Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 11/1 kur. 498-501
  • Walivutwa na Dhamiri ya Kimungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Walivutwa na Dhamiri ya Kimungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • DHAMIRI NI NINI?
  • WEPESI KUZIONA SHERIA ZA MUNGU ZA ADILI
  • NIA YA KUPATA HASARA
  • WAAMINIFU KATIKA MAMBO YOTE
  • Je! Wewe Unaongozwa na Dhamiri Nyepesi ya Kikristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Sauti ya Dhamiri Iliyomo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Kuendelea Kuwa na Dhamiri Njema
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
  • Dhamiri Njema Mbele za Mungu
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 11/1 kur. 498-501

Walivutwa na Dhamiri ya Kimungu

WAKATI fulani uliopita mmojawapo wa mashahidi wa Yehova katika Palm Springs, California, alitembelewa na ndugu yake na mchumba wake. Jioni ilipokaribia, Shahidi angeweza kuona kwamba ndugu yake asiye Shahidi alikuwa akipanga alale kwake usiku huo, na lulala pamoja na mchumba wake. Je! wewe ungalifanya nini?

Likuwa hali ngumu. Lakini Shahidi alimwambia ndugu yake kwamba asingeweza kulala na mwanamke ambaye hawajaoana naye katika nyumba yake. Hii ilimshangaza ndugu yule. Aliudhika sana, akiona yule Shahidi alikuwa mjinga sana. Ingawaje, yeye na mchumba wake walikuwa wenye umri wa kutosha kuweza kuwa na wajukuu, nao wangeoana zikiisha kupita siku chache.

Kwa nini Shahidi alichukua msimamo huo, akijua kwamba hii ingeleta shida na udhia? Dhamiri yake ilitiwa ndani.

DHAMIRI NI NINI?

Je! wewe umepata kusema: “Nilijua moyoni mwangu haikuwa sawa”? Au, “Siwezi kufanya unavyotaka, maana kitu fulani ndani yangu chasema ni kosa”?

Hiyo ni dhamiri yake iliyokuwa ikizungumza. Dhamiri ni ule ufahamu wa ndani au maono tuliyo nayo ya yaliyo haki na makosa. Mungu aliwaumba wanadamu wawili wa kwanza wakiwa na uwezo huu wa dhamiri, nasi sote tumeurithi kutoka kwao. Ni hekima kutotenda kwa makusudi mambo yaliyo tofauti na yanayosemwa na dhamiri iliyozoezwa sawasawa. Kwa sababu gani?

Kwa maana maono yetu ya adili au dhamiri yaweza, kama matokeo, kudhuriwa au hata kuharibiwa. Yaweza kuunguzwa “kama vile kwa chuma cha kupigia chapa.” (1 Tim. 4:2, NW) Hili litukiapo, maono yetu ya ndani ya yaliyo haki na makosa yanaacha kutenda kazi sawasawa. Lakini twaweza kuzuia hili lisitukie.

WEPESI KUZIONA SHERIA ZA MUNGU ZA ADILI

Yehova Mungu amefanya mpango wa kuimarisha dhamiri yetu kwa kutupa sisi sheria za haki na kanuni katika Biblia, na kwa ajili ya mpango huu tunayo sababu nzuri ya kushukuru. Twaweza kujifunza hizi, na dhamiri yetu ndipo inapoweza kuzitumia kwa hali mbalimbali zinazotokea. Kwa njia hii tutavutwa na dhamiri yetu kufanya yampendezayo Mungu.

Mtu anapojifunza Biblia, anafahamu kwamba sheria ya Mungu inakataza uasherati na uzinzi. (Ebr. 13:4; 1 Kor. 6:9, 10) Shahidi aliyetajwa mapema alikuwa mwepesi wa kuiona sheria hiyo. Dhamiri yake haikumruhusu ashiriki katika uasherati kwa njia yo yote​—kwa kweli, kuuachilia kwa kuuruhusu utendeke nyumbani mwake. Hivyo ndivyo watu wanavyoona wanaokuja kuipenda kweli sheria ya Mungu.

Miaka michache iliyopita mwanamke mmoja katika Honduras, Amerika ya Kati, aliyekuwa na nyumba ya kukodisha alianza kujifunza Biblia na mashahidi wa Yehova. Nyumaye, alisema kwamba dhamiri yake ilikuwa ikimsumbua. Kwa nini? Kwa sababu kwa kawaida wanaume walikuwa wakiitumia nyumba yake kama mahali pa kuleta malaya. Kama matokeo ya upendo wake kwa sheria ya Mungu alioupata majuzi, mwanamke huyu aliona uchungu juu ya kuiruhusu nyumba yake itumiwe kwa makusudi ya ufisadi.

Kwa hiyo alianza kukataa asiruhusu ye yote alale ndani yake usiku ikiwa kusudi lake lilikuwa kufanya ufisadi. Katika kila chumba aliweka ishara ndogo zikisema: “Bwana, tafadhali shirikiana na hii Nyumba ya Jamaa ya Kukodi. Usilete wanawake wasio na adabu. Asante.” Mabwana waliokuwa wakija hapo kwanza wakaacha. Lakini kupoteza biashara kulikuwa kwa muda tu; karibuni alipata hesabu kubwa ya jamaa zenye kuheshimika.

Hata hivyo, namna gani ikiwa umeajiriwa mahali ambapo kwa kawaida panatumiwa kwa makusudi ya ufisadi? Bila shaka, ulimwenguni uasherati na uzinzi yameenea pote, nayo Maandiko yaonyesha kwamba kuacha kujichangamanisha kabisa na waasherati ni jambo lisilowezekana. (1 Kor. 5:9, 10) Lakini namna gani ikiwa ufisadi unaonekana wazi kazini pa mtu, unakuwa hata mbaya sana, naye mtu anaona kwamba dhamiri yake na hali ya kiroho yanahatirishwa?

Nyakati kama hizo mashahidi wa Yehova waliacha kazi zao na kutafuta nyingine. Katika mwezi wa Aprili 1972, wanawake watatu walianza kufanya kazi kama watumishi katika hoteli moja iliyokuwa imefunguliwa majuzi katika Oakford, Pennsylvania. Nyumaye, waliona kwamba wanaume wale wale walikuwa wakileta wanawake mbalimbali kwenye hoteli kwa kawaida. “Dhamiri zetu zilitusumbua,” asema mmojawapo wa Mashahidi hao. Kwa hiyo wote walipaacha mahali hapo pa kazi.

Je! wewe mwenyewe wazionaje sheria za Mungu za adili? Je! dhamiri yako ni yenye wepesi wa kadiri gani juu ya mambo hayo?

NIA YA KUPATA HASARA

Je! wewe ungekuwa na nia ya kupata hasara ya kimwili ili uendelee kuwa na dhamiri safi? Mchezaji mmoja kijana wa sinema na televisheni alikuwa na nia hii.

Mwishowe aliiacha kazi yake nyuma ya kuwa mmoja wa mashahidi wa Yehova. Sehemu za kufanya mchezo wa sinema zilimhitaji akumbatiane na wanaume asiooana nao na kuwabusu. “Nisingeweza kuendelea kufanya hivi,” alisema. “Ningewezaje kufundisha wengine kanuni zilizo bora za Neno la Mungu na hali nionekane katika kitambaa cha sinema nikifanyia upendo wanaume wasio mume wangu?”

Mnakili mmoja wa afisi ya utangazaji katika New York alikataa kufanya kazi ya utangazaji wa sigareti. Halafu sigara za mfano zikaletwa, naye akaambiwa aandike tangazo la kusisimua wanawake wazivute. Lakini yeye akakataa tena kufanya hivyo. “Dhamiri yangu haitaniruhusu kuwa na ushirika wo wote katika kutangaza mazao yenye kudhuru afya,” akaeleza, “hata iwapo kukataa huku kutafanya nifutwe kazi.”

Katika hali fulani iliyo tofauti kidogo na hii, mwanamke mwuzaji wa duka kubwa katika mji wa New York alikataa kubandika shada la maua la Krismas katika vazi lake, lililorembeshwa na ishara za sikukuu. Msimamizi wa duka akamwambia kwamba asipolibandika vazini angehakikisha amefutwa kazi. Yule mwanamke mwuzaji alikwenda afisini na kueleza kwa nini dhamiri yake isingeweza kumruhusu abandike shada hilo la maua, na hivyo ashiriki katika roho ya sikukuu yenye alama za kipagani. Msimamizi alielewa, naye mwanamke huyu hakufutwa kazi.

Kufanya yampendezayo Mungu kuna muhimu gani kwako? Je! wewe unavutwa na dhamiri ya kimungu?

WAAMINIFU KATIKA MAMBO YOTE

Wakristo wa kweli wanajisikia kama alivyojisikia mtume Paulo, aliyesema: “Twaamini tunayo dhamiri ya uaminifu, kwa maana twataka tujiongoze kwa uaminifu katika mambo yote.” (Ebr. 13:18, NW) Je! dhamiri yako inakuvuta ujiongoze kwa uaminifu?

Miaka michache iliyopita kiongozi mmoja wa afisi kubwa ya utangazaji ya New York alikuja kuwa mmoja wa mashahidi wa Yehova. Hapo kwanza alikuwa ameongeza hesabu ya gharama zake, akiandika mambo ambayo hayakuwa gharama hasa za kazi. “Haya ni mazoea ya kawaida, karibu hata yanayotazamiwa,” anasema. “Lakini nilipokwisha kujifunza kanuni za Biblia dhamiri yangu isingeweza kuniruhusu nifanye hivyo tena. Kwa hiyo, hii imemaanisha kukata mshahara kwa hiari,” anaeleza. Je! wewe ungelionaje jambo hilo?

Nyakati nyingine mikazo ya kuwa mdanganyifu ni yenye nguvu. Shahidi msichana mwenye umri wa miaka 27 alianza kufanya kazi mapema mwaka uliopita katika afisi ya bima ya wakili wa New York Life Insurance Company. Mwishoni mwa mwezi wa kwanza wa kuajiriwa alipewa karatasi atie sahihi ambayo ilionyesha mshahara wake wa mwezi. Lakini tarakimu yenyewe ilikuwa na kiasi cha 25 kwa mia zaidi ya mshahara alioupokea! Alishangaa.

Lakini, karibuni alifahamu kwamba tajiri wake alipata malipo ya gharama za ukarani. Hivyo kama mshahara ungeonyeshwa mwingi zaidi tajiri wake angejipatia fedha zaidi. Angefanyaje? Kutia sahihi katika karatasi ile kungekuwa udanganyifu; kungeichafua dhamiri yake iliyozoezwa na Biblia. Na hali kama asingetia sahihi, angeweza kuipoteza kazi yake, ambayo aliihitaji sana aweze kujisaidia katika huduma ya Kikristo. Kama ingekuwa wewe ungefanyaje?

Yule msichana alijipa moyo, akamfikia tajiri wake, na kusema: “Bwana, mimi siwezi kuitia karatasi hii sahihi hata kidogo.”

“Kwa nini sivyo?” akataka kujua.

“Si jambo la uaminifu hata kidogo. Mimi sikupata fedha ya kiasi hicho,” msichana akajibu.

“Oh, lakini haya ndiyo mazoea ya kawaida ya biashara. Kila mtu anafanya hivyo,” akadai.

“Mimi sina jingine la kufanya. Siwezi kutia sahihi hata kidogo,” msichana akajibu.

Mwanamume yule alikasirika sana, akimdharau msichana yule kwa sababu ya msimamo wake. Lakini aliegemea kiti chake kwa muda mrefu, kwa wazi akiwaza sana. Mwishowe akasema: “Umesema kweli. Umesema kweli. Tutafanya ifaavyo,” akasema.

Mazoea mengine ya kawaida ni ya wafanya biashara wa motokaa kurudisha nyuma vyombo vinavyopima jumla ya maili zilizosafiriwa ili vionyeshe maili chache zaidi kuliko zilizosafiriwa. Lakini, wakati mmoja wa mashahidi wa Yehova katika Albany, Georgia, alipoambiwa na tajiri wake afanye hivi, dhamiri yake haikumruhusu. Alifutwa kazi, lakini aliendelea kuwa na dhamiri njema. Je! kuendelea kuwa na dhamiri safi kungeweza kuwa na muhimu huo kwako?

Udanganyifu ni wa kawaida vile vile katika kazi ya kutengeneza motokaa. Alipoajiriwa karibuni kama Msimamizi wa Utengenezaji (“Service Manager”) na banda moja la motokaa katika Ogden, Utah, ilimpasa mmoja wa mashahidi wa Yehova kufanya mazoea hayo. Kama anavyoeleza: “Fundi wa motokaa alikuwa akifanya kazi ya kupisha umeme na, ili apate fedha zaidi katika kazi hii, alitoza fedha ya kazi ya ziada. Nikamwuliza sababu ya kufanya hivyo, lakini yeye akasema hakuna mtu atakayeiona tofauti hiyo nayo kampuni itafaidika. Mimi nilimwambia nisingeweza kuvumilia udanganyifu huo.

“Fundi yule alifadhaika na kwa hiyo akamfikia mwenyewe na kusimulia kilichotukia. Niliambiwa niende afisini nami nikahojiwa habari za shauri hili mbele ya fundi yule. Nikamwambia mwenyewe mimi nisingeshiriki katika matendo hayo na kwamba, kama mtu huyo anaweza kuiba kwa ajili ya kampani, vile vile aweza kuiba kutoka kwayo. Mwenyewe alichekelea na kusema, ‘Twaufurahia uaminifu wako na kanuni bora. Ndiyo sababu tulikutaka wewe ufanye kazi hii.’”

Ni namna gani ya dhamiri uliyo nayo? Je! unasukumwa na dhamiri yenye wepesi wa kuyakumbuka mafundisho ya Neno la Mungu? Ikiwa ndivyo, hutazoezwa na maono ya hatia, bali utafurahia uradhi wa kweli na amani ya akili. Sikuzote utaongozwa kufanya yampendezayo Mungu. Mwishowe hii itamaanisha baraka ya Mungu kwako ya uzima usiokoma katika taratibu yake mpya ya mambo iliyo ya haki.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki