Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 7/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1996
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 7/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kuishi Milele Asanteni kwa mfululizo “Kwa Nini Maisha Ni Mafupi Mno?—Je, Yatapata Kuwa Tofauti?” (Oktoba 22, 1995) Makala hizi zilinisaidia si tu kuelewa vyema taraja la kuwa mwanadamu mkamilifu kwenye dunia iliyo paradiso bali pia zilinisaidia katika somo la sayansi. Wakati tu ambapo makala hizi zilitokea, tulikuwa na mtihani kuhusu chembe—sehemu zayo na kazi zinazofanya. Jinsi mlivyoifafanua waziwazi! Asanteni kwa maksi nilizopata na kwa chakula cha kiroho kwa wakati ufaao.

B. M., Marekani

Kioo Asanteni kwa makala “Kioo—Watengenezaji Wacho wa Kwanza Waliishi Zamani za Kale.” (Novemba 22, 1995) Baba yangu hufanya kazi ya vioo, kwa hiyo tuna vingi nyumbani mwetu. Nahisi kusukumwa kusema jinsi makala hizo zilivyoandikwa kwa njia bora sana. Sikujua ni tamaduni nyingi hivi zilizohusika katika kufanyiza kioo. Asanteni tena.

M. B., Marekani

Mashamba ya Mizabibu ya Hungaria Kwa miezi kadhaa nimekuwa nikifanya kazi katika sehemu ya divai ya duka kubwa Luxembourg. Kwa hiyo nilisoma kwa upendezi mwingi makala “Njoo Nasi Kwenye Mashamba ya Mizabibu ya Hungaria!” (Septemba 8, 1995) Hata hivyo, mmoja wa wasimamizi wangu alionelea kwamba ingawa makala hiyo ilikuwa sahihi, mlielekea kudokeza kwamba ukungu unaokua juu ya zabibu (Botrytis cinerea) ndio ukungu uleule ukuao katika vyumba vya kuhifadhia divai. Yeye asema kwamba ukungu huu wa pili hasa ni kitu kiitwacho Cladosporium cellare.

B. P., Ufaransa

Msimamizi wako asema kweli, nasi twamshukuru kwa rekebisho hilo.—Mhariri.

Rafiki ya Mungu Nataka tu kuwaeleza jinsi nilivyoguswa moyo na makala “Vijana Huuliza . . . Je, Kuwa Rafiki ya Mungu Kutanisaidia?” (Novemba 22, 1995) Kwa sehemu kubwa ya mwaka huu, nimekuwa nikipita kati ya bonde la giza kuu, huku mshuko-moyo ukiharibu kujistahi kwangu kulikobaki. Sikuwa hata na nguvu ya kusali au kujifunza Biblia. Kitia-moyo kilichotolewa na ndugu zangu wa Kikristo hakikuniathiri. Nilipokuwa nikisoma makala hiyo, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwangu kuhisi kuchangamka, baada ya muda mrefu.

S. K., Ujerumani

Inafariji kujua jinsi Yehova anavyopendezwa na kuwapenda vijana. Katika maisha yangu mafupi, nimepitia kulalwa kinguvu, utumizi mbaya wa dawa za kulevya, kuharibika kwa mimba, na kutendewa vibaya kihisia-moyo na shambulio la maneno machafu. Hata nilijaribu kujiua kimakusudi mara moja. Hata hivyo, mwishowe, nilianza kuhudhuria mikutano ya Kikristo tena. Kwa kudumu katika sala na kwa kumkaribia Yehova tena, nilirudishwa katika tengenezo lake. Neno la Yehova limeniletea amani ya akili kuliko dawa nyingineyo yote.

W. B., Marekani

Mashindano Makala “Maoni ya Biblia: Je, Mashindano Katika Michezo ni Kosa?” (Desemba 8, 1995) iliandaa faraja kwa mwana wangu mwenye umri wa miaka kumi. Wavulana wengine wenye umri mkubwa zaidi walimwalika kucheza mpira. Alidhihakiwa vibaya sana hivi kwamba akashuka moyo sana. Tulisoma hiyo makala na kupata faraja, tukijua kwamba Wakristo wanapaswa kudumisha maoni yaliyosawazika ya michezo na kwamba michezo yapasa kuburudisha, si kushusha moyo. Natumaini wachanga wetu wote watasoma makala hii kwa sababu michezo fulani imekuwa yenye jeuri sana.

S. H., Marekani

Makala hiyo ilinisaidia kikweli katika kufanya uamuzi kuhusu kujihusisha katika timu ya michezo shuleni. Maandiko yaliyoonyeshwa katika hiyo makala yalikuwa ya moja kwa moja kikweli. Kujihusisha na timu hii kungekuwa kwenye mashindano sana, kwa kuwa makocha kwa kawaida huwaambia mcheze kwa ushupavu na kushinda. Asanteni kwa makala hiyo yenye kuelimisha, na natumaini itasaidia vijana wengine kufanya uamuzi mzuri.

L. M., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki