Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 8/1 kur. 339-341
  • Kuongezeka kwa Uasi—kwa Sababu Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuongezeka kwa Uasi—kwa Sababu Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • N’NINl KINACHOTUKIA HASA?
  • SABABU? SABABU? SABABU?
  • LAWAMA YA MAKANISA
  • Kristo Aliuchukia Ukosefu wa Kufuata Sheria —Je! Wewe Wauchukia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Uhalifu Unaongezeka Ulimwenguni Pote—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
  • Kifo cha Mungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
  • Ongezeko la Kutokutii Sheria—Ni Ishara ya Mwisho wa Ulimwengu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 8/1 kur. 339-341

Kuongezeka kwa Uasi​—kwa Sababu Gani?

YESU KRISTO, Mwana wa Mungu, alitoa unabii wenye habari nyingi ajabu ambao kwao tungeweza kuujua wakati ambapo taratibu mbovu ya mambo iliyoitawala dunia hii kwa muda mrefu ingekomeshwa. Ukijulikana kama “ishara” ya kuwapo kwa Kristo, unabii huu unayo mambo mengi, mojawapo likiwa ni “kuongezeka maasi.”​—Mt. 24:12.

Je! maelekeo ya karibuni ya uasi yanalingana na masimulizi yake? Je! kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba wakati umefika ambapo Mungu atajiingiza katika mambo ya wanadamu na kufanya haki ienee pote?

N’NINl KINACHOTUKIA HASA?

Kuongezeka kwa uasi kunapotajwa, huenda watu wengine wakakumbuka habari zinazosema kwamba maelekeo haya yanapungua na huenda hata yakawa yameshindwa. Kulingana na habari za karibuni, mnamo mwaka wa 1972 kulikuwako upunguo wa karibu kiasi cha 2 kwa mia katika uhalifu mbaya sana ulioripotiwa katika United States, upunguo wa kwanza katika miaka kumi na saba. Lakini kwa kweli habari hizi hazitoi sababu kubwa ya kufarijika. Kwa sababu gani? Kwa maana habari zinaonyesha kwamba uhalifu wa kutumia nguvu zaidi uliongezeka sana. Hivyo mnamo miezi ile ile minane, uuaji uliongezeka kwa kiasi cha 9 kwa mia, mashambulio yalizidishwa kiasi cha 8 kwa mia na kunajisi kiasi cha 8 kwa mia vile vile. Nayo hii ndiyo namna ya uasi ambayo watu wanaogopa sana, kwa sababu ya ubaya wake. Zaidi ya hayo “upunguo” wa uhalifu usioonwa kama mbaya sana si lazima uwe haukutokea kwa sababu uhalifu mchache ulifanywa. Bali, wakuu wengine wanaamini kwamba ni kwa sababu uhalifu mchache ndio uliripotiwa.

Kwamba uhalifu ungali ukiongezeka ni wazi kwa namna ambavyo umeyageuza maisha ya kila siku. Mtaalamu mmoja wa mambo ya akili wa California University majuzi alisema hivi: “Kwanza kituo cha petroli kilikuwa hakikubali fedha baada ya saa nne. Halafu madereva wa mabas wakaacha kuvunja fedha wakati wo wote. Kampani za motokaa za kukodi zikaweka kioo kisichopenywa na risasi [kati ya madereva na abiria wao] . . . Vyombo vya nyumbani vya ulinzi vinauzwa sana. Kuna vidude vya kubonyeza vya kuitia mapolisi katika kituo chao, madirisha yenye nyuzi za kengele za hatari na vyombo vya kupima na kujua upande ambao kitu kinatoka; maendeleo ya kisasa ya mambo ya nyumba yanajivunia kuwa na walinzi wanaofanya kazi siku nzima. . . . Kuna kamera za televisheni kila mahali,” za kuwaona wavunja maduka, wenye kulazimisha matumizi ya dawa za kulevya, na wanyang’anyi wa benki. Je! hiyo yasikika kwako kana kwamba uhalifu unapungua?

Na si hayo tu. Namna gani juu ya vyombo vilivyomo katika gari lako vya kuzuia lisiibwe? kufuli nyumbani pako? Hofu inayokuzuia usifurahi unapokuwa katika bustani nzuri? hofu inayokuzuia usiende kutembea jioni ukiwa peke yako?

Uhalifu umeenea pote​—katika biashara, serikalini, barabarani, shuleni na, mara nyingi sana, unaingia nyumbani. Haupatikani katika mataifa machache tu; yote yanapatwa nao, tena vibaya sana. Iwapo matukio ya siku zetu hayatimizi “ishara” aliyoitoa Yesu, n’nini zaidi kinachohitajiwa?

SABABU? SABABU? SABABU?

“Lakini kwa sababu gani uasi unaongezeka?” Hilo ndilo ulizo linaloulizwa kila mahali.

Bila shaka mambo mengi yanashiriki kuuleta. Wengine wanaulaumu mpango wa kisasa wa magereza, ambao mara nyingi unaelekea kuwashupaza wahalifu mahali pa kuwageuza. Wengine wanalaumu mahakimu, wakisema kwamba wengi wao ni wenye huruma kupita kadiri.

Kati ya mambo mengine yanayoshiriki katika kuongezeka kwa uasi ni upotovu serikalina. Vile vile, sinema na vipindi vya televisheni vinatia moyo uasi kwa kuwaonyesha wahalifu kama mashujaa na watu wengine wasio na adabu.

Walakini, yawezekana kwamba mambo haya yote ni vyanzo tu vya ugumu wenyewe, na kwamba sababu za kuongezeka kwa uasi ni zenye nguvu zaidi? Mchunguzi wa uhalifu wa United States Senate anataja sababu tatu kubwa: nyumba, shule na makanisa.

Biblia inachunguza hata zaidi. Inamwonyesha Shetani Ibilisi kama mkosaji aliye mkuu. Huenda wengine wakadhihaki. Lakini maelezo wanayoyatoa wao ya hali zilizopo hayatoshi kueleza kuzuka kwa uasi kunakofadhaisha. Kwa upande mwingine, zamani sana Biblia ilikionyesha kizazi hiki kama ambacho kingepatwa na mambo haya.a Ilisema kweli. Vile vile inamwonyesha yeye aliye na daraka hasa la ole iliyoongezeka kuwa ni Shetani Ibilisi, ambaye ameghadhibika kwa maana anajua wakati wake ni mfupi. Kuna sababu nyingi za kuamini yale ambayo inayasema juu ya jambo hili.​—Ufu. 12:9-12.

LAWAMA YA MAKANISA

Mambo haya yatukiapo, yawezekana watu wengine wangalitazamia makanisa kuwa nguvu ambayo ingezuia maelekeo ya uasi. Lakini mambo yametukia vingine kabisa.

Alipohojiwa juu ya hali ya uhalifu, Senator John McClellan alisema hivi: “Kulingana na uamuzi wangu, makanisa mengine hayataki tena kanuni ya juu sana ya ukamilifu na uadilifu leo. Hawana mawazo yale yale ya maisha ya Kikristo yaliyotiiwa na kuzoewa wakati uliopita.” Na alipoulizwa kama hii ilikuwa sababu ya kuongezeka kwa uasi, akajibu: “Bila shaka.”​—U.S. News & World Report.

Walakini, maongozi hayakuwa yasiyo na matokeo. Katika visa vilivyotangazwa sana viongozi wa kidini wameweka mfano wenye kupotosha kwa wengine. Hivyo, mke wa marehemu Paul Tillich, katika habari alizoziandika juu ya maisha yake na mwanadini huyu wa Kiprotestanti ajulikanaye sana, anasimulia uzinzi mwingi alioufanya na wanawake wengine. Na hali alipendwa katika mambo ya dini.

Viongozi wa kidini wamevunja heshima ya kanuni za juu za uadilifu zilizoandikwa katika Biblia, hadharani, katika jukwaa zao na katika makala zilizoandikwa. Namna gani hivyo? Kwa maana wao wanazisadiki habari za Biblia za uumbaji kama hadithi ya uongo, habari za Gharika na za uharibifu wa Sodoma na Gomora, huku wakikubali mageuzi (“evolution”), ambayo hayahusiki hata kidogo na uadilifu. Na, kwa wazi, wakati watu wanapokuja kuwa na maoni ya kwamba sehemu moja ya Biblia ni hadithi ya uongo, je! watazionaje sehemu zilizobakia kwa uzito?

Mambo haya ni ya maana, hasa kwa sababu ya uhakika wa kwamba, Yesu Kristo alifungamanisha utendaji wa “manabii wa uongo” na “kuongezeka maasi” katika unabii wake wa siku zetu. (Mt. 24:11, 12) Kwa kuacha kiburi kiwafanye watangulize maoni yao wenyewe mbele ya Neno la Mungu, wanajiacha watumiwe na Ibilisi, na hivyo wanashiriki kuleta hali zenye magumu juu ya wanadamu.

Vile vile viongozi wa kidini wameshiriki kuongezea uasi kwa kukataa kwao mafundisho ya ufalme wa Mungu na kupendelea “injili ya kijamii.” Linalopendeza ni kwamba, mwandikaji ajulikanaye sana H. G. Wells aliuona uhakika huu: “Wa ajabu ni umuhimu mwingi alioutoa Yesu kwa fundisho la alichokiita Ufalme wa Mbinguni, na uhafifu wake katika utaratibu na mafundisho ya makanisa yaliyo mengi ya Kikristo.”​—The Outline of History.

Kwa kuwa hawautumaini ufalme wa Mungu ulete hali ya uadilifu na haki duniani, viongozi wa kidini, wa Katoliki na wa Kiprotestanti vile vile, wamejitia katika siasa na wakajiona huru kufanya jeuri mara kwa mara na kusaidia wengine wafanye matendo ya jeuri kwa kusema kwamba mwishowe matokeo yatakuwa mazuri. Lakini je! makosa mawili yanafanya jambo liwe la haki? Yesu aliwaonya wafuasi wake wasikimbilie jeuri naye akawatangaza kuwa heri wale wanaofuatia amani.​—Mt. 5:9, NW; 26:52.

Je! kuna sababu nyingine ya umwagaji wa damu katika Ireland isipokuwa kwa sababu ya dini kuchangamana na siasa? Na mmojawapo wa mifano ya karibuni zaidi u juu ya viongozi wengine wa kidini katika Chile, wengi wao ambao walifukuzwa watoke katika nchi hiyo. Kama vile mmoja wa kikundi hiki alivyolalamika: “Wao [serikali mpya ya kijeshi] wanatulaumu kwa kuleta uadui kati ya jamii nchini.” Wawe wanakubali shtaka hilo ni la kweli au sivyo, je! viongozi wa kidini wanaweza kukana kwa uaminifu kwamba wao hawakuwa wamekuwa wakijitia katika siasa kuliko kuuhubiri ufalme wa Mungu? Ni kwa sababu ya matendo hayo kwamba wao wamejiacha wafanyiwe shtaka walilofanyiwa.

Bila ya kujali kama wakuu na kiburi chao wanautetea au sivyo, ufalme wa Mungu ndio mpango wa Muumba wa kuondosha uasi duniani. Likihakikisha jambo hili Neno la Mungu linasema hivi: “Bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo . . . Wewe umngoje [Yehova], uishike njia yake, naye atakutukuza uirithi nchi, wasio haki watakapoharibiwa utawaona.”​—Zab. 37:10, 34.

Katika hiyo taratibu mpya, inayokaribia sana sasa, “haki itakaa.” (2 Pet. 3:13, NW) Hakutakuwa na haja ya kufuli nyumbani pako. Mtu ye yote atakapokaribia, utaweza kuwa na matumaini kwamba utaweza kumkaribisha yeye kama rafiki. Utaweza kutembea peke yako ukitaka, hata usiku bila hofu, ufurahie mlio wa panzi na uzuri wa mbingu zenye nyota huko juu. Kutakuwako usalama wa kweli duniani pote. Muumba wa mbingu na dunia ndivyo alivyoahidi.

Lakini je! wewe utakuwako? Huu ndio wakati wa kujifunza matakwa ya Yehova na kupatanisha maisha yako nayo. Mashahidi wa Yehova watafurahia kukusaidia.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa maelezo zaidi, tazama kitabu God’s Kingdom of a Thousand Years Has Approached.

[Picha katika ukurasa wa 339]

Woga unafanya watu waishi wakiwa wamefunga milango

[Picha katika ukurasa wa 341]

Lo! itakuwa vizuri ajabu wakati ambapo kufuli hazitahitajiwa, wakati ambapo kila mtu ataweza kukaribishwa kama rafiki!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki