Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 6/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
  • Thamani ya Faragha
    Amkeni!—1998
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 6/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kimbunga Pauline Sikuzote mimi hufurahi ninapokumbushwa kwamba niko sehemu ya tengenezo linalowajali watu kikweli. Asanteni kwa ajili ya makala bora “Mambo Mawili juu ya Msiba.” (Oktoba 8, 1998) Inaridhisha kama nini kujua kwamba watu wengine wanatambua kwamba Mashahidi wa Yehova wana “utaratibu na ni wenye kufuatia haki”!

D. F. S., Brazili

Faragha Ile makala “Maoni ya Biblia: Thamani ya Faragha” (Oktoba 8, 1998) ni kana kwamba ilinihusu mimi binafsi. Faragha ni jambo muhimu kwa ukuzi wangu wa kiroho na kihisia-moyo. Hata hivyo, nitakumbuka hoja ya kwamba faragha ni “mahali penye kuthawabisha ambapo mtu aweza kupatembelea lakini ambapo ni hatari kubakia.”

L. G., Marekani

Vatikani na Yale Maangamizi Makubwa Kwa miaka mingi Mashahidi wamezuru nyumbani kwangu, na tukawa na wakati mzuri. Hata hivyo, makala “Kanisa Katoliki na Yale Maangamizi Makubwa” (Oktoba 22, 1998) iliniudhi. Papa Pius wa 12 alikuwa mtu mtakatifu ambaye alijitahidi sana kuwasaidia Wayahudi, na maelfu waliokoka kwa sababu ya jitihada zake!

J. P., Marekani

Halikuwa kusudi letu kuwaudhi wasomaji Wakatoliki bali kutoa ripoti sahihi ya ubishi juu ya hati ya Vatikani yenye kichwa “We Remember: A Reflection on the Shoah.” Taarifa zilizotolewa kwenye makala hiyo ni maoni ya wanahistoria, waandishi, na wanasheria wenye kuheshimiwa—baadhi yao wakiwa Wakatoliki. Bila shaka, fungu lolote la kuokoa watu ambalo huenda Vatikani ilitimiza linastahili pongezi. Hata hivyo, ni jambo hakika kwamba papa alishindwa kushutumu hadharani utawala wa Nazi. Kama angefanya hivyo mamilioni ya watu hawangeuawa.—Mhariri.

Kupendana Ule mfululizo “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?” (Oktoba 22, 1998) ulikuwa bora kabisa! Umenisaidia kuzuia msukumo wenye nguvu wa kusitawisha uchungu wa moyo na chuki ambayo mimi huwa nayo nyakati nyingine. Asanteni sana! Natumaini kwamba kitia-moyo ninachopokea kutoka kwa vichapo vyenu kitanisaidia kuwa mtumishi wa Yehova Mungu.

G. C., Italia

Wamishonari Jasiri Baada ya kusoma makala “Twaishi Si kwa Ajili Yetu Wenyewe Tena” (Oktoba 22, 1998), ilinilazimu kutoa shukrani kwenu kwa ajili ya habari hiyo yenye kuimarisha imani. Hapa Uingereza watu wengi hawapendi ujumbe wetu. Lakini huwezi kulinganisha hali hii na yale ambayo yaliwapata Jack na Linda Johansson. Makala hiyo iligusa sana moyo wangu na kunifanya nithamini yale niliyo nayo.

L. J., Uingereza

Mimi na mke wangu tumekuwa wahudumu wa wakati wote kwa miaka kadhaa sasa, nasi twajua kwamba kuzoea mgawo mpya si jambo rahisi. Jack na Linda Johansson walieleza waziwazi jinsi walivyohisi walipohama. Simulizi lao lilituonyesha kwamba hisia zetu ni za kawaida na kwamba tunapaswa kuendelea kumtegemea Yehova.

S. E. C., Brazili

Kufanya Ukweli Uwe Mali Yako Mwenyewe Nina umri wa miaka 12, na nilifurahia makala “Vijana Huuliza . . . Naweza Kufanyaje Ukweli Uwe Mali Yangu Mwenyewe?” (Oktoba 22, 1998) Sasa kwa kuwa shule zimefunguliwa, ni vigumu kidogo kutayarisha kwa ajili ya mikutano ya Kikristo. Lakini inanibidi ninunue wakati. Nafikiri makala hii itasaidia vijana wengi kusitawisha upendo kwa Yehova na kupenda kweli kabisa.

C. S., Ureno

Mwaka mmoja uliopita nilikuwa nikifikiria maswali yayo hayo juu ya kweli. Sikuwa na uhakika iwapo nilipenda kweli au nilikuwa tu nikiifuata  kwa sababu ya familia yangu. Ndipo nilipofanya kama mlivyohimiza—nilijithibitishia kwa kufanya utafiti wa Biblia. Nina furaha sasa kusema kwamba kweli ni mali yangu. Ninatazamia kwa hamu kuwa mweneza-evanjeli wa wakati wote!

H. N., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki