Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 12/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoelewana Hatari
  • Je, Mnara wa Pisa Unaoegemea Umeimarishwa?
  • Matumizi Haramu ya Madawa ya Kulevya ya Ulimwenguni Pote
  • Maradhi Yenye Kuambukiza Yaendelea Kuongezeka
  • “Sheria Mkononi”
  • Ujitoaji Wenye Kufifia wa “Jiji Takatifu”
  • Kifua Kikuu Chakumba India
  • Panya Mzuri?
  • Wasichana Waliochinjwa Sehemu za Uzazi, na Kuzaa kwa Matineja
  • Kinga Mpya Dhidi ya Kifua Kikuu
    Amkeni!—1999
  • Shangwe ya Ushindi na Huzuni
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1996
  • Kifua Kikuu Charudi kwa Pigo!
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 12/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Kutoelewana Hatari

Katika 1977 kutoelewana kulikohusisha maana ya neno dogo kulichangia msiba wa ndege uliokuwa mbaya zaidi ulimwenguni, laripoti gazeti la habari The European. Rubani Mholanzi wa Boeing 747 alitangaza kwamba alikuwa “mahali pa kuanzia kuruka,” ambalo mwongoza-ndege wa Tenerife, Visiwa vya Canary, alielewa alimaanisha kwamba ndege ilikuwa imesimama. Hata hivyo, rubani alimaanisha kwamba alikuwa anaongeza mwendo wa ndege akielekea kwenye barabara iliyokuwa na ukungu mzito na kwamba alikuwa karibu kuruka. Tokeo likawa kwamba ndege hiyo iligonga ndege nyingine aina ya 747 na kuua watu 583. Hali kadhalika, kutofahamu vizuri lugha kulichangia mgongano wa angani wa mwaka wa 1996 karibu na Delhi, India, ambapo watu 349 walikufa. Ijapokuwa makosa mazito ni nadra na wafanyakazi wa ndege hupokea mazoezi makali ya maneno ya Kiingereza yatumiwayo katika uwasiliano wa ndege, baadhi ya wafanyakazi wa ndege hujua maneno ya kipekee tu yanayohusiana na uwasiliano wa ndege. Wakati hali ya dharura inapotokea, wao waweza kusahau kabisa maneno yale. Wataalamu wanapendekeza kutumia tekinolojia ya kompyuta katika chumba cha rubani ili kuhakikisha kwamba kuna uwasiliano sahihi wa ndege.

Je, Mnara wa Pisa Unaoegemea Umeimarishwa?

Baada ya karne za mwinamo kuelekea anguko lililoonekana halingeepukika, Mnara wa Pisa unaoinama waonekana umeimarishwa hatimaye—kwa msaada wa uzito wenye kusawazisha wa tani elfu moja za vidonge vya risasi vilivyowekwa kwenye msingi wake. Hili lilitangazwa na Profesa Michele Jamialcowsky, msimamizi wa tume ya kimataifa ya kuhakikisha usalama wa mnara huo. “Hata hivyo, tatizo la kuimarika bado ni zito,” lasema gazeti la habari la Italia La Stampa, “kwa kuwa mwinamo wa meta tano kutoka utosini uliotokea kwa zaidi ya miaka mia saba ya kuwako kwake umefikia hali ya hatari sana.”

Matumizi Haramu ya Madawa ya Kulevya ya Ulimwenguni Pote

Madawa haramu ya kulevya huchangia sana kufikia asilimia 8 ya biashara yote ya kimataifa na mapato ya karibu dola bilioni 400 kwa mwaka, yasema ripoti ya UM. Ripoti hiyo yenye kurasa 332 ndiyo utafiti wa kwanza wenye mambo mengi juu ya athari ya ulimwenguni pote ya madawa haramu ya kulevya. Inaonyesha kwamba karibu asilimia 2.5 ya idadi ya watu ulimwenguni—kama watu milioni 140—huvuta bangi. Milioni 30 hutumia aina ya vichocheo vya amfetamini, milioni 13 hutumia aina fulani ya kokeini, na milioni 8 hutumia heroini. Ingawa mashirika ya kutekeleza sheria yametwaa maelfu ya tani za bangi, kokeini, heroini, na afyuni, mengi zaidi yameepa ugunduzi. Viwango vya kugundua kokeini njiani ni karibu asilimia 30 na asilimia 10 hadi 15 pekee kwa heroini, ilisema ripoti hiyo. Usafirishaji wa madawa ya kulevya kimataifa umekuwa tata sana. “Tatizo hilo ni la tufeni pote hivi kwamba haliwezi kushughulikiwa na nchi mojamoja,” asema Giorgio Giacomelli, mkurugenzi-mkuu wa shirika la UM la kudhibiti madawa ya kulevya.

Maradhi Yenye Kuambukiza Yaendelea Kuongezeka

“Mnamo miaka 20 iliyopita, magonjwa 30 mapya kabisa na yenye kuambukiza sana yameibuka,” laripoti Nassauische Neue Presse. Mengi ya maradhi haya—kama vile Ebola, UKIMWI, na mchochota wa ini aina ya C—hayana tiba. Zaidi ya hilo, maradhi ya kuambukiza kama malaria, kipindupindu, na kifua kikuu yanaendelea kuongezeka pia. Kwa nini? Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), “maradhi mengi yanatokea tena kwa sababu virusi vingi zaidi na zaidi vinazidi kukinza viuavijasumu vingi. Viuavijasumu vipya vinatokezwa kwa uchache kwa kuwa utaratibu wa kuvitokeza ni ghali sana.” Katika jitihada za kutangua mwelekeo huu, Shirika la Afya Ulimwenguni limeomba serikali na kampuni za madawa “zitenge fedha zaidi za kutokeza viuavijasumu vipya na kwa ajili ya njia zilizoboreshwa za kuchunguza maradhi ya kuambukiza.” Vifo vya tufeni pote kutokana na magonjwa ya kuambukiza katika mwaka wa 1996 vilikuwa karibu watu milioni 55.

“Sheria Mkononi”

Chini ya kichwa hiki, Haim Shapiro, mshiriki wa wafanyakazi wa uhariri wa The Jerusalem Post aripoti juu ya visa katika Machi iliyopita ambavyo katika hivyo Mashahidi wa Yehova walishambuliwa kwa mawe na matofali, jumba lao lilivunjwavunjwa na kuharibiwa, na fasihi zao zikachomwa. Alieleza: “Wakati Kanisa Katoliki katika Jaffa liliposhambuliwa mwaka jana, kulikuwa na wimbi la kuteta la papohapo—lililokuwa na haki—katika Israeli na ng’ambo. Wakati jumba liliposhambuliwa katika Lod, hakukuripotiwa chochote kuhusiana nalo.” Ijapokuwa yeye binafsi ‘hapendelei na kukubaliana’ na Mashahidi wa Yehova, Shapiro akumbuka kwamba wao “walikuwa mojawapo ya vikundi vilivyonyanyaswa na kupelekwa kwenye kambi za mateso katika Ujerumani ya Nazi.” Aandika: “Kuwazia kwamba mtu yeyote aweza kwa kuepuka adhabu, kushambulia watu kama hawa, kuvunjavunja mahali pao pa ibada, na kuchoma vitabu vyao kwatisha sana, na kukumbusha juu ya matukio mabaya sana kama hayo ya historia.”

Ujitoaji Wenye Kufifia wa “Jiji Takatifu”

Ijapokuwa linaitwa jiji takatifu na lina kiongozi wa Kanisa Katoliki akiwa askofu wake, Roma halikaribii kuwa la kidini sana kama wengine wafikirivyo. Kulingana na uchunguzi wa kitaifa uliofanywa na Third University of Rome, karibu asilimia 10 ya Waitalia wanataarifu kwamba hawapendezwi “kabisa” na Ukristo, lakini katika Roma tarakimu hii hupanda kufikia asilimia 19. Asilimia 21 zaidi ya Waroma wana upendezi “kidogo” katika Kanisa Katoliki, lataarifu gazeti la habari La Repubblica. Kwa upande mwingine, ni asilimia 10 tu kati yao, inayopendezwa sana na dini. Kulingana na mwanasoshiolojia Roberto Cipriani, ni Mroma 1 tu kati ya 4 wanaofuata kwa ukaribu maagizo ya kanisa kuhusu mitazamo na tabia.

Kifua Kikuu Chakumba India

Ijapokuwa jitihada nyingi za kudhibiti bakteria ya kifua kikuu, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ladai kwamba mtu mzima 1 kati ya kila 2 katika India wameambukizwa kifua kikuu. Miongoni mwa idadi ya watu zaidi ya milioni 900 wa India, zaidi ya milioni 2 hushikwa na kifua kikuu kila mwaka na kufikia 500,000 hufa kutokana nacho, laripoti gazeti la habari The Asian Age. Kulingana na WHO, idadi ya watu walioambukizwa na hatari inayotokezwa na kuambukizwa na ugonjwa huo ni kubwa sana. Wale wanaoshikwa na kifua kikuu hawahitaji kukabili tu tatizo linaloletwa na ugonjwa huu; wahitaji pia kuishi na fedheha inayoambatanishwa kwa ukawaida na ugonjwa huu. Hili laweza kuongoza kwenye kukataliwa na majirani, waajiri, na wafanyakazi wenzi. Bibi-arusi wachanga ambao wanapatikana wakiwa na kifua kikuu mara nyingi hurudishwa kwa wazazi wao kuwa hawastahili kuzaa watoto.

Panya Mzuri?

“Panya wanajulikana kuwa wabaya,” lataarifu The Wall Street Journal. Lakini ni tofauti na Rattie, panya wa maabara wa mtaalamu wa biofizikia Judy Reavis. Rattie amesaidia kufunga maelfu ya meta za waya za kompyuta katika shule nyingi ili mifumo ya kompyuta iweze kuwekwa. “Akiwa amekaza sana nyuzi katika meno yake, Rattie hujipenyeza kati ya mihimili na mifereji ndani ya kuta, chini ya sakafu na kandokando ya paneli za dari,” laeleza Journal. “Yeye ashawishwa kufikia mahali pa kutokea na sauti zenye kugonga na sahani ya chakula kitamu cha paka. Anapoibuka, uzi anaovuta unatumiwa kuvuta waya za kompyuta kwa kufuata mkondo wake uliopindika.” Rattie amekuwa maarufu na ana safu katika gazeti juu yake na wimbo “kutoka” kwake katika Internet. Rattie akifa kwa ghafula, “tutazoeza mwingine,” asema Dakt. Reavis. “Kwa vyovyote, ni panya tu.”

Wasichana Waliochinjwa Sehemu za Uzazi, na Kuzaa kwa Matineja

“Karibu wasichana milioni 2 huchinjwa sehemu za uzazi kila mwaka,” lataarifu toleo la 1996 la The Progress of Nations, kichapo cha Shirika la Hazina ya Watoto la Umoja wa Mataifa, kuhusu afya, lishe, na elimu ya watoto. “Misri, Ethiopia, Kenya, Nigeria, Somalia, na Sudan huchangia asilimia 75 ya visa vyote. Katika Jibuti na Somalia, asilimia 98 ya wasichana huchinjwa sehemu za uzazi.” Zaidi ya maumivu, utaratibu huo waweza kusababisha ambukizo, kutokwa damu kwa muda mrefu, utasa, na kifo. “Uchinjaji wa sehemu za uzazi si takwa la dini yoyote. Ni pokeo linalokusudiwa kuhifadhi ubikira, kuhakikisha uwezo wa kuolewa, na kuzuia utendaji wa kingono,” yataarifu ripoti hiyo. Vikundi na mashirika yanayohangaikia haki za wanawake na hali njema ya watoto, yanakaza serikali ziharamishe zoea hili.

Ripoti ya pili yaonyesha kwamba katika nchi nyingi kuzaa kwa matineja ni tatizo linalodumu. Kwa mfano, Marekani ina kiwango cha juu zaidi katika nchi zilizoendelea: uzawa 64 kwa mwaka kwa kila wasichana 1,000 wenye umri wa 15 hadi 19. Japani ina kiwango cha chini zaidi cha wanne kwa mwaka. Si kwamba kuzaa kwa matineja huathiri tu maendeleo, elimu, na fursa za mwanamke mchanga bali pia kwaweza kuleta matatizo kwa vitoto vichanga, kama vile utunzaji mbaya, umaskini, na mazingira yasiyo thabiti.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki