Yerusalemu Na Hekalu La Siku Za Yesu
MUDA mfupi baada ya Yesu kuzaliwa, Yosefu na Maria walimpeleka Yerusalemu, jiji ambalo Baba yake wa kimbingu alikuwa ameweka jina Lake. (Lu 2:22-39) Alipokuwa na umri wa miaka 12 Yesu alienda huko tena kwa ajili ya Pasaka. Walimu waliokuwa hekaluni walishangazwa na uelewevu wake. (Lu 2:41-51) Ujenzi wa hekalu hilo ambao ulikuwa sehemu ya programu ya ujenzi ya Herode Mkuu ulichukua zaidi ya “miaka 46.”—Yoh 2:20.
Wakati wa huduma yake, Yesu alihudhuria sikukuu huko Yerusalemu, ambapo mara nyingi alifundisha umati. Mara mbili aliwafukuza wabadili fedha na wafanyabiashara kutoka kwenye ua wa hekalu.—Mt 21:12; Yoh 2:13-16.
Kwenye dimbwi la Bethzatha lililokuwa kaskazini ya hekalu hilo, Yesu alimponya mtu aliyekuwa ameugua kwa miaka 38. Mwana wa Mungu alimponya kipofu na kumwambia aende akanawe katika dimbwi la Siloamu lililokuwa kusini mwa jiji hilo.—Yoh 5:1-15; 9:1, 7, 11.
Mara kwa mara Yesu aliwatembelea marafiki wake Lazaro, Maria, na Martha huko Bethania, jiji lililokuwa “karibu kilometa tatu” mashariki ya Yerusalemu. (Yoh 11:1, 18, kielezi-chini, New World Translation of the Holy Scriptures—With References; 12:1-11; Lu 10:38-42; 19:29; ona “Eneo la Yerusalemu,” ukurasa wa 18.) Siku chache kabla ya kifo chake, Yesu alienda Yerusalemu akipitia Mlima wa Mizeituni. Wazia Yesu akisimama na kutazama upande wa magharibi mahali ambapo jiji hilo lilikuwa na kulililia. (Lu 19:37-44) Yesu aliliona jiji kama unavyoliona katika picha iliyo upande wa juu wa ukurasa unaofuata. Kisha aliingia Yerusalemu akiwa juu ya mwana-punda, labda kwa kupitia mojawapo ya malango yaliyokuwa mashariki mwa jiji hilo. Umati wa watu walimkaribisha kwa shangwe akiwa Mfalme wa Israeli wa wakati ujao.—Mt 21:9-12.
Mambo muhimu yaliyotendeka kabla ya kifo cha Yesu yalitukia Yerusalemu au karibu na jiji hilo: bustani ya Gethsemane, ambapo Yesu alisali; jumba la Sanhedrini; nyumba ya Kayafa; jumba la Gavana Pilato na, hatimaye Golgotha.—Mk 14:32, 53–15:1, 16, 22; Yoh 18:1, 13, 24, 28.
Baada ya kufufuliwa, Yesu alionekana Yerusalemu na maeneo yaliyokuwa karibu na hapo. (Lu 24:1-49) Kisha akapaa mbinguni akiwa kwenye Mlima wa Mizeituni.—Mdo 1:6-12.
[Mchoro katika ukurasa wa 31]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Yerusalemu/Hekalu la Herodi
Sehemu Za Hekalu
1. Patakatifu Zaidi
2. Patakatifu
3. Madhabahu ya Toleo la Kuteketezwa
4. Bahari ya Kuyeyushwa
5. Ua wa Makuhani
6. Ua wa Israeli
7. Ua wa Wanawake
8. Ua wa Mataifa
9. Kizuizi (Soreg)
10. Nguzo za Kifalme
11. Nguzo za Sulemani
HEKALU
Lango
Ua wa Makuhani
Lango
Patakatifu Madhabahu
Zaidi Patakatifu ya Toleo Ua wa Ua wa
Kuteketezwa Israeli Wanawake
Bahari
Kuyeyushwa
Lango Nguzo za
Kizuizi (Soreg) Sulemani
Ua wa Mataifa
Mlango
Nguzo za Kifalme
Malango
Mnara wa Antonia
Daraja
Jumba la Sanhedrini?
BONDE LA TIROPOA
Dimbwi la Siloamu
Mfereji
Nyumba ya Kayafa?
Jumba la Gavana
Golgotha?
Golgotha?
Dimbwi la Bethzatha
Bustani ya Gethsemane?
MLIMA WA MIZEITUNI
BONDE LA KIDRONI
En-rogeli
Chemchemi ya Maji ya Gihoni
BONDE LA HINOMU (GEHENA)
[Picha katika ukurasa wa 30]
Picha hii inaonyesha upande wa mashariki wa Yerusalemu la kisasa: (A) eneo la hekalu, (B) bustani ya Gethsemane, (C) Mlima wa Mizeituni, (D) nyika ya Yuda, (E) Bahari ya Chumvi
[Picha katika ukurasa wa 31]
Picha hii imepigwa kutoka upande wa magharibi wa Mlima wa Mizeituni katika siku za Yesu