Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 3/8 uku. 31
  • Ombi Kutoka Moyoni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ombi Kutoka Moyoni
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Uasilishaji—Je, Unakufaa?
    Amkeni!—1996
  • Uasilishaji—Kwa Nini na Jinsi Gani?
    Amkeni!—1996
  • Jinsi Watoto Wanavyobadili Ndoa
    Unaweza Kuwa na Familia Yenye Furaha
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 3/8 uku. 31

Ombi Kutoka Moyoni

AMKENI! la Mei 8, 1996, lilikuwa na mfululizo wa makala juu ya habari ya uasilishaji. Tumeshangazwa kwa njia ya kufurahisha kuona itikio la wasomaji tulilopokea kutoka ulimwenguni pote. Barua ifuatayo ilikuwa yenye kugusa moyo hasa.

“Nahisi kushurutishwa kutaja kwamba wengi wetu tulioacha watoto wetu waasilishwe kwa kweli tulitaka kubaki nao. Nilikuwa tineja asiyeolewa na bado nilikuwa shuleni. Mara tu wazazi wangu walipojua kwamba nilikuwa mjamzito, waliniarifu kwamba nitangulize hali-njema ya mtoto kuliko yangu na kumwasilisha. Niliambiwa kwamba ‘mtoto ahitaji mama na vilevile baba,’ jambo ambalo sikuweza kuandaa. Wazazi wangu hawakutaka kubaki na mtoto huyo—sikuruhusiwa kukaa hapo ikiwa ningekuwa na mtoto. Ningefanya nini? Walisema: ‘Utamchukia mtoto wako kwa kuondoa uhuru wako.’

“Mara tu nilipoanza kuonekana waziwazi kwamba nilikuwa mjamzito, nilitolewa shuleni na kupelekwa kuishi na mtu wa ukoo. Nilipoondoka nyumbani, nilijua kwamba singekaribishwa huko tena hadi nilipozaa na kuasilisha mtoto wangu.

“Nilipelekwa kwa makao ya akina mama wasioolewa. Mfanyakazi wa kijamii aliponiuliza ikiwa nilikuwa na uhakika kuhusu uamuzi wangu wa kumwasilisha mtoto wangu, nilijua kwamba hakutambua kwamba sikuwa na chaguo jingine lolote. NILITAKA KUBAKI NA MTOTO WANGU! Nimetamani sikuzote kumwona akicheza na kuwa na furaha. Wasomaji wenu wahitaji kujua kwamba akina mama wengi wa asili huhisi kama nilivyohisi.

“Sikupewa chaguo jingine lolote lifaalo. Kwa hiyo nilifanya kile nilichoambiwa kilikuwa ‘masilahi bora’ ya mtoto huyo. Na nimeishi na maumivu mengi ya moyoni tangu wakati huo. Nina wasiwasi kwamba mwana wangu huenda atafikiri kwamba sikumjali na kwamba sikumtaka.

“Sasa, nikiwa Mkristo, sikuzote mimi huthamini shauri la Biblia juu ya hali ngumu ambazo sisi hujiletea kwa sababu ya kutotumia Neno la Mungu katika maisha zetu. Huonyesha matokeo yenye maumivu na yenye kina ya kusababu kwa njia ya kilimwengu. Lakini watu walioasilishwa wahitaji kujua kwamba sababu tu kwamba waliasilishwa, haimaanishi kwamba hawakutakwa. Tafadhalini acheni wajue hilo!”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki