Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 12/15 kur. 5-6
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hali Yenye Kusikitisha ya Mpumbavu
  • Upumbavu Unapokuwamo Kati ya Jamii Yenye Kutawala
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Ni Nini Kinachofanya Maisha Yawe Yenye Kusudi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 12/15 kur. 5-6

Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hali Yenye Kusikitisha ya Mpumbavu

Akionyesha tofauti ya matokeo kati ya maneno ya mwenye hekima na yale ya mpumbavu, Sulemani anaandika hivi: “Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.” (Mhu. 10:12) Katika kinywa cha wenye hekima hutoka maneno yanayompa neema na mambo mema mwenye kuyasikiliza. (Linganisha Waefeso 4:29.) Wanayoyasema yanaelekea pia kuitikiwa katika njia inayofaa.

Bali maneno yake mpumbavu yanafanya alaumiwe na kwa hiyo yanamharibu au ‘kummeza.’ “Mpumbavu” ananena maneno ya upumbavu tangu mwanzo mpaka mwisho, mara nyingi akitoa sababu zisizofaa na kufanya maamuzi yasiyofaa. Sulemani anaeleza hili katika njia hii: “Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari. Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?” (Mhu. 10:13, 14) Mpumbavu anafikiri anaweza kufanya hivyo.

Mtu kama huyo anafanya maisha yake yawe magumu katika njia nyingine pia. Sulemani anaendelea kusema hivi: “Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, maana hajui hata njia ya kuuendea mji.” (Mhu. 10:15) Watu wanaoshindwa kufanya maamuzi mazuri huenda wakaendelea kufanya kazi ngumu, wakijichosha, hata hivyo wasiweze kutimiza jambo lo lote lenye maana ya kweli. Kwa ukaidi wanadharau hata mambo ambayo akili nzuri inapaswa kuwafundisha. Wanakosa kuona hata vitu vilivyo wazi, vitu vinavyoonekana kwa urahisi kama vile barabara kuu ya watu wote inayoenda mjini.

Upumbavu Unapokuwamo Kati ya Jamii Yenye Kutawala

Upumbavu ni mbaya unapoonyeshwa na raia wa vivi hivi. Walakini, watawala wanaposhindwa kutumia akili nzuri na kufanya uamuzi unaofaa, hiyo inaiharibu serikali na kuumiza raia zake. “Ole wako, nchi,” asema Sulemani, “akiwa mfalme wako ni kijana, na wakuu wako hula asubuhi!” (Mhu. 10:16) Hali inakuwa yenye kusikitisha kweli kweli mtawala anapokuwa na tabia kama ya kijana asiye na ujuzi na anapokuwa na wakuu au washauri wasiofanya kazi za serikali. Wakitumia wakati wao wa asubuhi wakila wakati wanapopaswa kuwa wakifanya kazi zao, ufalme utaangamia.

Akionyesha tofauti ya matokeo ya usimamizi mzuri wa mambo ya serikali, Sulemani anaendelea kusema hivi: “Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu [waungwana, kwa hiyo, yeye mwenyewe awe mtawala mwungwana na mwenye hekima], na wakuu wako hula wakati ufaao, ili makusudi wapate nguvu [za kufanya kazi zao], wala si kwa ajili ya ulevi [si kwa kujitoa sana katika ulafi na ulevi].” (Mhu. 10:17) Ndiyo, watawala wenye hekima wanaweza kusaidia sana kuleta furaha ya raia zao.

Usemi wa mithali ambao Sulemani anatumia baada ya hapo unaonyesha kwamba maangamizi pamoja na uharibifu yanatokea wakati kazi ya maana inapoachwa bila kufanywa. Tunasoma hivi: “Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.” (Mhu. 10:18) Nyumba isiyoangaliwa vizuri inaharibika. Paa itainama na kuvuja. Vivyo hivyo uharibifu unatokea mambo ya serikali yasipoangaliwa vizuri.

Wakati huu Sulemani anatoa usemi mwingine wa mithali akisema: “Karamu [chakula] hufanywa kwa ajili ya kicheko [cha wafanya kazi], na divai huyafurahisha maisha; na fedha huleta jawabu la mambo yote.” (Mhu. 10:19) Kula, pamoja na mazungumzo mazuri, kunaweza kufurahisha sana. Walakini, chakula hakiwezi kupatikana pasipo fedha, naye mtu aliye na mambo machache sana ya lazima ya maisha hupata furaha ndogo sana kwa kunywa divai. Katika taratibu hii iliyopo, fedha ndiyo njia ambayo katika hiyo, mambo yote ya kimwili yanaweza kupatikana, na kwa hiyo, “huleta jawabu la mambo yote.” Wazo katika usemi wa Sulemani laweza kuwa kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii mtu anaweza kupata fedha zinazohitajiwa kwa ajili ya chakula na divai, kwa mambo yanayoongeza furaha ya maisha.

Baada ya hapo Sulemani anaonya hivi: “Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo [“chumba chako cha kulala,” NW] lako; wala usiwalaani wakwasi [“matajiri,” NW] chumbani mwako; kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, na mwenye mabawa ataitoa habari.” (Mhu. 10:20) Hata ikiwa mambo ya serikali yanakosa kuangaliwa na jamii inayotawala, hata hivyo mtu mwenye hekima hajihatarishi isivyofaa. Ikiwa haimo katika uwezo wake kusahihisha hali, kungekuwa na faida gani kunung’unika na kulalamika akiwa katika sehemu ya ndani sana ya nyumba? Huenda mtu akafikiri kwamba hakuna mtu atakayemsikia. Walakini, mara nyingine mambo yanajulikana katika njia zisizo za kawaida kabisa na zisizotazamiwa. Kwa hiyo, kwa sababu gani mtu ahatarishe amani na usalama wake kwa kusema mambo yasiyofaa juu ya watu wenye mamlaka? (Linganisha Mathayo 12:36, 37; Warumi 13:1; Tito 3:1, 2; 1 Pet. 2:13-17) Lo! namna linalofaa shauri la Sulemani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki