Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 1/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Uasilishaji—Je, Unakufaa?
    Amkeni!—1996
  • Uasilishaji—Napaswa Kuuonaje?
    Amkeni!—1996
  • Uasilishaji—Kwa Nini na Jinsi Gani?
    Amkeni!—1996
  • Kuzaliwa Upya—Kunatimiza Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 1/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Uasilishaji Asanteni kwa mfululizo wa makala “Uasilishaji—Shangwe na Magumu.” (Mei 8, 1996) Mimi ni mtoto aliyeasilishwa, na sikujua kamwe jinsi ya kuongea habari hii na wazazi wangu walioniasilisha. Basi nilisisimka kupokea toleo hili la Amkeni! Hakuna makala ambazo zimepata kunigusa moyo kama hizi.

F. R. M., Brazili

Niliasilishwa, na hivi majuzi niliamua kuchunguza kwa kadiri niwezavyo kuhusu wazazi wangu walionizaa. Ingawa niliweza kupata habari muhimu kuhusu wazazi wangu, pia niligundua kwamba mama yangu alinilea kwa miezi mitatu kabla ya kunitoa niasilishwe. Jambo hilo liliniumiza sana! Nilijiuliza, ‘Kwa nini alifanya hivyo?’ Lile sanduku “Je, Mwana Wangu Atanitafuta?” lilifanya nielewe jinsi mama aonavyo mambo. Makala hiyo ilinisaidia kama nini kukabiliana na hali!

C. S., Marekani

Makala hizo zilikuwa nzuri na chungu kwangu. Nilitoa mwana wangu aasilishwe miaka 23 iliyopita. Nilifanya hivyo kwa sababu nilijua sitaweza kumtunza. Kila siku najiuliza, ‘Anaendeleaje? Maisha yamekuwaje kwake? Je, nitapata kumwona tena?’ Nyakati nyingine hatia hunilemea sana. Lakini namshukuru Yehova sana kwa ajili ya upendo wake na rehema.

S. F., Marekani

Ingawa tuna mwana wetu wenyewe, mume wangu nami tumekuwa tukifikiria kumwasilisha msichana mdogo. Makala hiyo ilinisaidia kuona mazuri na mabaya nayo itatusaidia kufanya uamuzi.

J. G., Marekani

Niliona kama mlikuwa mkishauri dhidi ya uasilishaji ulio mgumu. Lakini itakuwaje kwa watoto hao wakikataliwa? Leo tuna matatizo fulani na mwana wetu aliyeasilishwa. Lakini ni matatizo ya aina gani watoto hao watafanyia jamii ikiwa hawakupata kamwe upendo na usalama wa familia?

D. M., Ujerumani

Twasikitikia watoto wasiopata utunzi wa wazazi wenye upendo. Makala hizo hazikuandikwa ili kuzuia uasilishaji wa watoto “wagumu,” bali kutia moyo wenzi wa ndoa ‘kuhesabu gharama’ ya kufanya hivyo, katika njia halisi. (Linganisha Luka 14:28.) Wazazi wanaotaka kuasilisha mtoto wapaswa kufikiria ikiwa kweli wana uwezo wa kutimiza mahitaji ya watoto kama hao kihisia moyo, kiroho, au kifedha. Wao wapaswa pia kupima athari ambazo uasilishaji waweza kutokeza kwa watoto wengine ambao tayari wamo nyumbani.—Mhariri.

Tumeasilisha watoto watano, kwa kuongezea watoto wetu watatu. Tumepata shangwe kuu mliyotaja na maumivu ya moyo. Watoto wetu wote ni wasifaji wa Yehova ila mwana wetu. Baada ya kuasilishwa akiwa na umri wa miaka 16, aliwatenda vibaya watatu kati ya binti zetu wachanga. Shirika la uasilishaji halikutuarifu juu ya historia yake. Basi mtu anapaswa kupata habari zote iwezekanavyo anapofikiria uasilishaji—hasa kama mtu anataka kuasilisha mtoto mkubwa. Makala zenu ziliandikwa vizuri nazo zilieleza vizuri mazuri na mabaya ya suala hilo.

P. B., Marekani

Nilihuzunika sana kujua kwamba wazazi fulani wenye kuasilisha watoto wamepatwa na maono mabaya kama hayo. Mume wangu nami tumeasilisha watoto wawili warembo, nao wametufanya tuwe na shangwe tele katika maisha yetu. Sikuzote tumeeleza wazi kuhusu uasilishaji wao. Tulifanya kila mmoja wao aelewe kwamba mama zao halisi ‘hawakuwatupa’ bali walipanga watunzwe kwa sababu wakati huo hawakuweza kutunza mtoto. Mara nyingi watu hutuambia kwamba watoto wetu wafurahi kwamba tuliwaasilisha. Lakini, ukweli ni kwamba ni sisi tunaofurahi zaidi.

B. M., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki