Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 2/22 uku. 25
  • Yule Tai-Mzoga-Kidevu Mwenye Uweza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yule Tai-Mzoga-Kidevu Mwenye Uweza
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Wakaguzi wa Usafi wa Angani
    Amkeni!—1993
  • Mfupa—Una Ugumu Usio na Kifani
    Amkeni!—2010
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
Amkeni!—1996
g96 2/22 uku. 25

Yule Tai-Mzoga-Kidevu Mwenye Uweza

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UINGEREZA

TAI-MZOGA-KIDEVU aliye mkuu ni ndege mwenye fahari, ana urefu wa sentimeta 120 toka mdomoni hadi mkiani. Anaweza kuonekana akielea angani kwa urahisi kwa kutumia mabawa yake yenye kupanuka meta tatu akiwa juu ya safu za milima katika Ulaya na Afrika, na hata nyakati nyingine akiwa kimo cha kilometa nane kwenda juu katika milima ya Himalaya. Kiumbe huyu mwenye fahari, akiwa na kifua na shingo yenye rangi ya machungwa na kichwa chenye rangi nyeupe na nyeusi, ana manyoya marefu yanayoning’inia kutoka mdomo wake wa chini. Hii ndiyo sababu ya jina lake, tai-mzoga-kidevu. Kwa kuwa anaishi maeneo ya mbali na ya ukame, ni chakula cha aina gani anachopata ili kujiruzuku?

Vitabu vingine vya marejezo hushikilia kwamba tai-mzoga-kidevu huwinda viumbe hai—chamoisi, wana-kondoo, wana-mbuzi, sungura, na wanyama wadogo wenye kutembea kwa miguu minne—lakini vyanzo vingine vyenye mamlaka hupinga hilo. “Hakuna kamwe visa vilivyothibitishwa vya ndege huyu akishambulia mnyama aliye hai,” yasema The World Atlas of Birds, ingawaje anajulikana kuwa yeye hula manyoya-manyoya yaliyotapikwa na ndege wengine, ambayo mnofu wote umesagwa kutoka kwayo. Basi ndege huyu hula nini?

Tai-mzoga-kidevu hubeba mifupa ya wanyama waliouawa na wanyama wawindaji au waliokufa kwa njia nyingine juu sana na kuiachilia ianguke kwenye miamba iliyoko chini. Sikuzote imekisiwa kuwa yeye huvunja mifupa kwa njia hii ili apate kuufikia uboho. Sasa, kufuatia uchunguzi wa kina uliofanywa juu ya ndege hao walio hai na waliokufa, watafiti, kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland wameweza kutoa maelezo yaliyo tofauti, gazeti The Economist laripoti.

Tai-mzoga-kidevu humeza vipande vya mifupa vyenye urefu wa sentimeta 25 na upana wa sentimeta nne. Hata hivyo, watafiti, walishangaa walipogundua kwamba ndege huyo hana viungo vya pekee vya kusagia chakula, kama vile firigisi, vya kumsaidia kukabiliana na chakula chake kisichoweza kuyeyushwa. Kiungo cha pekee kisicho cha kawaida ni koo yenye uwezo mkubwa wa kunyumbuka inayowezesha vipande vya mifupa kupita. Hata hivyo, tumbo la tai-mzoga-kidevu lina mengi ya kueleza.

Wanasayansi walishangaa kugundua kwenye tumbo chembe-chembe nyingi zinazotoa asidi kali—iliyo kali kuliko asidi ya betri—inayoyeyusha kalsiamu ya mifupa, kwa njia hiyo ikiitenganisha protini kutoka kwa mafuta ya uboho. Chakula hiki kinatoa kiwango cha juu cha nguvu kuliko mlo wa nyama wenye uzito uleule. Jambo lenye kushangaza hata zaidi ni kwamba vimeng’enya vinapatikana katika mazingira haya ya asidi. Kwa hivyo sasa lile fumbo la jinsi kiumbe huyu mwenye nguvu anavyoishi kwa chakula kidogo ambacho asilimia 90 yacho ni mifupa limefumbuliwa—ajabu nyingine ya uumbaji.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

© Nigel Dennis, Photo Researchers

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki