Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Mwanabarafu wa Alpine Nimemaliza tu kusoma “Lile Fumbo la Mwanabarafu wa Alpine.” (Mei 8, 1995) Ni lazima nikubali kwamba nilipoipata mara ya kwanza, kwa kweli sikufikiri ningependa hiyo habari. Lakini nilipata hiyo makala ikiwa yenye kupendeza sana! Nilithamini vile ambavyo ilionyesha kwamba maoni ya kidesturi ya mtu “asiyestaarabika” si sahihi.
J. S., Marekani
Kichwa chenye kuvutia kilinisaidia kumwangushia mwanamume mmoja niliyekutana naye hilo gazeti kwenye gari-moshi. Juma lililofuata nilikutana naye tena, naye akasema kuwa aliona hiyo makala ikiwa “uandishi bora kabisa” na habari iliyokuzwa vizuri. Yeye alikubali toleo la Mnara wa Mlinzi la karibuni zaidi.
G. C., Japani
Komahedhi Katika mfululizo wenu “Uelewevu Mzuri Zaidi wa Komahedhi” (Februari 22, 1995), mlitaja kutumia “mafuta ya mimea au ya matunda, vitamini-E, na geli za kulainisha” kuwa ponyo kwa kukauka kwa uke. Nikiwa mwanafunzi wa darasa la juu wa uuguzi, nahisi kushurutika kutaja kwamba ulainishaji wa mafuta ya matunda au mafuta huandaa mahali pa ukuzi wa bakteria. Kwa hiyo vilainishaji vinavyoweza kuyeyuka majini ni bora.
H. W., Marekani
Twathamini kupata habari hii ya karibuni zaidi.—Mhariri.
Nilipofika umri wa miaka 45, nilianza kupatwa na vipindi vya joto ya ghafula mwilini. Nilivivumilia kwa miaka mingi bila tiba. Kwa hivyo nililia nilipokuwa nikihisi utunzi wenye upendo uliodhihirishwa katika makala yenu. Ilinisaidia kuelewa komahedhi vizuri zaidi, nayo ikajibu mengi ya maswali yangu.
S. T. B. A., Brazili
Michezo ya Kompyuta Nilisisimuka kuona makala “Je, Mchezo Huu Unakufaa?” (Mei 8, 1995) Nikiwa mzazi, naudhiwa na mtazamo wa kutojali wa watu fulani ambao hufikiri michezo hii ni furaha isiyo na dhara. Kuna michezo mingi yenye kuelimisha na isiyo na jeuri.
K. G., Marekani
Mimi ni mkaguzi wa programu za kompyuta, na majuzi nilipewa nakala ya mchezo Doom 2 kwa ajili ya ukaguzi. Nilipata kwamba huo mchezo hutumia mifano ya kishetani, kama vile misalaba iliyopinduliwa na nyota za kimazingaombwe ziitwazo pentagramu. Natumaini watu watatambua jinsi michezo hii ilivyo mibaya.
R. B., Marekani
Ndoa Changa Asanteni kwa makala “Vijana Huuliza . . . Tumeoana Mapema Mno—Je, Tunaweza Kufaulu?” (Aprili 22, 1995) Tukiwa waangalizi wa kutaniko, tulikuwa tumepanga kufanya ziara ya uchungaji kwa mume na mke wachanga waliokuwa na matatizo ya ndoa. Nilishangaa kama nini wakati toleo hili lilipofika! Kilikuwa kile tulichohitaji tu ili kusaidia mume na mke hao wachanga. Tulizungumzia makala nzima na vilevile maandiko ya Biblia yaliyonukuliwa.
M. C., Brazili
Uvinjari wa Chini ya Bahari Tulithamini sana ile makala “Kuvinjari kwa Usalama Ulimwengu Ulio Chini ya Mawimbi.” (Mei 8, 1995) Tumerudi tu nyumbani kutoka safari huko Bahari Nyekundu tukapata kwamba shauri lenu lilikuwa lenye mafaa sana. Hatukuvinjari sakafu ya bahari yenye fahari tu bali pia tuliokoa pesa nyingi sana!
V. C. na K. B., Italia
Mume wangu nami pindi kwa pindi hupata matatizo kuhusiana na utendaji wa kufurahisha wa wana wetu wawili. Mume wangu hupendezwa na kuruka mtumbwi, na shule mpya ya urukaji mtumbwi imeanzishwa katika eneo letu. Baada ya kusoma makala yenu, nafurahi kwamba naweza kuwa na dhamiri njema wanaposhiriki utendaji huo.
C. P., Ujerumani
Kuokoka Ukomunisti Asanteni sana kwa ile makala “Zaidi ya Miaka 40 Chini ya Marufuku ya Ukomunisti.” (Aprili 22, 1995) Moyo wangu uliguswa kwa kina nilipokuwa nikiisoma. Ilinionyesha jinsi Yehova hutoa utegemezo unaohitajiwa kwa wakati ufaao ili mtu aweze kudumisha uaminifu-maadili.
S. A. A., Ghana