Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 3/8 uku. 31
  • Wafanya-amani au Wachochea-vita?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wafanya-amani au Wachochea-vita?
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Baraza la Makanisa Ulimwenguni Ushirikiano au Mvurugo?
    Amkeni!—1992
  • Kuna Tumaini Gani kwa Mwisho wa Vita?
    Amkeni!—1993
  • Jumuiya ya Wakristo Imesaliti Mungu na Biblia
    Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?
  • Ushindi wa Kimungu—Maana Yake kwa Wanadamu Wanaotaabika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 3/8 uku. 31

Wafanya-amani au Wachochea-vita?

“MKRISTO hapaswi kushiriki katika vita.” Taarifa hiyo inaeleza kwa ufupi maoni ya Wakristo wa mapema juu ya vita, Thoko na Malusi Mpulwana wasema katika gazeti Echoes, linalochapishwa na Baraza la Makanisa ya Ulimwengu (WCC). Wao waendelea kusema kwamba ni “baada tu ya Kanisa la Kikristo kuungana na wenye madaraka kisiasa” ndipo kanisa lilipoanza kupendelea “kukubali umuhimu wa vita.” Tokeo limekuwa nini? Hali ya kwamba Jumuiya ya Wakristo imeunga mkono vita kwa muda mrefu imekuwa wazi sana hivi kwamba baada ya vita ya ulimwengu ya pili, United ­Church of ­Christ la Japani liliona uhitaji wa kutoa rasmi “Ungamo la Fungu Letu Katika Vita ya Ulimwengu ya Pili.”

Leo, miaka 50 baada ya vita hiyo, sifa ya Jumuiya ya Wakristo ya kuwa wapiganaji haijabadilika. Dakt. Roger Williamson, anayefanyia kazi Kanisa la Uingereza akiri hivi: “Sisi Wakristo tukiulizwa kama tumekataa katakata mambo ya vita na kukubali kabisa upendo wa Kristo, ni wazi kwamba . . . bado tuna mengi ya kuungama.” Ijapokuwa WCC lilitangaza katika mwaka wa 1948 kwamba “vita ikiwa njia ya kusuluhisha mabishano haipatani na fundisho na kielelezo cha Bwana wetu Yesu Kristo,” makanisa ya Jumuiya ya Wakristo, aonelea Williamson, yametokeza “ushupavu, kutovumiliana, kuzuia uhuru wa kibinadamu na kuzidisha vita hata zaidi.” Si ajabu kwamba yeye amalizia kwa kusema “mara nyingi dini . . . huzidisha vita badala ya kuvikomesha.”

Ile vita iliyosambaratisha ile iliyokuwa Yugoslavia ni mfano unaofaa. Ijapokuwa udhalimu na ukatili ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, imekuwa vigumu sana kwa makanisa kupinga kwa kauli moja vita katika nchi hiyo. Kwa nini? Dakt. Williamson asema kuwa licha ya ule unaodhaniwa kuwa muungano wa Kikristo, hata makasisi Waserbia na Wakroatia wamegawanyika tu kama wanasiasa wa nchi zao. Huko na kwingineko makasisi wa Jumuiya ya Wakristo, wawe Wakatoliki, Waothodoksi, au Waprotestanti, hawawi wafanya-amani bali “wenye kuunga mkono jeshi la upande wao.” Ingawa makanisa zaidi ya 300 ni washiriki wa WCC, Dakt. Williamson akiri kwamba “kwa kushangaza ni vigumu kupata mifano ya makanisa . . . yanayoleta amani.”

Ndiyo, ni vigumu. Lakini tofauti na makanisa washiriki wa WCC, ambayo husema tu juu ya mapatano, kunayo dini moja ambayo tayari imefaulu kuwapatanisha wale waliokuwa washiriki wa dini tofauti-tofauti na kuwasaidia wawe Wakristo wa kweli. Leo, wakisukumwa na upendo wao kwa Mungu na tamaa yao ya ‘kufuatia amani pamoja na watu wote,’ katika nchi 233 Mashahidi wa Yehova zaidi ya milioni 5.8 wanakataa kushiriki katika vita baina ya mataifa—viwe vinapiganwa katika Asia, Amerika ya Latini, Ireland Kaskazini, Mashariki ya Kati, Rwanda, au katika ile iliyokuwa Yugoslavia. (Waebrania 12:14; Mathayo 22:36-38) Badala yake, wao wanautimiza unabii wa Biblia kwa ‘kufua panga zao ziwe majembe’ na ‘kutojifunza vita tena kamwe.’—Mika 4:3.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Baadhi ya Mashahidi wa Yehova katika Afrika wamepigwa vibaya sana kwa sababu ya kutokuwamo kwao au wamekuwa wakimbizi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki