Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 12/22 kur. 8-9
  • Suluhisho la Duniani Pote—Je, Lawezekana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Suluhisho la Duniani Pote—Je, Lawezekana?
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ushindi Utakuja
  • Kinga Mpya Dhidi ya Kifua Kikuu
    Amkeni!—1999
  • Shangwe ya Ushindi na Huzuni
    Amkeni!—1997
  • Kifua Kikuu Charudi kwa Pigo!
    Amkeni!—1996
  • Muungano Hatari
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 12/22 kur. 8-9

Suluhisho la Duniani Pote—Je, Lawezekana?

WATAALAMU wakubaliana kwamba kifua kikuu ni tatizo la duniani pote ambalo lahitaji suluhisho la duniani pote. Hakuna nchi iwezayo kudhibiti kifua kikuu ikiwa peke yake, kwani mamilioni ya watu huvuka mipaka ya kimataifa kila juma.

Wengi waamini kwamba ushirikiano wa kimataifa, huhitaji mataifa tajiri kusaidia mataifa maskini, ambayo yamekumbwa sana na kifua kikuu. Kama Dakt. Arata Kochi asemavyo, “ni kwa faida ya mataifa tajiri kusaidia mataifa yasiyoendelea ili kupambana na kifua kikuu, kabla nchi zao hazijawa uwanja wa mapambano.”

Lakini mataifa tajiri, yakiwa yanahangaishwa na mambo wayaonayo kuwa ya kutangulizwa zaidi na matatizo, hayajachukua hatua za haraka kusaidia nchi maskini kupambana na kifua kikuu. Baadhi ya nchi maskini mara nyingi huacha kukazia uangalifu utunzaji wa afya, badala ya hivyo zikitumia fedha nyingi katika zana za vita. Kufikia katikati ya mwaka 1996, ni asilimia 10 tu ya wagonjwa wa kifua kikuu ulimwenguni waliokuwa wakitibiwa kwa mbinu ya DOTS, ambao ni wachache sana kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu.

Shirika la WHO laonelea hivi: “Ujuzi na dawa zisizo ghali za kutibu kifua kikuu zimekuwepo kwa miongo kadhaa. Kile ambacho ulimwengu wahitaji sasa ni juhudi zenye sulubu kutoka kwa watu wenye uwezo, uvutano na huruma ambao watahakikisha kwamba dawa hizi zinatumika kwa mafanikio ulimwenguni pote.”

Ushindi Utakuja

Je, twaweza kutazamia kwa hakika uwezo na uvutano wa wanadamu kutatua tatizo hili? Mtunga-zaburi wa Biblia aliyepuliziwa aliandika: “Msiwatumainie wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.” Basi, twaweza kumtumaini nani? Andiko hilo laendelea kueleza hivi: “Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake, aliyezifanya mbingu na nchi, bahari na vitu vyote vilivyomo.”—Zaburi 146:3, 5, 6.

Akiwa Mbuni na Muumba wa dunia, Yehova Mungu ana uwezo na hekima ya kumaliza ugonjwa. Je, ana huruma? Kupitia nabii wake aliyepuliziwa, Yehova aahidi: “Nitaonyesha huruma juu ya [watu wangu], kama vile mwanadamu aonyeshavyo huruma juu ya mwana wake ambaye anamtumikia.”—Malaki 3:17, NW.

Sura ya kumalizia ya Biblia yafafanua ono lililotolewa kwa mtume Yohana. Aliona “miti ya uhai yenye kutokeza mazao kumi na mawili ya matunda, ikitoa matunda yayo kila mwezi.” Miti hii ya ufananisho na matunda itokezayo yawakilisha maandalizi ya kimungu ambayo yatawawezesha wanadamu watiifu kuishi milele juu ya dunia.—Ufunuo 22:2.

Akiendelea, Yohana aliandika: “Na majani ya hiyo miti yalikuwa ya kuponya mataifa.” Majani ya ufananisho yaonyesha baraka kutoka kwa Mungu ambazo zitatokeza kuponywa kwa wanadamu, kiroho na kimwili. Hivyo, twaweza kuwa na hakika kwamba katika ulimwengu mpya wenye uadilifu chini ya utawala wa Mungu, kifua kikuu kitashindwa kabisa na kwa umilele.—Ufunuo 21:3, 4.

[Picha katika ukurasa wa 8, 9]

Mungu aahidi kuponywa kikamili kwa wanadamu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki