Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Furahia Kukimbia-Kimbia—Lakini Chunga Hatari!
    Amkeni!—1995
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Uanastampu—Hobi Inyweayo Wakati Iliyo Biashara Kubwa
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 11/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Tuliokolewa na Amkeni! Miaka kadhaa iliyopita Amkeni! (Mei 8, 1984) lilidokeza kwamba kila familia izungumze jambo la kufanya kukitokea moto na iwe na mazoezi ya kawaida ya jinsi ya kutoroka wakati wa moto. Mume wangu nami tulifuata shauri hili. Katika Januari wa mwaka huu, tulikuwa na fursa ya kutumia kile tulichokuwa tumejizoeza wakati ambapo niliamka na kupata orofa ya chini ya nyumba yetu ikiungua sana. Kila mmoja wetu alifanya kama tulivyokuwa tumejizoeza na tukatoka nje salama. Sijapata kamwe kuwa na shukrani kwa ajili ya makala ya Amkeni! kama nilivyo!

G. E., Ujerumani

Ni Mashahidi tu Wenye Kutokuwamo? Toleo lenu la Mei 8, 1995, (“Si Siri Tena Kamwe”) lilitaarifu hivi: “Ni Mashahidi wa Yehova tu ambao wamedumisha kutokuwamo kwao na kukataa kujifunza ama kufanya kamwe vita tena.” Katika Vita ya Ulimwengu 2, kati ya wanaume 11,996 waliokataa kupigana, ni 940 tu walikuwa Mashahidi wa Yehova. Mimi mwenyewe nilikuwa mkataaji kidhamira. Neno “tu” katika taarifa yenu lilitumiwa kutoa wazo lenye kosa kwamba ni Mashahidi wa Yehova pekee walikuwa na itikadi hiyo.

P. B., Marekani

Twatambua kwamba watu fulani wamekataa kushiriki katika vita, na tumekubali hili katika vichapo vyetu. (Ona “Amkeni!” (Kiingereza) la Septemba 8, 1987, ukurasa 7.) Hata hivyo, taarifa inayozungumziwa hapa ilirejezea kihususa kukosa kwa “waamini wa Katoliki na Othodoksi” kudumisha kutokuwamo katika Rwanda, Liberia, Balkani, na mahali kwingineko kwenye mapigano ya hivi majuzi. Kati ya matengenezo mengine ya kidini, ni Mashahidi wa Yehova tu wamekuwa na msimamo wa kutokuwamo kwa kuendelea.—Mhariri.

Seminari za Hospitali Asanteni sana kwa ile makala “Seminari za Kuboresha Mahusiano Kati ya Madaktari na Mashahidi wa Yehova.” (Machi 22, 1995) Ninashukuru sana kwa ajili ya Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali. Nina umri wa miaka 81, na nilivunjika mfupa wangu wa paja na bega nilipokuwa nimesafiri kutoka nyumbani. Halmashauri ya mahali hapo ilifika hospitali dakika 30 kabla ya mimi. Kwa kuwa sikuwa na mtu wa familia huko, mmoja wa hao ndugu alibaki nami katika muda wote wa upasuaji. Ni kitulizo kilichoje! Kwa kweli mpango wa HLC ni baraka kutoka kwa Yehova.

A. W., Marekani

Hatari za Kukimbia-Kimbia Mimi ni mkimbiaji wa kawaida. Kwa sababu ya makala yenu “Furahia Kukimbia-Kimbia—Lakini Chunga Hatari!” (Machi 22, 1995), nina uhakika kwamba wengi wa Wakristo wenzangu wataniona kuwa mtu asiye na usawaziko. Pia ninaogopa wengi wataepuka kukimbia kwa sababu ya maoni hasi mliyotokeza. Wakimbiaji hawaelekei kupatwa na mshiko wa moyo kama mnavyodai. Na endorphins hutokea katika ubongo si katika neva za misuli ya mwili kama mnavyotaarifu.

C. D., Marekani

Haikuwa nia yetu kupatia ukimbiaji sifa mbaya. Tulikubali manufaa za mazoezi lakini tukatia moyo wasomaji kuwa na usawaziko na kutotumikisha miili yao kupita viwango vifaavyo. Utafiti zaidi utahitajika kufanywa kabla ya kujulikana kukimbia kuna hatari ya kiafya kadiri gani kwa watu fulani. Kuhusu “endorphins,” “The New Encyclopædia Britannica” yahakikisha kwamba hizo “husambazwa katika njia inayofanana kotekote katika mfumo wa neva.” Kwa habari ya hatari ya mshiko wa moyo, “The Medical Post” lakubali kwamba mazoezi ya kujikaza sana hupunguza hatari ya jumla ya kukoma kwa mpigo wa moyo; hata hivyo, hilo hutaarifu kwamba kuna “hatari iliyoongezeka kwa mfanya-mazoezi wakati anapofanya mazoezi.”—Mhariri.

Ukusanyaji Stampu Nilipenda ile makala “Uanastampu—Hobi Inyweayo Wakati Iliyo Biashara Kubwa.” (Januari 8, 1995) Ninasadiki kwamba Amkeni! haliachi chochote—si hata stampu za barua. Mimi hukusanya stampu ikiwa hobi yangu na nilihisi makala hiyo ikiwa kamili sana. Asanteni kwa madokezo yenu yenye thamani.

R. C., Venezuela

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki