Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/8 kur. 3-4
  • Wenyeji wa Amerika—Mwisho wa Muhula

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wenyeji wa Amerika—Mwisho wa Muhula
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Upinzani wa Mwisho wa Custer na Machinjo Katika Wounded Knee
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Jinsi Ulimwengu Wao Ulivyopotea
    Amkeni!—1996
  • Je, Wahindi wa Brazili Wanakabili Hatari ya Kutoweka?
    Amkeni!—2007
  • Mlima Wachongwa Kuwa Sanamu ya Ukumbusho
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/8 kur. 3-4

Wenyeji wa Amerika—Mwisho wa Muhula

NI NANI ambaye hajapata kuona sinema asili za cowboys na Wahindi? Watu ulimwenguni pote wamepata kusikia juu ya Wyatt Earp, Buffalo Bill, na Lone Ranger na Wahindi Geronimo, Fahali Aketiye, Farasi Mwehu, na Chifu Joseph, pamoja na wengine wengi. Lakini sinema za Hollywood zimekuwa sahihi kwa kadiri gani? Nazo zimekuwa zenye haki kadiri gani katika kuonyesha Wahindi?

Hadithi ya ushindi wa watu wa Ulaya dhidi ya Wenyeji wa Amerika Kaskazini (Wahindi) huzusha maswali.a Je, vitabu vya historia vimeeleza juu ya Wahindi kwa njia ya haki? Je, kuna masomo yoyote ya kujifunza kuhusu pupa, udhalimu, ubaguzi wa rangi, na mambo ya ukatili? Ni nini hadithi ya kweli juu ya wale walioitwa eti cowboys na Wahindi?

Upinzani wa Mwisho wa Custer na Machinjo Katika Wounded Knee

Katika mwaka wa 1876, mganga aitwaye Fahali Aketiye wa Lakota (ambayo ni mmojawapo migawanyiko mitatu ya kabila la Sioux) alikuwa kiongozi kwenye vita maarufu ya Mto Little Bighorn, katika Montana. Akiwa na wanajeshi 650, Luteni Kanali Custer “Nywele Ndefu” alifikiri kwamba angeweza kushinda kwa urahisi wapiganaji Wasioux na Wacheyenne 1,000. Alikosea vibaya sana. Alikuwa akikabili labda kundi kubwa zaidi la wapiganaji Wenyeji wa Amerika ambalo lilipata kukusanywa—wapatao 3,000.

Custer aligawanya Kikosi chake cha 7 katika vikundi vitatu. Bila kungoja utegemezo wa vile vikundi vingine viwili, kikundi chake kilishambulia pale Custer alipoona kuwa dhaifu katika kambi ya Wahindi. Wakiongozwa na wakuu wao Farasi Mwehu, Nyongo, na Farasi Aketiye, Wahindi hao waliangamiza Custer na kikundi chake cha wanajeshi wapatao 225. Huo ulikuwa ushindi wa muda tu kwa makabila ya Wahindi lakini ushinde mchungu kwa Jeshi la Marekani. Hata hivyo, kisasi kibaya sana kililipizwa miaka 14 baadaye.

Hatimaye, Fahali Aketiye alisalimu amri, baada ya kuahidiwa kwamba atasamehewa. Badala ya hivyo, alifungwa kwa muda fulani Fort Randall, Eneo la Dakota. Katika miaka yake ya uzeeni, alitokea mbele ya umma katika maonyesho ya kusafiri ya Wild West ya Buffalo Bill. Huyo ambaye awali alikuwa kiongozi mwenye sifa sana alikuwa amepoteza umashuhuri wa uganga.

Katika 1890, Fahali Aketiye (jina lake la Kilakota likiwa Tatanka Iyotake) alipigwa risasi akafa na polisi Wahindi ambao walikuwa wametumwa kumshika. Wauaji wake walikuwa Wasioux “Vifua Chuma” (polisi wenye beji), Luteni Kichwa Fahali na Sajini Shoka Jekundu.

Katika mwaka uo huo, upinzani wa Wahindi kwa udhibiti wa wazungu hatimaye ulishindwa katika machinjo ya Wounded Knee Creek kwenye Nyanda Pana za Marekani. Huko, wanaume, wanawake, na watoto Wasioux wenye kutoroka wapatao 320 waliuawa na majeshi ya serikali wakitumia mizinga yao aina ya Hotchkiss ya kulipua haraka-haraka. Wanajeshi hao walijigamba kwamba hicho kilikuwa kisasi walicholipiza juu ya machinjo ya wenzao, Custer na watu wake, katika mabonde yanayokabili Mto Little Bighorn. Basi vikaisha vita na mapambano ya hapa na pale yaliyochukua zaidi ya miaka 200 kati ya masetla wa Amerika wenye kushambulia na makabila ya wenyeji wenye kushambuliwa.

Lakini Wenyeji wa Amerika walikujaje kukaa Amerika Kaskazini? Walikuwa na mtindo-maisha wa aina gani kabla ya mzungu kufika Amerika Kaskazini?b Ni nini kilichofanya washindwe na kutiishwa hatimaye? Na hali ya sasa ya Wahindi ikoje katika nchi inayodhibitiwa na wazao wa wahamiaji wa mapema kutoka Ulaya? Maswali hayo pamoja na mengine yatazungumziwa katika makala zifuatazo.

[Maelezo ya Chini]

a Ingawa neno “Mwenyeji wa Amerika” sasa hupendelewa na wengine, “Mhindi” bado pia hutumiwa sana katika vitabu vingi vya marejezo. Tutatumia maneno hayo kwa kubadilikana. “Mhindi” ni jina lisilofaa ambalo wenyeji walipewa na Columbus, ambaye alifikiri kwamba alikuwa amefika India alipofikia pale ambapo sasa panaitwa West Indies.

b Katika makala hizi tunashughulika na Wahindi wa Amerika Kaskazini pekee. Wahindi wa Amerika wa Mexico, Amerika ya Kati, na Amerika Kusini—Waaztek, Wamaya, Wainka, Waolmek, na wengineo—watazungumziwa katika matoleo yajayo ya gazeti hili.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Kuzika Wafu katika Wounded Knee

[Hisani]

Montana Historical Society

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki