Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 12/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • “Kaa Tuli na Ukaze Fikira!”
    Amkeni!—1997
  • Kunguru—Ni Nini Kinachomfanya Awe Tofauti?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 12/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kuumwa na Nyoka Nikiwa mtaalamu wa nyoka, nina daraka la kuwatunza na kuwashika nyoka na vilevile kuondoa sumu zao. Zile makala “Je, Ungependa Kukutana na Fira?” (Machi 22, 1996), “Habu—Nyoka wa Kuepukwa” (Julai 8, 1996), na “Hatari! Nina Sumu” (Agosti 22, 1996) zote zilionyesha mtazamo chanya kuelekea uumbaji wa Yehova. Lakini, ningependa kutaja kwamba haipendekezwi kufunga mipira ukiumwa na nyoka. Watu wengi hawajui kuitumia vizuri, na wengine wamepoteza viungo kwa sababu hiyo. Napendekeza sana kutumia bendeji ya mkazo ili kufunga kiungo kilichoumwa kwa mkazo uleule utumiwao kufunga bendeji kwenye kifundo cha mguu au cha mkono kilichoteguka. Ingawa sumu inabaki karibu na mahali palipoumwa, damu huendelea kuzunguka, ikifanya kiungo hicho “kiendelee kuwa hai.”

P. R., Uingereza

Vitabu kadhaa vya mafundisho ya kitiba vya hivi karibuni vinakubaliana na jambo hili, na tunamshukuru msomaji wetu kwa kuelewesha jambo hili.—Mhariri.

Kunguru Nilikuwa mgonjwa wakati makala “Kunguru—Ni Nini Kinachomfanya Awe Tofauti?” ilipotokea. (Januari 8, 1997) Karibu hakukuwa na kitu chochote ambacho kingeweza kunifurahisha. Lakini ustadi wa kunguru ulinifanya nicheke. Baadaye, nilitayarisha ripoti ya shule kuhusu ndege, nikitumia habari kutoka makala za Amkeni! Nilipata maksi za juu kwa ripoti hiyo!

J. B., Slovakia

Kasoro za Kujifunza Asanteni kwa mfululizo “Msaada kwa Watoto Wenye Kasoro za Kujifunza.” (Februari 22, 1997) Nina shule ya binafsi na nimefanyiza fotokopi kwa ajili ya walimu ambao nimewaajiri. Pia nimetengeneza vijarida vyenye msingi wa habari zilizo katika gazeti lenu. Asanteni kwa ajili ya usawaziko mlio nao katika kushughulikia masuala haya.

E. G., Honduras

Mimi ni mkurugenzi mkuu wa shirika kubwa zaidi la kitaifa lisilo la kujipatia faida linalotenda kazi kwa bidii kwa niaba ya watoto na watu wazima walio na Kasoro ya Upungufu wa Makini (ADD). Mnahitaji kupongezwa kwa ajili ya toleo lenu lenye ufikirio kuhusu Tatizo la Upungufu wa Makini Kutokana na Utendaji wa Kupita Kiasi (ADHD) na Kasoro ya Upungufu wa Makini (ADD). Hizi huwa ni kasoro zenye kulemaza na ambazo hazieleweki mara nyingi. Tunathamini mlivyokiri kwamba utambuzi unaofaa wa ugonjwa na tiba zilizothibitishwa kwa sasa zinasaidia watu wengi mmoja-mmoja ambao wanatafuta msaada. Mkazo wenu juu ya upendo wa wazazi na uelewevu watoa ujumbe wa maana pia.

L. R., Marekani

Nina mwana mwenye Tatizo la Upungufu wa Makini Kutokana na Utendaji wa Kupita Kiasi (ADHD), na imekuwa vigumu sana kwangu kukubali kwamba yeye si mtoto mkorofi tu. Mambo mengi yasiyo ya fadhili yamesemwa, kama vile, “Kwa nini hawamtii nidhamu?” Maneno kama hayo huumiza sana ninapofikiria uhakika wa kwamba nimetumia wakati mwingi nikijaribu kumtia nidhamu. Ninatumaini ya kwamba maelezo yenu juu ya kasoro hii itasaidia wengine watambue ya kwamba kwa kweli kuna tatizo na kwamba wengine wangeweza kuwa wenye kutia moyo zaidi.

M. T., Marekani

Mwaweza kuwazia tu jinsi sisi, tukiwa wazazi walio na mtoto mwenye kasoro za kujifunza, tulivyofurahia toleo hili. Twathamini hasa kutaja kwenu jinsi hili huathiri wazazi na ya kwamba tuna mzigo wenye kulemea wa kutosha kubeba bila kuhitaji kusikia maneno yenye kuchoma moyo kutoka kwa wengine.

J. C. na B. C., Kanada

Rafiki ya Mungu Asanteni sana kwa makala “Vijana Huuliza . . . Nawezaje Kuwa Rafiki ya Mungu?” (Februari 22, 1997) Ilinisaidia sana. Sasa nahisi nimeridhika, kwa kuwa sasa naelewa kwamba Yehova ni rafiki yangu! Nangojea kwa hamu makala juu ya namna ya kudumisha urafiki huu.a

T. E., Italia

[Maelezo ya Chini]

a Ona Amkeni! la Mei 22, 1997.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki