Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/8 kur. 12-13
  • Je, Misitu Yetu ya Mvua Itaokoka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Misitu Yetu ya Mvua Itaokoka?
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Uzalendo Mpya Baina ya Mataifa”?
  • Manufaa za Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998
  • Kutumiwa Vibaya kwa Misitu ya Mvua
    Amkeni!—1998
  • Misitu ya Mvua Je, Inaweza Kuokolewa?
    Amkeni!—2003
  • Huzuni kwa Msitu Huo wa Mvua
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/8 kur. 12-13

Je, Misitu Yetu ya Mvua Itaokoka?

MWANZONI mwa karne hii, ndege aliyeitwa passanger pigeon wa Amerika Kaskazini alitoweka. Huenda ikawa ndege huyu alikuwa na idadi kubwa zaidi ya ndege ambao wamewahi kuwako. Wataalamu wa ndege hukadiria kwamba karne mbili zilizopita idadi yake ilikuwa kati ya bilioni tano na bilioni kumi!

Hata hivyo, katika kipindi cha miaka mia moja, gawio lililoonekana kama haliwezi kwisha la nyama ya ndege likatoweka katika lile lielezwalo kuwa “kupunguka kwenye kutazamisha zaidi [kwa spishi] kwa kiwango cha juu kabisa.” Nguzo ya ukumbusho kwa ajili ya passenger pigeon katika Mbuga ya Wyalusing State, Wisconsin, Marekani, husomeka hivi: “Spishi hii ilitoweka kwa sababu ya ulafi wa mali na kutofikiria kwa mwanadamu.”

Masaibu ya passenger pigeon hutukumbusha kwamba hata viumbe wa dunia wenye kuzaa sana wanaweza kudhuriwa kwa urahisi na mashambulio ya mwanadamu. Ulafi wa mali na kutofikiria kungali kumeenea pote. Na leo si spishi moja tu bali ni mfumikolojia wote ulioko hatarini. Misitu ya mvua ikitoweka, wakazi wake wote—karibu nusu ya spishi zote za sayari—watatoweka pamoja nayo. Wanasayansi husema kwamba msiba kama huu ungekuwa “msiba mkubwa zaidi wa kibiolojia ambao umeweza kutokea wakati wowote [kwa kosa] la mwanadamu.”

Kweli, tuna ujuzi zaidi kuhusu mazingira kuliko tulivyokuwa nao karne moja iliyopita. Lakini ufahamu huu hautoshi ili kusimamisha wimbi lisilotulia la uharibifu. “Tunaangamiza kitu chenye thamani sana,” aomboleza mwanabotania Manuel Fidalgo, “na hatuna muda mwingi uliobaki. Nahofu kwamba katika muda wa miaka michache, misitu ambayo itabakia bila kuguswa tu itakuwa ile iliyoko kwenye miteremko ya milima ambayo haiwezi kufikiwa na wakataji-miti.”

Wanaviumbe wanashtuka kwa hofu kwa sababu ni vigumu sana kuirudisha misitu ya mvua. Kitabu The Emerald Realm: Earth’s Precious Rain Forests kwa wazi hueleza kurudisha misitu kuwa kwa “polepole na ghali, . . . msaada wa mwisho uliopo kwa ajili ya uharibifu wa misitu ya mvua.” Kwa ubora zaidi, kupanda upya huenda kukatia ndani spishi chache tu za miti ya kitropiki, na miti hiyo midogo huenda ikahitaji utunzaji wa daima ili kuzuia magugu yasiisonge.

Kama msitu utapata tena fahari yake wakati wowote itategemea ukaribu wa eneo lililopandwa upya na msitu wa mvua usioguswa. Ni eneo lililo karibu tu la eneo lililopandwa misitu upya ambalo hatimaye lingeweza kuchukuliwa na mamia ya maelfu ya spishi ambazo hufanyiza msitu wa mvua wa kweli. Hata hivyo, hatua hiyo ingechukua karne kadhaa. Sehemu kadhaa zilizoachwa maelfu ya miaka iliyopita wakati ustaarabu wa Mayan ulipoanguka zingali hazijarudia hali ya hapo awali kabisa.

“Uzalendo Mpya Baina ya Mataifa”?

Mwanasayansi mmoja katika Taasisi ya Smithsonian katika Washington, D.C., alipendekeza kwamba asilimia 10 ya misitu ya mvua iliyoko iwekwe kando kwa ajili ya wazao, ili kulinda spishi nyingi iwezekanavyo. Kwa sasa ni karibu asilimia 8 zinazolindwa, lakini nyingi za hifadhi hizi au mbuga za kitaifa ni mbuga kwa jina tu, kwani hakuna fedha wala wafanyakazi wa kuzitunza. Kwa wazi, jambo fulani zaidi lapasa kufanywa.

Peter Raven, msemaji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ya mvua, aeleza: “Jitihada za kuokoa msitu wa mvua hutaka kuwe na uzalendo mpya baina ya mataifa, utambuzi wa kwamba watu kila mahali wanashiriki daraka katika masaibu ya dunia. Njia za kupunguza umaskini na njaa ulimwenguni pote lazima zipatikane. Mikataba mipya kati ya mataifa itahitaji kufanyizwa.”

Mapendekezo yake ni yenye kiasi kwa wengi. Kuokoa misitu ya mvua kwahitaji kitatuzi cha tufeni pote—kama vile tu hali nyingine zinazowakabili wanadamu. Tatizo linakuwa katika “kupata mikataba kati ya mataifa” kabla msiba mkubwa wa ulimwenguni pote haujatokea na kabla madhara hayajawa yasiyoweza kurekebishwa. Kama vile Peter Raven anavyodokeza, uharibifu wa msitu wa mvua wahusiana kwa ukaribu na matatizo mengine yasiyoweza kudhibitiwa kwa urahisi, ya nchi zinazoendelea, kama vile njaa na umaskini.

Kufikia sasa, jitihada za kimataifa zilizofanywa kuelekea matatizo haya hazikufanikiwa sana. Watu fulani huuliza, Je, siku moja mataifa yataweza kushinda tofauti zao ndogo za kitaifa kwa ajili ya manufaa ya wote, au kutafuta “uzalendo mpya baina ya mataifa” ni ndoto tu?

Historia haielekei kutoa misingi kwa ajili ya matumaini mema. Hata hivyo, jambo moja hupuuzwa mara nyingi—maoni ya Muumba wa msitu wa mvua. “Inapasa kuwekwa akilini kuwa tunaharibu sehemu ya Uumbaji,” Profesa wa Harvard Edward O. Wilson, atoa hoja, “kwa njia hiyo tukinyima vizazi vijavyo kile ambacho sisi wenyewe tuliachiwa kama urithi.”

Je, Muumba wa dunia atawaruhusu wanadamu kuiharibu kazi yake kabisa? Hilo lingekuwa lisiloeleweka.a Badala ya hivyo, Biblia hutabiri kwamba Mungu ‘atawaleta kwenye uangamizi wale wanaoiangamiza dunia.’ (Ufunuo 11:18) Mungu atatekelezaje kitatuzi chake? Anaahidi kusimamisha Ufalme—ufalme wa kimbingu wa mataifa yote—ambao utatatua matatizo yote ya dunia na ambao “hautaangamizwa milele.”—Danieli 2:44.

Si kwamba tu Ufalme wa Mungu utaleta mwisho wa utumiaji mbaya wa mwanadamu kwa sayari bali pia utasimamia kurudishwa kwa urembo wa dunia wa asili. Dunia yote hatimaye itakuwa mbuga ya tufeni pote, kama vile tu Muumba wetu alivyokusudia hapo mwanzoni. (Mwanzo 1:28; 2:15; Luka 23:42, 43) Watu kila mahali “watafundishwa na BWANA,” na watajifunza kupenda na kuthamini uumbaji wake wote, kutia ndani msitu wa mvua.—Isaya 54:13.

Akielezea wakati huo wenye baraka, mtunga-zaburi aliandika: “Miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha; mbele za BWANA, kwa maana anakuja, kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake.”—Zaburi 96:12, 13.

Kwa furaha, wakati ujao wa msitu wa mvua hautegemei hangaiko—au ulafi wa mali—wa mwanadamu. Biblia hutupa sababu ya kuwa na uhakika kwamba Muumba mwenyewe ataingilia kati ili kuokoa misitu yetu ya kitropiki. Katika ulimwengu mpya ulioahidiwa na Mungu, vizazi vijavyo vitaona utukufu ulioko katika msitu wa mvua.—Ufunuo 21:1-4.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa kupendeza, wanaotetea kuhifadhiwa kwa mali ya asili ambao lengo lao ni kuokoa spishi nyingi iwezekanavyo zilizo hatarini hueleza maadili yao kuwa “kanuni ya Noa,” kwani Noa aliagizwa kuweka katika safina “kila kilicho hai chenye mwili.” (Mwanzo 6:19) “Kuendelea kuwapo [kwa spishi] katika asili kwafikiriwa kuwa na haki isiyo na lawama ya kuendelea kuwako,” abisha mwanabiolojia David Ehrenfeld.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki