Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 11/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 11/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Upasuaji Mume wangu nami twamshukuru Yehova kutoka mioyoni mwetu kwa makala “Upasuaji Bila Kisu Kidogo cha Kupasulia.” (Februari 22, 1998) Mume wangu alikuwa amepangiwa kwenda kufanyiwa upasuaji ndani ya ubongo kwa sababu ya hitilafu ya arteriovenous malformation. Makala hiyo ilikuwa kama jibu kwa sala zetu. Mume wangu alifanyiwa upasuaji kwa njia inayotajwa katika makala hiyo, na anaendelea vizuri.

L. J., Marekani

Waandishi wa Habari wa Urusi Shukrani nyingi kwa makala “Waandishi wa Habari wa Urusi Wawasifu Mashahidi wa Yehova.” (Februari 22, 1998) Nilitaka tu mjue kwamba si mara ya kwanza kutokwa na machozi kwa kusoma mojawapo makala zenu zenye kupendeza. Inafurahisha kujua kwamba siku moja dunia yote itapendeza kama majengo mapya ya ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Solnechnoye.

I. C. S. A., Brazili

Baba Asiyeamini Abadilika Makala “Moyo Wake Uliguswa” (Februari 22, 1998) ilinikumbusha juu ya familia yangu mwenyewe. Mume wangu pia si mwamini. Makala hiyo ilinipa tumaini kwamba huenda siku moja moyo wake ukaguswa.

S. M., Marekani

Familia Yakinza Wanazi Sijapata kamwe kusoma jambo lililoonwa nzuri ajabu kuliko lile la Horst Henschel, katika makala “Nilichochewa na Uaminifu-Mshikamanifu wa Familia Yangu kwa Mungu.” (Februari 22, 1998) Ilinibidi kutua mara nyingi katikati ya mafungu ili kuzuia kulia kwangu. Baba ya Horst kwa hakika alikuwa mtu aliyevumilia chini ya msongo, nami nitathamini kielelezo chake sikuzote.

A. K., Marekani

Jambo lililoonwa la Horst Henschel lilikuwa lenye kuchochea sana. Moyo wake mkuu na upendo wake kwa Yehova ulinichochea. Siwezi kusahau maneno yaliyomtia moyo alipokuwa gerezani: “Msiwaogope waua mwili.”

J. V. S., Brazili

Nina umri wa miaka kumi, nami nilitaka kuwaambia jinsi inavyotia moyo kujua jinsi ambavyo Mashahidi wa Yehova waliishi siku hizo—jinsi ambavyo ikiwa hawangesema “Heil Hitler!” wangeweza kupoteza maisha zao. Lakini Mashahidi walidumu wakiwa imara na hawakusema hivyo.

R. B., Marekani

Fahari ya Jamii Nilifurahi kusoma makala “Vijana Huuliza . . . Namna Gani Kuonea Fahari Jamii Yako?” (Februari 22, 1998) Nimeulizwa mara nyingi, “Wewe ni wa taifa gani?” Nikishindwa kueleza juu ya nasaba ya familia yangu, ningejibu kwa mzaha, “Chotara!” Mhudumu anayesafiri alisema, “Mtu yeyote akikuuliza wewe ni nani, mwambie tu, ‘Mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova.’” Nina fahari kuwa katika tengenezo ambalo huona jamii zote kuwa sawa.

D. H., Marekani

Nina umri wa miaka 14 na ninataka kuwashukuru kwa makala hiyo. Fahari yangu ya kijamii iligeuka kuwa ubaguzi wa jamii. Makala hiyo ilinifanya nielewe kwamba machoni pa Yehova sisi sote tuko sawa.

I. P., Italia

Nilipokuwa mchanga, wengi wa wanashule wenzangu walionea fahari jamii na rangi yao, wakisema kwamba walikuwa wa ukoo wa Kihispania, ilhali nilikuwa wa kikundi kidogo. Nilianza kujihisi nikiwa mtu duni sana na kukosa kujistahi. Nyakati nyingine nimehisi, ‘naichukia rangi yangu!’ Shauri lililo katika makala hii lilinisaidia kujistahi tena na kuhisi natosheka na kile ambacho Yehova amenipa.

A. G., Filipino

Kwa kweli nilikuwa na maoni yaliyopotoka, nikifikiri kwamba watu waliozaliwa katika nchi zilizo tajiri walikuwa bora zaidi. Makala yenu ilinisaidia kuona kwamba kwa kweli kuna jamii moja tu—jamii ya kibinadamu.

L. G., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki