baina ya watoto na wazazi wao. Wanaonelea kwamba watoto wengi huishi katika mazingira ya nyumbani ambamo televisheni hutawala. Kama tokeo, watoto hawawezi kuzungumza na kushiriki mahangaiko yao pamoja na wazazi wao. Mstadi mmoja alionelea kwamba ukosefu wa uwasiliano baina ya wazazi na watoto waweza kusababisha “mahangaiko yao kuongezeka na kutokeza mtoto asiye na furaha.”

Kupuuza Taa za Trafiki

Katika Argentina, kulingana na gazeti la habari la Buenos Aires Clarin, kulikuwa na aksidenti mbaya 7,700 za magari katika 1994. Aksidenti hizi ziliacha watu 13,505 wakiwa wameumia vibaya na 9,120 wakiwa wamekufa. Uchunguzi uliofanywa na shirika la serikali umefunua kwamba asilimia 90 ya aksidenti zote za magari husababishwa na dereva au mtu anayetembea kwa miguu kukiuka sheria za barabara. Aksidenti ambazo hutokea mara nyingi sana katika majiji ni migongano ya upande inayotokana na kupita taa nyekundu ya trafiki bila kusimama. Eduardo Bertotti, afisa wa serikali, alionelea kwamba ingawa katika nchi nyingine ni jambo lisilowazika kupuuza taa nyekundu za trafiki, katika Argentina “si tukio la mara kwa mara tu bali kuna wale ambao hata huona fahari katika kufanya hivyo.”

Jeuri ya Matineja

Kwa miaka mitatu mfululizo, Marekani imepata upungufu katika idadi ya uhalifu mbaya ulioripotiwa. Hata hivyo, idadi ya matineja waliohusika katika uhalifu inaongezeka, hasa miongoni mwa vijana wa kati ya umri wa miaka 14 na 17. Wastadi fulani wanatabiri kwamba uhalifu wenye jeuri utaongezeka kadiri idadi ya matineja inavyozidi kuongezeka. Mstadi mmoja, James Alan Fox, wa Chuo cha Sheria za Jinai kwenye Chuo Kikuu cha Northeastern katika Boston, alionelea kwamba “idadi ya vijana katika Marekani itaongezeka kwa kiwango kikubwa katika miaka michache ijayo, kukiwa na asilimia 23 ya matineja zaidi kufikia mwaka 2005,” laripoti The New York Times. Fox aonya kwamba “tusipotenda sasa, watoto wetu wakiwa wangali wachanga na wawezapo kufinyangwa, huenda damu nyingi ikamwagika kwa sababu ya jeuri ya matineja kufikia mwaka 2005.”

Kutangua Ubatizo wa Wafu

Hivi majuzi waokokaji wa Kiyahudi wa Teketezo la Umati walishtushwa kujua kwamba baadhi ya watu wao wa ukoo walikuwa wamebatizwa kuwa Wamormon muda mrefu baada ya vifo vyao. The New York Times liliripoti juu ya zoea hilo “ambalo kwalo wafu wanabatizwa kuwa Wamormon na washiriki wa kanisa walio hai ambao wanawawakilisha.” Wamormon walikuwa wamepata majina ya baadhi ya Wayahudi 380,000 ambao walikuwa wamekufa katika kambi za mateso au kwa upande mwingine walikuwa majeruhi wa lile Teketezo la Umati. Kisha, kwa kipindi fulani cha wakati, waliwabatiza katika sherehe ambazo kwazo washiriki wa kanisa walitumbukizwa majini wakiwa wawakilishi huku majina ya waliokufa yakisomwa. Mashirika fulani ya Kiyahudi yamepinga taratibu hii. Kama tokeo, viongozi wa Wamormon walikubali kufuta kutoka katika orodha ya Wamormon waliobatizwa, majina ya majeruhi wa Kiyahudi wa Teketezo la Umati ambao wamefanyiwa sherehe hizo.

Mkazo Katika Hong Kong

Uchunguzi wa majuzi ambao katika huo watu 5,000 kutoka nchi tofauti 16 walihojiwa ulifunua kwamba Hong Kong ndilo jiji lenye mkazo kuliko yote ulimwenguni, laripoti The Medical Post. Kwa wengi, mkazo unahusiana na kazi. Mtafiti Dakt. David Warburton, wa Chuo Kikuu cha Reading cha Uingereza, aonelea kwamba “yapata 70% ya wanaume wa Hong Kong na 64% [ya] wanawake walilalamika kuhusu mkazo kazini, wakilinganishwa na 54% ya watu ulimwenguni pote.” Asilimia 41 hivi ya waliohojiwa kutoka Hong Kong walihisi kwamba kazi zao zilikuwa zenye kuchosha kwa kulinganishwa na asilimia 14 katika nchi nyinginezo. Post laongeza kwamba “mmoja kati ya watu watano katika Hong Kong (wakilinganishwa na wasiozidi mmoja kati ya 10 ulimwenguni pote) walisema kutompenda mkubwa wao kulikuwa sababu kuu ya mkazo kazini.”

Vifaa vya Kiumeme Vyashukiwa

Kulingana na FDA Consumer, gazeti la shirika la Usimamizi wa Chakula na Dawa la Marekani, vifaa vya kitiba vyaweza kukosa kufanya kazi vizuri vinapotatanishwa na sumaku-umeme, kama ile itokayo katika mfumo wa simu unaotumia mawimbi ya redio ulio karibu. “Hospitali fulani za Ulaya tayari zimepiga marufuku mifumo ya simu inayotumia mawimbi ya redio katika majengo yao, na FDA imetia moyo hospitali katika Marekani kuchukua hatua iyo hiyo ikihitajiwa,” lasema hilo gazeti. Athari za sumaku-umeme zinashukiwa katika aksidenti kadhaa ambazo kwazo vifaa vya kuokoa uhai kama vile vinavyochochea mpigo wa moyo na vile vinavyochunguza hali ya kushindwa kupumua vimekosa kufanya kazi vizuri. FDA Consumer laonya hivi: “Wagonjwa na madaktari ambao hutumia kwa ukawaida vifaa vya kitiba vinavyoweza kuathiriwa haraka wanapaswa kutambua tatizo hilo na kufikiria kuweka mbali na vifaa vyao mifumo ya simu inayotumia mawimbi ya redio.” Athari za sumaku-umeme zaweza pia kusababishwa na miunganisho ya kompyuta isiyo na waya, viashirio vya vijiwimbi, transmita za redio na televisheni, viliabipu, na vifaa vingine vya kiumeme. Watafiti wanachunguza njia za kupunguza tisho hilo.

Ile Ngano ya Kiunganishi Kinachokosekana

Wanamageuzi wametafuta kwa muda mrefu uthibitisho wa vitu vya kale ili kudhibitisha ile dhana ya kwamba mwanadamu alitokana na sokwe. Hata hivyo, gazeti la habari la Paris Le Monde lasema kwamba “dhana kuhusu asili ya mwanadamu zimetikiswa” na ugunduzi katika Ethiopia wa mfuatano wa mifupa 90 inayowakilisha kile ambacho wachimbuzi wa vitu vya kale wanaamini kuwa mabaki ya kiunzi cha umbo linalofanana na mtu mzima. Kulingana na wachimbuzi wa vitu vya kale tatizo ni kwamba vitu vya kale vilivyopatikana karibuni havipatani na dhana zozote ambazo zajaribu kuonyesha mlingano kati ya binadamu na sokwe. Badala ya hivyo, vitu vya kale vimetokeza maswali zaidi kuliko kuyajibu. Watafiti fulani wamefikia mkataa kwamba kile kiitwacho eti kiunganishi kinachokosekana kati ya mtu na sokwe huenda kisiwe “chochote ila ngano,” lasema Le Monde.

Pornografia ya Kompyuta Yapatikana kwa Watoto

Huku shule za Australia zikiunganishwa kwenye mfumo wa duniani pote wa habari wa Internet, wanaunganishwa pia kwa hali zinazotokeza hatari za maadili. Kulingana na gazeti la habari la The Sydney Morning Herald, wanaweza kutazama “picha za pornografia za watoto walio uchi, kujiingiza kupita kiasi katika ngono, sehemu za vidio zilizorekodiwa kutoka kwenye miunganisho ya madanguro, ‘haki zinazohakikishiwa watu’ kwa watu wanaotaka kufanya ngono na wanyama—na habari ya jinsi ya kujiunga na uwasiliano wa kompyuta wa ‘kuzungumza na kupiga punyeto.’” Makala hiyo yaongeza hivi: “Herufi zinazohitajiwa ili kuruhusiwa kutumia mfumo wa kompyuta au ithibati ya umri hayakuhitajiwa—ni muunganisho wa moja kwa moja.” Wataalamu wanasema kwamba haiwezekani kuchuja mfumo huo “kwa sababu mfanyizo wao ulibuniwa . . . na Idara ya Ulinzi ya Marekani ili kuokoka vita ya nyuklia.” Habari iliyopo haijapangwa vizuri mahali pamoja lakini inapatikana kwenye maelfu ya mahali pa kupata habari ulimwenguni pote. Hivi majuzi mtafiti mmoja Msweden alihesabu ujumbe au habari za kutumwa 5,651 kuhusu pornografia ya watoto katika vikundi vinne vya watumizi wa kompyuta kwa juma moja.

Makasisi Wanaosumbuka

“Asilimia 50 ya makasisi wanaonijia ili kutibiwa masumbuko ya kiakili wana matatizo yenye asili ya kingono,” ataarifu Valerio Albisetti, mmoja wa wanasaikolojia Wakatoliki wa Italia wajulikanao sana, kulingana na gazeti la habari La Repubblica. Zaidi ya kitu kinginecho chote, tamaa ya kingono na uhitaji wa kuwa baba ndiyo mambo ambayo yanasumbua wanaume hawa, ambao hivi majuzi wajibu wao wa useja ulikaziwa tena na John Paul 2. Albisetti anadokeza kutia moyo wanaume kuingia ukasisi wanapokuwa na umri mkomavu zaidi na kupandisha umri wa kuingia katika seminari. Yeye adokeza kwamba “ni jambo lenye kudhuru sana kwa afya ya kiakili na usawa wa kisaikolojia wa kasisi wa wakati ujao” kuishi maisha yake ya ubalehe “katika mpango ambamo hakuna watu wa kike.” Kando na matatizo yanayohusiana na hali ya ngono, Albisetti asema kwamba “mara nyingi makasisi hupatwa na mshuko-moyo, masumbufu ya hali ya kichaa na tamaa ya chakula isiyo ya kawaida.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki