Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 7/15 kur. 3-5
  • Ni Jambo Gani Linalofanya Serikali Iwe Halisi Kwako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Jambo Gani Linalofanya Serikali Iwe Halisi Kwako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • FALME ZA ULIMWENGU
  • UFALME MWINGINE
  • ALAMA ZA SERIKALI HALISI
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Serikali ya Mungu ya Amani
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Je! Wewe U Raia Mshikamanifu wa Serikali ya Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Kuwa Raia wa Serikali ya Mungu
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 7/15 kur. 3-5

Ni Jambo Gani Linalofanya Serikali Iwe Halisi Kwako?

SASA kunazo nchi 150 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa. Inaelekea wewe unaishi katika mojawapo ya nchi hizi, kwa kuwa watu zaidi ya 4,000,000,000 wanaishi ndani yazo​—kwa kweli idadi ya watu wote wa ulimwengu! Kila moja ya nchi hizi ina namna fulani ya serikali. Je! wewe unajua ni namna gani inayopatikana karibu kila mahali?

Ni jamhuri. United States of America, Misri, Urusi na China zimo kati ya zaidi ya mataifa 100 ya Umoja wa Mataifa ambayo ni jamhuri. Kulingana na Webster’s Third New Intemational Dictionary, jamhuri ni: “Serikali ambayo mkuu wake si mfalme na ambaye katika nyakati za kisasa [kwa kawaida] ni rais.” Tofauti na vile watu wengine wangefikiri, hakuna nchi ambayo leo ni demokrasia ya kweli, ambayo ni “namna ya serikali ambayp mamlaka yake iliyo kuu zaidi yamekabidhiwa watu na kutumiwa nao moja kwa moja.”

Je! serikali hizi​—jamhuri hizi​—ni halisi kwako? ‘Bila shaka,’ huenda ukajibu. Lakini sababu gani? Je! sababu moja si kwamba viongozi wa mataifa haya ni watu halisi? Wanaume kama Rais Carter, Rais Sadat, na Rais Brezhnev majina yao yamejulikana katika kila nyumba. Vilevile, mahali ambako kutoka huko wanaume hao hutawala ni halisi​—Washington, Cairo na Moscow. Matokeo ya maamuzi yao yanawapata, si raia wao wenyewe, bali watu ulimwenguni pote.

FALME ZA ULIMWENGU

Falme ni namna nyingine ya serikali inayopatikana mahali pengi. Kulingana na The World Almgnac, nchi 15 za Umoja wa Mataifa ni falme. Ufalme ni serikali ambayo mtawala wake ni mfalme. Kati ya falme katika Umoja wa Mataifa ni Lesotho, Nepal, Denmark, Sweden, Norway, Yordan, Saudi Arabia na Morocco.

Ni kweli, leo wafalme wengi au malkia ni wa jina tu, kama kwa mfano, katika Denmark, Sweden na Norway. Wafalme katika sehemu hizo wana mamlaka halisi ndogo sana, ikiwa wako nayo. Walakini katika nchi nyingine sivyo ilivyo. Ebu fikiria Yordan, Morocco na Saudi Arabia. Watawala wa nchi hizi ni Mfalme Hussein, Mfalme Hassan na Mfalme Khalid. Wana mamlaka kweli kweli, ijapokuwa hivi karibuni utendaji wa Mfalme Khalid umepunguzwa na ugonjwa mbaya sana.

Je! falme zilizo wanachama wa Umoja wa Mataifa ni halisi kwako? Huenda ukajibu, ‘Ndiyo.’ Ni jambo gani linalozifanya kuwa halisi? Si kwamba tu wafalme ni watu halisi, bali pia zina raia halisi​—Wayordan, Wamorocco na Waarabu wa Saudi. Raia hawa wanatawaliwa kwa sheria fulani, kama kisemavyo World Book Encyclopedia: “Kila kikundi cha watu​—kuanzia na jamaa mpaka taifa​—kina kanuni za mwenendo za kuongoza maisha za washiriki wake.” Sheria hizi, pamoja na utamaduni, lugha na tabia za taifa, mara nyingi ndizo ambazo hufanya watu wa serikali moja watofautiane na wengine.

UFALME MWINGINE

Falme ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa si ndizo falme peke yazo. Ufalme ulio wa maana zaidi kuliko zote si sehemu ya chama hicho cha ulimwengu cha mataifa. Ni jambo gani linaloufanya ufalme huu kuwa wa maana hivyo?

Si idadi ya raia zake, wajapokuwa ni wengi. Ukilinganishwa ni yale mataifa 150 ya Umoja wa Mataifa, sasa ufalme huu una watu wengi zaidi ya mataifa moja moja 42 ya tengenezo hilo la ulimwengu. Ndiyo, una zaidi ya raia washikamanifu 2,100,0001 Walakini katika mwaka wa karibuni, raia hawa, pamoja na rafiki zao, wote pamoja jumla yao ikiwa 5,095,831, walikusanyika katika siku moja katika mikutano ulimwenguni pote kujikumbusha yale ambayo mfalme wao amewafanyia. Hiyo ni hesabu kubwa kweli kweli! Ni mataifa 77 tu ya Umoja wa Mataifa​—kama nusu yao​—walio na idadi kubwa ya watu kuliko hiyo.

Serikali nyingi za ulimwengu zina mipango mizuri ya elimu. Lakini ufalme huu una mpango ulio bora zaidi. Kitabu chake kikubwa cha mafundisho kimeenezwa zaidi katika lugha zaidi kuliko kitabu kingine cho chote cha ulimwengu. Na vitabu kadha ambazo inachapa za kusaidia watu waifahamu Biblia zimo kati ya vitabu 10 vya ulimwengu ambavyo vimeenezwa zaidi kuliko vingine vyote. Kuongezea hayo, kila mwaka raia zake huchapa na kuenza mamia ya mamilioni ya vitabu, kama hivyo vya kuelimisha watu pamoja na vijitabu na magazeti. Wanakuwa na madarasa matano kila juma, katika vikundi zaidi ya 40,000 kuuzunguka ulimwengu, ambako wanajifunza sheria za serikali hii na kutiana moyo waitii.

Serikali hii ya ufalme ni serikali gani?

Katika unabii wa kale juu ya yule ambaye angekuwa mtawala wake, Biblia yasema hivi: “Kwa kuwa.kwetu sisi mtoto amezaliwa, kwetu sisi tumepewa mwana; na serikali itakuwa begani mwake: na jina lake litaitwa Ajabu, Mshauri, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mwana wa Kifalme wa Amani. Hakutakuwa na mwisho wa ongezeko la serikali yake na la amani.”​—Isa. 9:6, 7, American Standard Version.

Huenda ukaufahamu huo kuwa unabii kuhusu Yesu Kristo. Kabla ya kuzaliwa kwake, Malaika Gabrieli alimwambia mama yake Mariamu hivi: “[Yehova] Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. [Naye atatawala kama mfalme], . . . na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.” (Luka 1:32, 33) Yesu alipokua akawa mwanamume mzima yeye alitumia maisha yake yote katika faida za serikali hiyo.

Pindi moja Yesu alipaza sauti hivi: “Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa.” (Luka 4:43) Yesu hata aliwafundisha wafuasi wake kuiombea serikali hii: “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”​—Mt. 6:9, 10.

Je! ufalme huu wa Mungu ni serikali halisi kwako?

Yesu Kristo alisema kwamba ni serikali ambayo ingekuwa na raia washikamanifu. Wakati liwali Mrumi Pontio Pilato alipomwuliza Yesu kama yeye alikuwa mfalme, alijibu hivi: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.”​—Yohana 18:36.

Upesi kabla ya kifo chake, Yesu aliwaambia viongozi wa kidini Wayahudi hivi: “Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.” (Mt. 26:64) Yesu alimaanisha nini?

Alikuwa akitaja unabii wa Biblia wa Danieli juu ya “mwanadamu” aliyeahidiwa ambaye aliletwa mbele za “mzee wa siku,” Yehova Mungu. “Naye akapewa jnamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote wamtumikie.” (Dan. 7:13, 14) Hiyo inaonyesha kwamba Yesu Kristo aliyefufuliwa angetawala mbinguni, na kwamba mamlaka yake kama mfalme yangekuwa juu ya dunia.

Lakini kwa kuwa u’falme wa Mungu ni wa mbinguni​—mtawala wake Yesu Kristo akiwa sasa haonekani​—wengi hawaioni kuwa serikali halisi. Hata hivyo, kama tulivyokwisha kuona, kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba ni halisi.

ALAMA ZA SERIKALI HALISI

Kama ilivyokwisha tajwa, ushuhuda mmoja mkubwa wa serikali halisi ni kwamba iwe na raia. “Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake,” yasema Biblia. (Mit. 14:28) Vilevile inakuwa na sheria ambazo hutekelezwa, pamoja na namna fulani ya mpango wa elimu. Je! ufalme wa Mungu una alama kama hizo za serikali halisi?

Ndiyo, tumeona kwamba inazo. Jamii nzima yenye watu zaidi ya milioni mbili ulimwenguni pote imezikubali sheria za Biblia kuwa katiba yao, ziwe ndizo sheria za kuongoza maisha zao. Watu hawa wanachukua jina la Mfanyasheria aliye Mkuu, wakijiita Mashahidi wa Yehova. (Isa. 33:22; 43:12) Katika makundi ya Kikristo ya Mashahidi wa Yehova duniani pote, wanazitii sheria za ufalme wa Mungu.

Wajapokuwa wanaishi katika nchi nyingi ulimwenguni pote, na kusema lugha nyingi na kuwa na utamaduni unaotofautiana, raia hawa wa Ufalme wana umoja wa ajabu sana. Wanasema “lugha iliyo safi” ya kweli ya Biblia yenye kuunganisha.. (Sef. 3:9) Katika kuyatii maagizo ya Mfalme wao, hawashiriki sehemu yo yote katika mambo ya siasa au vita vya mataifa ya ulimwengu. (Yohana 17:16; 18:36) Katikahili, wanashikamana vilevile na amri ya Mfalme wao kwamba “[rawe] na upendo ninyi kwa ninyi,” hivyo wanatambuliwa kuwa wanafunzi wake.​—Yohana 13:34, 1 Yohana 4:20, 21.

Wakati unapofikiria mambo ya hakika yanayoifanya serikali iwe halisi, inakuwa wazi kwamba ufalme wa Mungu unazo alama zote za serikali kama hiyo. Ni jambo la maana sana kwetu, si kwamba tu tukubali uhakika huu bali pia tuwe wategemezaji watendaji wa serikali hiyo ya mbinguni.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki