Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 8/8 uku. 31
  • Kushuka kwa Dini Uingereza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kushuka kwa Dini Uingereza
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Kuagizwa Rasmi kwa Wanawake Kwaghadhibisha Makasisi wa Anglikana
    Amkeni!—1995
  • Kanisa—Mabadiliko na Mvurugo
    Amkeni!—1993
  • Kwa Nini Kanisa Linapoteza Uvutano?
    Amkeni!—1996
Amkeni!—1999
g99 8/8 uku. 31

Kushuka kwa Dini Uingereza

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UINGERESA

GAZETI The Sunday Times la London liliripoti kwamba Waingereza 1,500 wanaacha makanisa mashuhuri kila juma. Kanisa Katoliki limepoteza wahudhuriaji wapatao 600,000 tangu 1980, na Kanisa la Uingereza—ambalo lingali linapoteza watu 600 kila juma—lina watu wasiozidi milioni moja katika ibada zake, hudhurio ambalo halifikii nusu ya wahudhuriaji wa miaka 50 iliyopita. Baada ya uamuzi wa Mkutano Mkuu kuweka rasmi wanawake kuwa makasisi, karibu makasisi 500 wa Kanisa la Uingereza wameacha kanisa.

Wengi ambao wameacha kanisa mara nyingi hukasirika na kutamauka kwamba hakuna mtu aliyejaribu kuwazuia wasiondoke au kuwafuata waone jambo linaloweza kufanywa ili kuwasaidia walipoondoka, likaripoti gazeti The Times. Wengine “walisema kwamba Kanisa limeshindwa kufanya mapatano nao,” gazeti hilo likasema.

Jamii ya Uingereza inaishi kwa “ugavi wa kiroho na rasilimali zinazofifia,” akasisitiza kadinali Basil Hume, askofu mkuu wa Westminster wa Kanisa Katoliki. Ni nini ambacho kimesababisha upungufu huu? “Njaa kuu ya Neno la Mungu,” ndicho kilichokuwa kichwa kikuu cha gazeti Catholic Herald. Lilisema hivi: “Kwenye misa tunasomewa madondoo kutoka katika Agano la Kale na Jipya, lakini ni nadra sana muktadha wake kutolewa. . . . Maisha ya watakatifu na vitabu mbalimbali vya mambo ya kiroho ni vizuri, lakini havitoshi kutumiwa kuyaelewa Maandiko.” Makala hiyo ilimalizia kwa kusema kwamba “maelezo ya kisasa ya Biblia yenye mradi wa kuchunga kundi” yakosekana.

Katika barua moja kwa Boston Target la Lincolnshire, msomaji mmoja alisema hivi: “Watu wanapoteza imani katika dini . . . Wahudumu hawa wa kanisa wanafanya nini siku yote? Hawatoki kama Kristo alivyofanya ili kukutana na watu . . . Dini tu ambayo yaonekana kuwa yenye kujali ni Mashahidi wa Yehova, ambao huendea watu na kujihusisha kikweli katika kuhubiri kweli—wanakualika kwenye ibada yao, wao huongea juu ya mazingira na hata kuchukua hatua. Mimi si mmoja wa MY [Mashahidi wa Yehova], lakini nastahi watu hawa na kuwasikiliza.”

Je, umepata kuhudhuria mikutano kwenye Jumba la Ufalme la mahali penu? Huko utapata mafundisho yenye kuchangamsha na yenye kusaidia. Je, ungependa kujibiwa maswali yako ya Biblia? Mwaka jana, katika nchi 233, Mashahidi wa Yehova walitoa zaidi ya muda wa saa bilioni moja za wakati wao bila malipo kusaidia watu waielewe Biblia, wakiongoza mafunzo ya Biblia ya nyumbani zaidi ya milioni nne. Mashahidi wa Yehova huiona kazi hii ya elimu ya Biblia kuwa ya maana zaidi kufanyika wakati huu. Twakualika uchunguze sababu hiyo.—Mathayo 24:14; 28:19, 20.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki