Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 11/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Waazteki—Pambano Lao Lenye Kuvutia Ili Kuokoka
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2004
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 11/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Komahedhi Nawashukuru kutoka moyoni kwa ule mfululizo “Uelewevu Mzuri Zaidi wa Komahedhi.” (Februari 22, 1995) Nina umri wa miaka 43, nanyi mlinipa majibu yenye kuridhisha ya maswali yangu. Wanawake wawili ninaofanya kazi pamoja nao waliniomba nakala kadhaa, lakini ilinibidi kuwaazimu nakala yangu ya kibinafsi. Yalikuwa yamekwisha kutanikoni!

M. H. S., Brazili

Hizo makala zilifungua akili na moyo wangu ili kuona aina ya badiliko analolipitia mama yangu. Natumaini nitaweza kuendelea kulielewa badiliko hili katika maisha yake na kuwa mwenye kusaidia zaidi.

A. K., Marekani

Nina umri wa miaka 47, na hadi nilipopokea toleo hilo la Amkeni!, sikuelewa lolote kuhusu hiyo habari, hata baada ya kuwaona madaktari. Mmenisaidia kuelewa kwamba mabadiliko haya ni ya kawaida. Sasa niko tayari kukabili hayo matatizo.

E. M., Sierra Leone

Hivi majuzi nilihudhuria semina ya muda wa saa tatu juu ya habari hii. Ilipangwa na idara za elimu za hospitali mbili kuu. Programu yenyewe ilikuwa yenye kuarifu kwelikweli, lakini nilijifunza mengi katika dakika 30 kwa kusoma Amkeni! kuliko niliyojifunza kwa muda wa saa tatu kwenye semina.

J. B., Marekani

Je, Makala Hazipo? Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 11. Niligundua kwamba hamchapishi tena ule mfululizo wa makala “Vijana Huuliza . . .” Kwa nini? Kwa kweli nilifurahia sehemu hiyo. Baadhi ya maswali yalinihusu, nami jinsi nilivyopenda kuyasoma! Hilo lilikuwa jambo la kwanza kuangalia nilipopata Amkeni! Nina hakika kwamba watoto wengineo wanahisi vivyo hivyo. Je, wakati ujao mtachapisha sehemu hiyo?

E. K., Marekani

“Vijana Huuliza . . .” itaendelea kuchapishwa mara moja kwa mwezi. Itatokea katika toleo la tarehe 22 la kila mwezi. Tangu mifululizo hiyo ianze katika 1982, makala zipitazo 300 zimechapishwa katika mfululizo huu. Tunawatia moyo wasomaji wetu wachanga kuchunguza baadhi ya makala hizo za zamani zaidi. Hata hivyo, mwe na hakika kuhusu upendezi wetu wa daima juu ya matatizo ya walio wachanga.—Mhariri.

Baraza la Kuhukumu Wazushi Katika makala yenu “Lile Baraza la Kuhukumu Wazushi Mexico—Lilitendekaje?” (Oktoba 8, 1994), mlirejezea “mfalme wa Waazteki, Netzahualcóyotl.” Hata hivyo, Netzahualcóyotl hakuwa mfalme wa Waazteki bali mfalme wa Wachichimeka.

E. R. C. L., Mexico

Kwa kweli Netzahualcóyotl alikuwa Mchichimeka, si Mwazteki. Ingawa hivyo, kwa kupendeza vitabu vya marejezo, kama vile “Nueva Enciclopedia Cultural IEPSA,” humrejezea kuwa “mfalme wa Waazteki.” Kama vile kitabu “Historia de México” kielezavyo, Netzahualcóyotl alitawala “katika muungano na Waazteki,” ambao tayari waliwatawala Wachichimeka.—Mhariri.

Vijana “Wapotovu” Siwezi kuanza kuwasimulia ile motisha ya kiroho niliyopokea kwa kusoma ile makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kunyooshaje Maisha Yangu?” (Januari 8, 1995) Hiyo ilinipa ujasiri wa kusali kwa Yehova na kumwomba msamaha kwa dhambi nilizotenda awali. Kabla ya kusoma makala hii, mchana na usiku moyo wangu uliugua kuhusu dhambi hizi. Siku nyingi nilikuwa nikilala kitandani na kuhisi kwamba kujiua kulikuwa suluhisho la pekee. Sasa najua kwamba kanuni za Yehova ni zenye kutunufaisha, nami nitajifunza kutokana na makosa yangu ya awali.

Q. B., Marekani

Nikiwa kijana, nilimwacha Yehova na tengenezo lake. Ingawa, ni miaka ipatayo mitano tangu nirudi, nyakati nyingine nilikuwa nikihisi kwamba Yehova hangeweza kunisamehe kabisa. Sasa najua kwamba nilikosea; zile hisia za mashaka zenye kusumbua zilizokuwa ndani ya moyo hatimaye zimetulia.

R. D., Trinidad

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki