Tafsiri ya Biblia ya Mapema Yadumu
Wakati wa miaka ya 1994/1995 Maktaba ya Uingereza ilionyesha chapa kamili ya mwaka wa 1526 ya tafsiri ya William Tyndale ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo iliyochapishwa alipokuwa uhamishoni katika Worms, Ujerumani. Kitabu hiki kilinunuliwa kutoka katika Chuo cha Baptisti cha Bristol Uingereza kwa karibu dola 1,600,000, kwani kilionwa kuwa nakala kamili pekee iliyodumu—sehemu kubwa ya zile nakala zilizokaribia 3,000 zilizoingizwa Uingereza kisiri zilichomwa kutokana na uchochezi wa askofu wa London. Hata hivyo, nakala nyingine iliyo kamili imepatikana katika maktaba ya Stuttgart, Ujerumani. Ikiwa bila jina la utambulishi na kuachiliwa kwa mamia ya miaka, inadumisha si jalada lake la kwanza tu bali pia ukurasa wake wenye jina ulio na thamani.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 15]
By kind permission of the Principal, Fellows and Scholars of Hertford College, Oxford
© Württ. Landesbibliothek/Fotograf: Joachim Siener